Hatimaye Dr. Slaa aonekana, asema kuzungumza muda ukifika

Hatimaye Dr. Slaa aonekana, asema kuzungumza muda ukifika

RUCCI

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
1,702
Reaction score
1,716
slaa2.jpg

Mbunge mstaafu wa Moshi Mjini, Mzee Philemon Ndesamburo, maarufu kama "Ndesa Pesa", amekutana jijini Dar es Salaam leo na Katibu Mkuu wa CHADEMA ambaye ilielezwa hapo awali na chama chake kuwa kwa sasa yuko mapumzikoni, Dkt. Wilbrod Slaa, nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.

Ndesamburo alifuatana na makada wenzake wa chama hicho, baadhi yao ni Meya wa Manispaa ya Moshi ambaye pia ni mgombea ubunge (mtarajiwa), wa jimbo hilo, Japhary Michael.

Hakuna taarifa yoyote iliyotolewa ya nini wamezungumza, ingawa makada hao wa CHADEMA walikuwa jijini kuhudhuria mkutano mkuu maalum wa chama hicho uliomteua Waziri Mkuu wa zamani Mhe. Edward Lowassa, kuwa mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya mwavuli wa muungano wa vuguvugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi, UKAWA. Mgombea mwenza aliyeteuliwa ni Mhe. Juma Duni Haji.


Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Moshi Mjini (Chadema), Philemon Ndesamburo (wa pili kulia) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Japhary Michael (kushoto) na viongozi wengine wa chama hicho walipomtembelea Slaa nyumani kwake Dar es Salaam jana.

Dar/Moshi. Siku tatu baada ya Baraza Kuu la Chadema kuridhia kumpumzisha kwa muda Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa baada ya kutofautiana na Kamati Kuu kwa kumkaribisha waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kiongozi huyo amesema yupo salama na wakati mwafaka ukifika atazungumza ya moyoni.



Akizungumza kwa mara ya kwanza na gazeti hili tangu Chadema imkaribishe Lowassa na hatimaye kumpitisha kuwania urais kupitia muungano wa Ukawa, Dk Slaa alisema amekuwa akisikia mengi yakisemwa juu yake lakini yote yamekuwa yakimchekesha tu.

Hakuhudhuria vikao muhimu vya chama hicho na vile vya Ukawa, vikiwamo; wakati Lowassa akitambulishwa rasmi, akichukua fomu, kikao cha Baraza Kuu na juzi Mkutano Mkuu na hakuwa akipatikana kwa simu yake ya mkononi.

Wakati kimya kikitawala juu ya hatima yake, baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiandika kuwa amejivua uanachama Chadema.

Lakini jana alisema: "Naangalia mambo mengi yanayoendelea kwenye mitandao halafu ninacheka tu, usifikiri sifuatilii, nafuatilia kinachoendelea na ninabaki nikicheka."

Kuhusu hatima yake kisiasa na madai ya kujiuzulu uanachama ndani ya Chadema, alisema hawezi kuzungumza lolote kwa sasa na atafanya hivyo wakati mwafaka ukifika. "Usijali wakati wangu wa kuzungumza ukifika nitasema tu, sasa hivi nawaachia mzungumze, lakini nitazungumza," alisema.

Kadhalika, alipoulizwa kuhusu taarifa zilizozagaa kuwa maisha yake yapo hatarini kwa kuwa anatishwa, Dk Slaa alisema hata hilo pia atalizungumzia wakati mwafaka ukifika.

"Ndiyo hayohayo ninayosema, wala msijali nitazungumza wakati ukifika," alisema na kusisitiza: "Nipo salama."

Dk Slaa alisema kwa sasa yupo mapumzikoni nje ya jiji la Dar es Salaam ingawa hakutaka kueleza ni eneo gani.

Juzi, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alifafanua tofauti iliyojitokeza kati ya Kamati Kuu ya Chadema na Dk Slaa wakati wa mchakato wa kumpokea Lowassa.

Katika mkutano huo wa Baraza Kuu la Chadema, Mbowe alisema wamekubaliana katibu mkuu huyo apumzike kwa muda... "Nina hakika kwa tabia na hulka za Dk Slaa… kwa sababu anajua tunampenda na yeye anakipenda chama hiki, tunamwombea kwa Mungu ampe nguvu na ujasiri wa kuona kwamba kauli ya wengi ni kauli ya Mungu."

Ndesamburo na siri nzito

Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo na makada wengine wa Chadema, jana walikwenda kuonana na Dk Slaa nyumbani kwake na kufanya naye kikao cha faragha.

Picha zilizomuonyesha Ndesamburo akiwa na Dk Slaa na makada wengine akiwamo Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Jaffar Michael, zilisambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii jana na kuibua mijadala.

Baadhi ya waliochangia mijadala hiyo walidokeza kuwa huenda Ndesamburo anayeheshimika ndani ya chama hicho alikwenda kujaribu kusawazisha hali ya mambo.

Mkuu wa Idara ya Habari wa Chadema, Tumaini Makene alikiri kuwa picha hizo ni halisi, baadhi zilipigwa juzi na nyingine jana mchana, lakini hakutaka kuingia undani wa mkutano wa wanasiasa hao.

Ndesamburo alithibitisha kukutana na Dk Slaa: "Ni kweli tulikwenda, kwani kuna tatizo gani? Si mzee mwenzangu? Halafu bado ni mwanachama wetu, hajatoka Chadema, hivyo tuna kila haki ya kwenda kumsalimia."

Alipoulizwa kama alikwenda kumsihi Dk Slaa arejee kuendesha mapambano ya kuing'oa CCM, Ndesamburo alisisitiza kuwa walikwenda kumsalimia.

Michael alipoulizwa nia ya safari hiyo alijibu kwa kuuliza; "Dk Slaa ni katibu mkuu wetu kwani tunazuiwa kwenda kumsalimia?"

Dk Slaa aligombea urais mwaka 2010 na kushika nafasi ya pili baada ya Rais Jakaya Kikwete na ndiye aliyekuwa akitajwa kuwania tena nafasi hiyo kupitia Chadema na Ukawa kabla ya "kubadili gia angani" na kumteua Lowassa.

Chanzo: Mwananchi
 

Attachments

  • slaa1.jpg
    slaa1.jpg
    26.2 KB · Views: 24,208
hii ni ya leo maana hata iyo t-shirt walizovaa jana inaonekana anyway simlaumu dr alipumzika kupata akili mpya ya kushinda nguvu ya matarajio ya uraisi iliyokuwa ikikinzana kwenye akili yake. nadhani atarudi ulingoni kujenga chama
 
Back
Top Bottom