HATARI: Zama za Wakatoliki kuendelea kutubu mbele ya Padri zimepitwa na wakati

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,131
35,173
Zama za kiimani kwa Kanisa Katoliki zimebadilika, maisha ya waumini na Mapadri ndani ya Kanisa Katoliki yamebadilika, na mifumo ya kimaisha imebadilika.

Sio siri tena, Kutubu mbele ya Padri kwa sasa kumekuwa sumu ya kuwaumiza waumini au kitendawili chenye kukosa majibu.

Kiapo cha Upadri kutunza siri za waumini kimepoteza mwelekeo, Mapadri wamekosa uaminifu mbele ya waumini na mbele ya jamii, imani na amani baina yao haipo tena. Muumini anazini, padri naye anazini nani wamkutubisha mwenzie.

Muumini ametoa mimba na Padri amebaka mtoto anayemfundisha komunio, nani akatubu kwa mwenzie?

Muumini anayetafuta msaada wa kuokoa ndoa yake kwa kumwambia Padri naona alivyokosea, Padri anatumia mwanya huo kuzini na mkewe.

Sasa huu ndio wakati muafaka zaidi kwa kila mtu kwenda kutubu kwa Mungu wake ili kila mtu apambane na dhambi zake kwa muumba wake?
 
Pentecostal and born again churches zinafanya Ukatoliki kua dini outdated vijana wengi na wanawake wamakamu wote wanahama Katoliki kuenda ulokole, hizo dini ni pingo kumbwa kwa uhafidhina wa katoliki in 50yrs Ukatoliki utapungua sana au utabadili jinsi ya kuendesha ibaada zao na kuacha baadhi ya misimamo yao.
 
Na sisi wakatoliki hatuna shida.

Hakuna dhambi ambayo itakua Ngumu kutubu, kwani Dhambi ni kuvunja kusudi Amri ya Mungu au kanisa.

Mfano ukisema nilizini Unadhani padre atakuuliza na nani?

Na sidhani kama wewe ni mkatoliki, ungekuwa Mkatoliki Ungeelewa kuwa sakrament ya kitubio iliwekwaje wekwaje.
 
Samahani kwa ntakayoyasema hapa hii inanihusu na nasema ukweli

Nakumbuka kuna kipindi nilikua napenda sana masuala ya upadre hususani ubraza na yale maisha ya utawa vile mapadri wanavyoishi yaan nilikua napenda sana ilinivutia kuona wale mabraza jinsi wanavyovaa na kupendeza zile nguo zao za kimisionari.

Basi nikaenda kuomba kuanza kujifunza kusimamia kanisani pale mbele, enzi hizo nakumbuka nilikua mdogo sana nilikua km na miaka 7/8 hivi nilimwambia mzee mimi napenda sana kuhudumia kanisani mzee akakubari ila kipindi hicho mzee alikua busy sana kukaa nae mezani ilikua imezidi sana dakika 5 yeye ni mtu wa kazi na kazi na yeye muda wa kukaa na sisi labda wiki end.

Basi nikapeleka barua kwenye jumuiya kutoka kanisani ikaenda ikasainiwa na mwenyekiti safi nikarudisha kanisani nikaanza mafundisho ya kutumikia, I am telling you niliweza kuhudhulia wiki moja tu narudia tena nilihudhulia mafunzo ya kutumikia wiki moja tu baada ya hapo nilikaa pembeni mwenyewe yaani niliacha mwenyewe bila kulazimishwa na mtu.

Mzee aliponiona sihudhurii tena yale mafundisho akaanza kunihoji vipi mboni hauendi tena kujifunza kutumikia kanisani, umeacha? Nikamwambia mzee nimegairisha sitaki tena kusikia habari za kutumikia kanisani, kuanzia hapo nikaanza kuchukia zile habari za kutumikia na wale mabraza pamoja na wale wanaotumikia kanisani nikawa siwakubari tena km jinsi nilivyokua nawakubari pale mwanzo kabla sijajiunga na mafundisho ya kutumikia kanisani.

Niliona nini? Hio ni Siri yangu.
 
Kanisa Katoliki kufa ni ndoto za mchana.

