Hatimaye Dr. Slaa aonekana, asema kuzungumza muda ukifika

Hatimaye Dr. Slaa aonekana, asema kuzungumza muda ukifika

Kaonekana kwani alipotea? mbona mlikuwa hamjaripoti polisi atafutwe? bavicha bana akili zenu mnazijua wenyewe.
 
View attachment 273790

View attachment 273791

Mbunge mstaafu wa Moshi Mjini, Mzee Philemon Ndesamburo, maarufu kama "Ndesa Pesa", amekutana jijini Dar es Salaam leo na Katibu Mkuu wa CHADEMA ambaye ilielezwa hapo awali na chama chake kuwa kwa sasa yuko mapumzikoni, Dkt. Wilbrod Slaa, nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.

Ndesamburo alifuatana na makada wenzake wa chama hicho, baadhi yao ni Meya wa Manispaa ya Moshi ambaye pia ni mgombea ubunge (mtarajiwa), wa jimbo hilo, Japhary Michael.

Hakuna taarifa yoyote iliyotolewa ya nini wamezungumza, ingawa makada hao wa CHADEMA walikuwa jijini kuhudhuria mkutano mkuu maalum wa chama hicho uliomteua Waziri Mkuu wa zamani Mhe. Edward Lowassa, kuwa mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya mwavuli wa muungano wa vuguvugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi, UKAWA. Mgombea mwenza aliyeteuliwa ni Mhe. Juma Duni Haji.


Mh. Dr. Slaa tupo nyuma yako. Baba tumslize vita kwanza ya nyumbani tutayarudia na kuyamaliza. Adui yetu ni ccm tusianze tena vita ya wenyewe kwa wenyewe! Tutafhoofika!!!
 
Niliipenda CHADEMA kwasababu ya Dr Slaa na Zitto,basi.

Mmmmmh mkuu kwa hayo mapenzi binafsi unatia shaka. Ila wenye akili na wa ukweli wanakipenda chama kutokana na Sera na itikadi zake
 
Kama hamuamini basi hebu tajeni jina la mtu wa kwanza kushoto

Hii picha ya kitambo sana

hii ni ya leo maana hata iyo t-shirt walizovaa jana inaonekana anyway simlaumu dr alipumzika kupata akili mpya ya kushinda nguvu ya matarajio ya uraisi iliyokuwa ikikinzana kwenye akili yake. nadhani atarudi ulingoni kujenga chama

Picha hii ni current? ... Mbowe amewiva kisiasa ... Slaa anafifia kifkra japokuwa anahitajika kwaajili ya kuhakikisha CCM wanaingia kaburini coming October ... Shuntama la Josephine balaa ...

Ya leo au ya miaka? Naona Mzee Ndesa Pesa
 
h. Dr. Slaa tupo nyuma yako. Baba tumslize vita kwanza ya nyumbani tutayarudia na kuyamaliza. Adui yetu ni ccm tusianze tena vita ya wenyewe kwa wenyewe! Tutadhoofika😛hoto:!!!
 
Ahsante Mungu. Sasa kazi awamu ya kwanza imekwisha. Ccm imezikwa rasmi. Tuanze kujipanga na ujenzi wa taifa imara la Watanzania!. Ahsante Bwana Yesu!.

Lizabon: au ccm yeyote, kabla hatujaendelea, una swali la nyongeza???

..........................................................................................................
.........................................................................................................

Kimya maana yake umeridhika. Haya tunasonga mbele. Mwambie JK aache kupaniki na kuhalalisha msemo wa Nape wa kufunga hata kama kwa mkono.

Huko golini hafiki na hawezi kufunga goli letu kutokea Lumumba. Aanze kuwaandaa wana ccm kukabidhi nchi kwa amani kwa kuwa hatutakubali tamaa zenu za madaraka kutuharibia nchi. Wakti huo huo, anzeni kuondoa personal items ofisini kwetu. Wenyewe wanakuja!.

Tena mwambie, ni afadhali akubali mabadiliko ili ayaongoze kuliko kujidai hayatambui halafu yaje yambadilishe bila ridhaa wala maandalizi. Hayo ni mafuriko hayajawahi kushindwa popote.


Haya ujumbe wa leo ni huu!.

Unakila dalili ya ugonjwa wa kipindu pindu...

