Wewe na huyo profesa mna walakini katika kuelewa athari ya serikali kukopa mabenki ya ndani. Kwanza Duniani kote serikali ikianza kukopa kwenye mabenki ya ndanì, huongeza inflation.
Pili huyo prof na wewe mpo mbali kuuelewa uhalisia. Hakuna bank hapa ndani yenye uwezo wa kuikopesha serikali trillion 2. Haipo! CRDB wamechukua mkopo wa zaidi ya dola 260m toka ADB ili kupata uwezo wa kuwakopesha wateja, hiyo ndiyo serikali inaikodolea.
Mzunguko wa pesa hunawiri zaidi pale bank inapowakopesha wafanyabiashara/wawekezaji kuliko inapoikopesha serikali. Serikali inaweza kukopa hiyo hela yote dola 260m kwaajili ya mradi mmoja ambao upo Dar, wakati pesa hiyo hiyo inaweza kukopeshwa kwa wafanyabiashara zaidi ya 50 waliotapakaa nchi nzima. Watu binafsi hupata bidhaa zao kutoka kwa wauzaji mbalimbali wakati serikali hutumia supplier mmoja tu