Hatimaye fedha kurudi mitaani

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,767
239,437
Muhadhiri wa chuo kikuu cha Dar - es salaam, Dr. Joel Silas ameelezea matumaini yake kuwa mpango wa serikali wa kukopa kwenye benki za biashara za ndani utarudisha fedha zilizoadimika mitaani kwa sasa hatimaye .

Kwamba hatua hiyo itarudisha fedha iliyopotea mitaani kwa sababu itasaidia kuimarisha mzunguko wa fedha kwenye uchumi .

Chanzo - Nipashe .

Mytake - Elimu ni ufunguo wa maisha .
 
kwa serikali kukopa za ndani ni kuondoa hata zile chache zilizopo mitaani kwakuwa baada ya kukopa serikali inapeleka bank kuu kama ifanyavyo kwenye makusanyo ya mapayo.maana yake hela zitapungua zaid ya sasa kwakuwa serikali saiz inaweka fedha zake bank kuu.na sio bank binafsi ambazo wafanyabiashara na watu wengine wanachukua mikopo na hela kurud kwenye mzunfuko.
 
Imekuwaje tena nje hatukopesheki! au umeshaingia katika sifa ya kundi lisilokopesheka.
Nahisi kama tunaingia kwenye joto zaidi,mzunguko wa fedha hivi sasa umekuwa mgumu baada ya serikali kuamuru taasisi zake kuhifadhi fedha hazina na hivyo kuzuia kuingia kwenye mzunguko na sasa hizo zilizobaki wanazikopa kisha wanaenda kuzihifadhi hazina.
 
Khaa udsm kaz mnayo yaan huyo ndio dokta wa uchumi yaan serikali ikope hela kwa. Commercial bank halaf mzunguko wa fedha uongezeke!

Simple tu ni kwamba itaongeza ukata sababu benki zitaacha kuwakopesha wananchi sababu serikali inakopa kwa riba kubwa na ukopeshaji huu hauna hasara kwa kuwa serkali hulipa kwa wakati

Pia serikali inakopa pesa kwenye mabenki halafu inakwenda kununua ndege kama siyo kuweka malumbesa BOT

Mwisho pesa nyingi itakuwa kwenye mikono ya serikali hivyo wananchi mjifunge mikanda maana hamtapata mikopo kutoka benki mungu ibarik Tanzania
 
Nachukia sana taarifa kama hizi. Umeamua kutoa habari somewhere kuwahabarisha wenzio unaleta heading tu. Hii hata vichwa vya habari kutoka redioni tumesikia so nilifikiri hapa ungeleta "nyama" zaidi juu ya hii habari
 
Nauliza hii 18% vat kwenye Airtel money na kununua salio inakwenda wapi na je tunamkomoa nani kati ya wanavijiji na wale wenye uwezo wa kupata kipato kila mwezi? Vat kubwa kuliko interest za banks?? Au ndo mwanzo wa pesa kurudi kitaa?
 
Sio kila Mhadhiri ana akili sawasawa.

Kukopa kwa serikali kwenye Bank za ndani kunarudisha vipi pesa kwenye mzunguko??

Kila mwezi serikali inakusanya (kama ambavyo wamekuwa wakituaminisha) 1Tril +, kwanini kwa kipindi chote hicho hizi zisitumike kurudisha pesa kwenye mzunguko??

Naona huyu Mhadhiri anatafuta kuteuliwa, maana wateule wengi siku Hizi ni wahadhiri.
 
Huyu atakuwa ni professor maji marefu huyo professor gani anaongea upuuzi kiasi hicho ....

Yaani Serikali ikope kuwalipa wachina pesa wazipeleke China wajenge Reli halafu useme pesa itaingia kwenye mzunguko?

Tanzania inatumia mzunguko wa wakandarasi wa china..

Labda kama wanakopa kuwalipa wafanyakazi hapo sawa........
 
Kunawakati wasomi wetu ni janga kuliko kawaida wasomi badala ya kupeleka ushauri namna ya kunusuru uchumi anashangilia serikali kukopa

Elimu haina mwisho ila mawazo ya binadamu yana ukomo nae huyu msomi wetu mawazo yake ndo yalipo ishia
Hakuna nchi isiyokopa duniani
 
Muhadhiri wa chuo kikuu cha Dar - es salaam, Dr. Joel Silas ameelezea matumaini yake kuwa mpango wa serikali wa kukopa kwenye benki za biashara za ndani utarudisha fedha zilizoadimika mitaani kwa sasa hatimaye .

Kwamba hatua hiyo itarudisha fedha iliyopotea mitaani kwa sababu itasaidia kuimarisha mzunguko wa fedha kwenye uchumi .

Chanzo - Nipashe .

Mytake - Elimu ni ufunguo wa maisha .
Wapiga Dili wanahaha Kama Mapaka ya Rose Garden mkuu.
Mytake: Maisha ni Ufunguo wa Elimu.
 
Back
Top Bottom