Mbona hujaelewa tu hiyo simple logic. Kazi ya benki ya kibiashara ni kuweka pesa za wateja ambao hawana kazi ya kuzifanyia pesa hizo wakati huo. Benki hiyo huwakopesha watu ambao wana kazi za kufanyia hizo pesa. Wanaokopeshwa huilipa benki hiyo riba kubwa, kwa mfano 20% kwa mwaka. Benki inamlipa yule aliyeweka pesa yake riba ndogo, kwa mfano 2% kwa mwaka, hivyo benki inapata faida ya 18% kwa mwaka kwa wewe kuweka pesa yako benki na benki kukopesha pesa yako kwa wengine wakaifanyie kazi. This is the buisness of all commercial banks.
Pesa ikichukuliwa na aliyeikopa anaenda kuifanyia kazi. Kwa mfano atajenga hoteli, ataajili watu na kutoa huduma. Atanunua vyakula, vitapikwa na kuuzwa. Hivyo pesa hiyo itaingia kwenye mzunguko. Waliojenga hiyo hoteli watapata pesa wakiwemo mafundi, vibarua, mama ntilie, wauza vifaa vya ujenzi, viwanda vya vifaa vya ujenzi, ma transporters wa vifaa vya ujenzi na hata bodaboda. Akianza kutoa huduma ya hoteli wauza nyama, samaki, maziwa, kuku na vyakula vingine watapata hela. Vivyo hivyo wazalishaji wa hivyo vyakula wakiwemo wakulima, wavuvi na wafugaji watapata hela pamoja na wasafirishaji wa hivyo vyakula. Huo ndio mzunguko wa fedha unaoletwa na benki kukopesha fedha. It is a long chain, directly ana indirectly.
Sasa serikali ikisema itakopa trilion 2 kutoka kwenye benki hizi za biashara kwenda kutekeleza miradi yake ya maendeleo huoni kuwa hiyo ni neema? Benki lazima zitachekelea maana zimepata mkopeshwaji mkubwa mwenye uhakika. Serikali ikichukua hela hizo itaenda kujenga barabara, reli na miundo mbinu zingine nyingi kama zilivyoainishwa kwenye bajeti ya maendeleo. Hivyo pesa hiyo itaingia kwenye mzunguko huo huo nilioutaja hapo juu tena kwa kiwango kikubwa zaidi ya yule mkopaji binafsi mmoja mmoja. Wote wakakaohusika na hizo kazi za maendeleo directly or indirectly watajaa pesa. Hivyo kila mtu anayefanya kazi halali ataipata hiyo pesa ambayo ataiingiza kwenye mzunguko mitaani kwake na benki zetu za biashara zitapata hiyo riba zake za kukopesha kwa uhakika. Hakuna cha risk ya kutorejesha mkopo kama ilivyo kwa wakopaji binafsi.
Hiyo ndiyo logic ambayo professa amejaribu kuwaeleza, hamkumuelewa na badala yake mnajiona mnajua kuliko profesa. Si vizuri mnachofanya. Kitu kama hujaelewa uliza tu ueleweshwe.