Mwamtetea bure... ukiangalia anachokifanya Mushi pamoja na kuonekana ni mwanamapinduzi, kuna walakini mkubwa sana ambao unaonyesha dhumuni lake si kuleta hamasa ya Uanaharakati au Mapinduzi bali ni kuchochea vurugu ambayo inaweza kufikia kijiwe kufa.
Sitakuwa msiri kubainisha nahisi Mushi katumwa kwa makusudi kuleta vurugu humu kwa niaba ya wale ambao tangu awali walitaka kuua JF tangu kule Jambo Forum na sasa hapa JamiiForum.
Wengi tunapingana hoja, kuna wale wa CCM, kina Kada Mpinzani na wengine, kuna wanaopingana kuhusiana na Dataz, kina Kubwajinga, hata ndugu yangu Kuhani.
Lakini wote wale watetea Serikali au wakosoaji wa Serikali, hatujafikia hatua za Mushi ambazo zinaonekana kuwa ni uropokaji bila mpango.
Akiulizwa swali badala ya kujibu swali, huzua jambo, ataruka kama panzi kutoka thread moja mpaka nyingine akilizungumzia jambo lile lile na kuzua mapya.
Kuhani alijaribu sana kuwa Wakili kwa Mushi alipofungiwa, lakini naona si mbali sana wema wa Kuhani utafika kikomo.
Sisi tunaupenda huu ukumbi, ndio maana Mchungaji leo yupo tayari kubishana hoja na Kuhani, FMES, Game Theory, Kada Mpinzani, Mwafrika wa Kike katika kuelimishana.
Hii thread ilikuwa ni kuhusu Kikwete kupokea ripoti ya madini, kaletwa Anna Killango kuwa analinda ufisadi, wametuhumiwa kina Iddi Simba mpaka Zitto kusema wanalinda ufisadi wa EPA.
Sasa tunapokuwa na mchafuzi ambaye ishara zote zinaonyesha kuwa nia yake ni kuleta vurugu mnataka tukae kimya?
Mbona tunamvumilia Kada Mpinzani na UCCM wake pamoja na kuwa tumeichoka CCM?
Mushi is an exceptional character, na matendo yake kila siku yananifanya nijiulize, je huyu ana nia nzuri na JF au katumwa kuvuruga JF ili kina Invisible waanze kulala nyumba tofauti kila siku na hata credibility ya JF ikapotea?