Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 64
Narudia tena...Sikuambiwa hiyo ni sababu...Lakini pia iliibuliwa,na niliwaomba msamaha kwa kutumia lugha hizo.
Hata hivyo wana jf waliniombea msamaha na sasa niliwashukuru Wana jf/Mods na mjadala unaendelea!
Una hakika kuwa umesamehewa ... kwi kwi kwi
NB:Maswali mawili muhimu ambayo unakwepa bado..
Tofauti yangu na wewe, mimi najibu maswali yako lakini wewe hujibu yangu. Natumaini baada ya hili utaanza kujibu maswali yangu.
1)Kwanini ulihojiwa na FBI kuhusu kifo cha ballali.
Sijawahi kuhojiwa na FBI kuhusu kifo cha Ballali, Ila nimewahi kwa utashi wangu mwenyewe kupiga simu FBI na kuongea nao kuhusu kifo cha Ballali.
2)Kwanini ulisema Kikwete apewe mwezi kwasababu kuna kitu kikafanyika na miezi imepita bila ya wewe kusema ni nini hasa ulichokuwa ukikifahamu!Hata hivyo sisi tunajua ballali alipotea!
Niliposema kuwa Kikwete apewe mwezi mzima, mambo mengi sana yalitokea ikiwemo chuo ninachosoma hapa US kikamaliza muhula wa spring. Je katika hilo nalo nina mkono?
Nilimpa Kikwete muda kufanya kazi na sikumpa muda kwa vile aliahidi kufanya kazi (kama unajitaji nikuletee thread yangu basi nitaileta hapa tuichambue).
3)Hujasema ni kwanini wewe na SINCLAIR MNA RIPOTI KABLA YA WANANCHI KUWA NAYO!
Hata report ya E&Y na zile zingine zote ikiwemo mkataba wa Buzwagi nilizipata kabla wananchi hawajazipata na ninaziweka hapa. Je kuna makosa kuwa na siri za serikali na kuziweka hapa JF?
Tuanze na hayo...
Nitashukuru kama huta SPIN!
Umeridhika?
Kama bado uliza upate ufafanuzi zaidi na ujiandae sasa kujibu maswali yangu.