Makanisa mengi yalikuja na kuondoka, lakini lenyewe mpaka leo karne na karne lipo.

Hata Paulo na Petro mifupa yao iliyolala pale Vatican ukiwaambia kanisa la Roma litakufa watakushangaa.

Very vingine tuwe tu realistic.
 
Kanisa lolote au msikiti linapokosa taratibu na miiko yake linakuwa halina tofauti na kikundi cha wanaojiuza usiku, manake wao terms zinatengenezwa hapo hapo.

Hizi nguvu za makanisa mengine kupambana na Roma zingeelekezwa kupambana na Shetani hakika pengine Mwovu angekuwa ameshatoweka, na sasa ni historia.
 
Tatizo kubwa Sana.

Usimuabudu binadamu.

Binadam hatuaminiki na sio wakamilifu na watakatifu, kwanini ukamtubie mtu et akuombee.. Nonsense kabisa.

Dini uchafu umezidi sana tulio na neema ya kujua Mungu anataka Nini huwezi kusumbuka na Dini.

Hi yote inatokana na ujinga na umasikini lazima utakuwa mtumwa wa dini.

Ukiamini huko utapata baraka, miujiza, kwenda mbinguni (wakati unafanya mabaya hiyo mbingu gani) kupona magonjwa (mengine ni sababu ya afya na lishe duni, kazi ngumu n.k badala ya kwenda hospital unaenda kanisani ukiona bado unaenda kwa waganga au unakuwa unafanya vyote kwa pamoja yaani unafiki).

Viongozi wa dini nao ni tatizo kuwakalisha waumini muda wote kanisani ili wapate pesa, uzinzi, hawafundishi watu kuishi maisha mema na kutenda wema kwa wengine. Wanacho waza ni vipi michango itolewe n.k

Watanzania ujinga na umasikini unatupeleka pabaya sana.
 
Niliona nini? Hio ni Siri yangu..
Samahani kwa ntakayoyasema hapa hii inanihusu na nasema ukweli

Nakumbuka kuna kipindi nilikua napenda sana masuala ya upadre hususani ubraza na yale maisha ya utawa vile mapadri wanavyoishi yaan nilikua napenda sana ilinivutia kuona wale mabraza jinsi wanavyovaa na kupendeza zile nguo zao za kimisionari

Basi nikaenda kuomba kuanza kujifunza kusimamia kanisani pale mbele, enzi hizo nakumbuka nilikua mdogo sana nilikua km na miaka 7/8 hivi nilimwambia mzee mimi napenda sana kuhudumia kanisani mzee akakubari ila kipindi hicho mzee alikua busy sana kukaa nae mezani ilikua imezidi sana dakika 5 yeye ni mtu wa kazi na kazi na yeye muda wa kukaa na sisi labda wiki end

Basi nikapeleka barua kwenye jumuiya kutoka kanisani ikaenda ikasainiwa na mwenyekiti safi nikarudisha kanisani nikaanza mafundisho ya kutumikia, I am telling you niliweza kuhudhulia wiki moja tu narudia tena nilihudhulia mafunzo ya kutumikia wiki moja tu baada ya hapo nilikaa pembeni mwenyewe yaani niliacha mwenyewe bila kulazimishwa na mtu

Mzee aliponiona sihudhurii tena yale mafundisho akaanza kunihoji vipi mboni hauendi tena kujifunza kutumikia kanisani, umeacha? Nikamwambia mzee nimegairisha sitaki tena kusikia habari za kutumikia kanisani, kuanzia hapo nikaanza kuchukia zile habari za kutumikia na wale mabraza pamoja na wale wanaotumikia kanisani nikawa siwakubari tena km jinsi nilivyokua nawakubari pale mwanzo kabla sijajiunga na mafundisho ya kutumikia kanisani

Niliona nini? Hio ni Siri yangu..
Mpaka hapa chochote utakachokiandika ukiwa umebanwa na watu utakuwa umejitungia ilibidi useme straight uliona nini na nini toka mwanzo na hapa sote hatujulikani tunatumia fake IDs ni nani angekujua?
 
Back
Top Bottom