Hatari ya Kufanyika kwa Kosa kubwa la kihistoria: Viongozi CHADEMA kutaneni kwa dharura!

Nakubaliana na wewe kwa asilimia miamoja, kwani watu wengine wamejaa hofu ambayo haina msingi. Hayo ni maamuzi ya Kamati Kuu, ni maamuzi ya watu wengi na ambao wameaminiwa na wanachama wa CDM kwahiyo sidhani kama kunatatizo lolote.

Ndugu yangu hawa watu nashindwa kuwaelewa watoa wapi uoga huu?

Ni kweli zito ni nguzo muhimu sana ndani cdm ila pia anahitaji kuheshimu maamuzi ya chama.

kama mwalimu nyerere alitufikisha hapa tulipo "what did we give him in return"Ni heshima iliyotukuka japo hakuiomba leo iwaje zitto apigiwe magoti kisa kaisimamisha cdm?

Michezo ya ccm michafu sana ndiyo maana nchi yetu hasongi mbele sababu ya kutumia fedha za nchi kukandamiza fikra za watu na kuwatumia baadhi ya viongozi wa upinzani kuharibu vyama vyao i real hate this system
 
Mkuu naomba kutofautiana na wewe ... kwa hapa ilipofikia mimi naona hakuna kurudi nyuma,msimamo wa chuma ndio dawa ... hakuna kurudi nyuma ... chadema isiyumbishwe na ma ccm waliotapakaa mikoani wakizusha hili na lile ... Ki ukweli kwa sasa ndio namna pekee ya ccm kuendeleza ghilba zao kuwatumia mamluki wao ndani ya chama ... chadema isichoke kujibu mapigo... wasaliti wote wachukuliwe adhabu stahiki kwa mujibu wa maamuzi ya cc... chama kitabaki imara.
 
Naona ZITTO anaanza kutafuta huruma kupitia ID zake,msaliti huwa hasamehewi.
Mkuu tujilazimishe kwa lazma kufikiri nye ya jina la Zitto kama mtu mmoja na kujisukuma hadi kwenye kufikiri juu ya ukweli, uhalisia na mazingira halisi ya kile kilichotokea, kinachotekea na kitakachotokea.Kuhusu kujadili ID, Sidhani kama inaweza kutusaidia sana kwa sasa.
 
Mkuu tatizo la msingi ndani ya CHADEMA kwa sasa ,ni tatizo la kutengenezwa na sio tatizo halisia.Kuridhiana ndio kujenga, ndio kuunganisha, ndio kupatana na kinyume chake ndio kugawanyika, kugombana kuzozana n.k mkuu kibanga usinisukume nikaongea kitu ambacho sitaki kukiongea. naomba kama unaniamini niamini.Maridhiano kwa sasa ni jambo muhimu kuliko kitu kingine chochote. Zaidi ya hapo kama tunaamua liwalo naliwe, basi dunia yetu, chaguo letu.
Mkuu betlehem kama ndio hivyo unaonaje ikawa hata kwa Walid kaborour nae arudishwe bila kusahau wale madiwani wa Arusha waliofukuzwa? mkuu acha katiba ifuatwe siku 14 zikikatika fukuza kabisa
 
Last edited by a moderator:
Mkuu betlehem kama ndio hivyo unaonaje ikawa hata kwa Walid kaborour nae arudishwe bila kusahau wale madiwani wa Arusha waliofukuzwa? mkuu acha katiba ifuatwe siku 14 zikikatika fukuza kabisa

Zitto ndio anaibeba CHADEMA, wenye akili timamu pale CHADEMA wanamtazama Zitto, akifukuzwa na CHADEMA ndio itakuwa imefikia ukomo wake.
 
Mkuu, mbona huonyeshi huo umuhimu wa kukutana kwa dharura? Umepiga lamri ama umeota vibaya nini? Thread imekaa kinajimu najimu hivi... kama walimu aka majini yamepanda kamanda.
Ok mnafiki MM ni wakutoa chamani.
Mkuu.unajua ni kwa nini viongozi wa vyama hawapaswi kusema baadhi ya mambo kwenye mitandao bali kwenye vikao vya ndani tena ambavyo waandishi wa habari hawatakiwi kuwepo? Natumia hekma hiyo ijapokuwmimi sikiongozi.Naomba katika uzi huu univumilie rafiki yangu.
 
tushawishi kuhusu yafuatayo
1.Kwanini unataka tuvunje taratibu za kuwajibishana?
2.kwamba wewe ni mwanachadema na ugamba ulijitia kùuvua juzijuzi umeisha
3.na kwamba huna maslahi chadema?
MUHIMU:1.Màamuzi ya kamati kuu hayakuwa ya kukurupuka na hivyo lazima yazingatiwe kwa gharama yoyote ile
2.Bado kuna masalia na mapandikizi yanayohaha kumwokoa incharge wao
 
kuna watu wakishalipwa na mbowe wanaona kama chadema ni yao vile!!asante kuu kwa ushauri atakayefuata sawa asiyeufuata itakula kwake
 
Babu hawezi zungumza na waasi.. ! Watu wataky kukunyang'anya kamuhogo kako uzungunze nao!!!!
 
Mnapewa Ushauri wa maana badala ya kuufanyia kazi, mnaishia kutukana watu msiowajua, Wafuasi wa Padri babu sijui mkoje!