Maanake huu ushuzi unaoumwaga sio mchezo
 
Humu kuna watu wabushi hata ukiwaambia hii ni Jamii forum watabisha....picha za Leo hizo angalia mavazi Yao....viva uKawa.
 
Josephine mbona kama anataka kushika dyudyuu ya Ndesa Pesa??????
 
Huna la kutuambia wewe nyani mzee,nenda Lumumba kamalize kwanza songombingo la kura za maoni,nyani we
Mmawia pole Mangi wangu umemfuata Nicholas?
unatumia nguvu nyingi kujieleza na matusi juu hatimaye wamekuminya
sasa unakuja kwa gia za kuchungulia km Janson Barne
attachment.php

Hii ppicha ni ya zamani
kani huyo wa katikati kushoto kwa Dr Slaa ni Lucy Owenya na kwa sasa hajavaa wigi Mkutano wa jana nywele ni ina tupu na huyo Jafary Meya hakuwa na gwanda
kilichopo ni kuwa Dr yupo salama na tumuombee
si mchezo kuwatumikia watu miaka 20 leo wanakufyeka bila kujijua
 
Last edited by a moderator:
Ahsante Mungu. Sasa kazi awamu ya kwanza imekwisha. Ccm imezikwa rasmi. Tuanze kujipanga na ujenzi wa taifa imara la Watanzania!. Ahsante Bwana Yesu!.

Lizabon: au ccm yeyote, kabla hatujaendelea, una swali la nyongeza???

..........................................................................................................
.........................................................................................................

Kimya maana yake umeridhika. Haya tunasonga mbele. Mwambie JK aache kupaniki na kuhalalisha msemo wa Nape wa kufunga hata kama kwa mkono.

Huko golini hafiki na hawezi kufunga goli letu kutokea Lumumba. Aanze kuwaandaa wana ccm kukabidhi nchi kwa amani kwa kuwa hatutakubali tamaa zenu za madaraka kutuharibia nchi. Wakti huo huo, anzeni kuondoa personal items ofisini kwetu. Wenyewe wanakuja!.

Tena mwambie, ni afadhali akubali mabadiliko ili ayaongoze kuliko kujidai hayatambui halafu yaje yambadilishe bila ridhaa wala maandalizi. Hayo ni mafuriko hayajawahi kushindwa popote.


Haya ujumbe wa leo ni huu!.

JK alishawaambia wana CCM wenziwe kitambo kuwa, WAJIANDAE
KISAIKOLOJIA; alimaanisha wajiandae kukabidhi serikali kwa upinzani. Wenye kumbukumbu wanalijua hilo. Ukisema wa nini, wenzio wanasema watampataje? Akichukuliwa unaanza kulia, ooh! makapi!! Tulieni mmwagiwe!! Si mmechezea koki? Lazima mlowe.
 
Mnaosema picha hii ya zamani, kwan mmeambiwa Dr. Slaa alikua mgonjwa, na hawezi kuwa hivyo? Yupo na ataendelea kuwepo CDM
 
Jaman mm kweli Dr slaa namuamin anahekima na so mroho wa madalaka. Kwa hiyo naamin atatokaa tuu na amani itatawala chadema Mung ibarki Chadema
 
Mmawia pole Mangi wangu umemfuata Nicholas?
unatumia nguvu nyingi kujieleza na matusi juu hatimaye wamekuminya
sasa unakuja kwa gia za kuchungulia km Janson Barne
attachment.php

Hii ppicha ni ya zamani
kani huyo wa katikati kushoto kwa Dr Slaa ni Lucy Owenya na kwa sasa hajavaa wigi Mkutano wa jana nywele ni ina tupu na huyo Jafary Meya hakuwa na gwanda
kilichopo ni kuwa Dr yupo salama na tumuombee
si mchezo kuwatumikia watu miaka 20 leo wanakufyeka bila kujijua
Naona mnahangaika kukimbizana na upepo.
 
Last edited by a moderator:
Ambacho mtafanikiwa kukifanya ni kumshawishi huyo padri asiingie ktk mikono ya CCM but msitegemee kumpigia kampeni Lowassa..hiyo ni NEVER
 
Humu kuna watu wabushi hata ukiwaambia hii ni Jamii forum watabisha....picha za Leo hizo angalia mavazi Yao....viva uKawa.

Zimeunganishwa hizooooooooooooooo

Angalia intersection ya hao watu
 
Back
Top Bottom