Mwambie simiyu akutumie tamko la chadema mkoa wa simiyu ili ulisambaze kwenye vyombo vya habari naona liko tayari analo mkononi na hyo ndiyo kazi unayoweza ifanya kwa ufasaha zaidi ya hapo wewe ni mzandiki tu
 
Mkuu betlehem kama ndio hivyo unaonaje ikawa hata kwa Walid kaborour nae arudishwe bila kusahau wale madiwani wa Arusha waliofukuzwa? mkuu acha katiba ifuatwe siku 14 zikikatika fukuza kabisa
Ndugu, nataka nikuhakikishie kwamba kinachonisumbua si woga.Pili napenda unielewe kwamba ninachozungumzia hapa sio samehe samehe tu, au kumhurumia mtu.Tatu unapozungumzia watu waliofukuzwa mwanzo, mazingira, hoja vielelezo n.k vinatofautiana. Sasa labda tu kama pengine unadhani nami pengine nimetumwa hapo sawa. lakini zaidi ya hapo, naomba unielewe kwamba nina nia safi.
 
Mkuu tatizo la msingi ndani ya CHADEMA kwa sasa ,ni tatizo la kutengenezwa na sio tatizo halisia.Kuridhiana ndio kujenga, ndio kuunganisha, ndio kupatana na kinyume chake ndio kugawanyika, kugombana kuzozana n.k mkuu kibanga usinisukume nikaongea kitu ambacho sitaki kukiongea. naomba kama unaniamini niamini.Maridhiano kwa sasa ni jambo muhimu kuliko kitu kingine chochote. Zaidi ya hapo kama tunaamua liwalo naliwe, basi dunia yetu, chaguo letu.

Mkubwa unaweza ukawa na jambo la maana sana ila kuwa mpole kwani kila wazo la kila mtu hapa jamvini linafanyiwa kazi barabara na hata hivyo haya yaliyotokea ndani ya chama ni kwamba yamebidi tu.

Wazo lako liko jikoni shaka ondoa!

Tunapenda Taifa linalojengwa na watu wenye uchu wa Nchi yetu.
 
Jamani ! chonde chonde! chonde! Viongozi wa CHADEMA,

  • Naomba kwa heshima kubwa Viongozi wa CHADEMA (waandamizi) wakutane kwa haraka kadiri iwezekanavyo, Waridhiane na kuita vyombo vya habari na kuwaeleza maeneno machache tu "Tumeyamaliza, yaliyopita yamepita, tuko pamoja na tunasonga mbele" au maneno yenye maudhui kama hayo.Ni muhimu kuwaona Mbowe, Dr.Slaa na Zitto wakiwa kwenye press conference kwa pamoja huku wakishikana mikono. Nivyema kufanya hivyo bila kupoteza hata dakika. tafadhali sana!
  • Wafute shutuma zote zinazomkabili Zitto bila masharti. Kuhusu wengine wanaokabiliwa na shutuma watumie busara tu kufikiri ni nini wanaweza kufanya.
  • Chonde chonde tafadhali; fanyeni hivyio ikiwezekana leo.Msisubiri zile siku kumi na nne zifike.Fanyeni hivyo kabla tuhuma hizo 11 hazijavuja kwa wananchi na kujadiliwa. Mkichukulia masikhara, Muda si mrefu linaweza kutokea kosa kubwa sana la kihistoria litakalobadilisha kabisa historia ya chama chetu na kukifanya kionekane kwa sura tofauti kabisa.Chonde chonde viongozi wa chama fanyeni hivyo kukinusuru chama tafadhali.
  • Mtu anaweza kusema hatuwezi kuwachagulia viongozi chakufanya: Tafadhali sana: naomba tusilaumiane, kuzozana au kuendelea kunyosheana vidole katika wakati huu.Tufanye hili kwanza halafu ndo tuendelee na mengine.Ni hatua ya dharura!
Tumieni busara kufikiri hili ninalolisema. Ninyi ndio mmeandika tuhuma 11, zinazowakabili Zitto na wenzake na mnazijua vizuri na mnafahamu mengi. Kadhalika nina uhakika mnapata idea ya ninachokisema.

Nawahakikishieni:
Nina akili timamu wakati huu naandika hapa, nina nia njema na nimefanya utafiti wa kutosha kabla ya kuongea ninachoongea. Ukali wa kichwa cha habari hapo juu ni halisia na sio kuigiza. Tafakarini kwa haraka na kuchukua hatua tafadhali sana sana!

Mkuu kwa nini debate ? Kama kweli una nia njema kama hii kwa nini uje JF ? Maamuzi hayakutolewa na JF busara yako funga safari hadi Chadema Kinondoni milango iko wazi tafuta viongozi kaa nao useme yako kwa ushahidi wataona hiyo haraka na kuamua baada ya kuyapima maneno yako kwa ushahidi na mtafute Zitto pia kaa naye onyesha ushahidi then waache waamue .Why JF ? Au unataka utafutwe pembeni na wabaya au hata wazuri mkafanye deal maana tukio hili angalau sasa kuna watu wanaamka wanasema wanaenda kazini au wamesha safiri wanasema wako kazini .Epuka hayo nenda Chadema ofisini na ushahidi wako .
 
betlehem: Mkuu kwa nini hutaki kutulia....suala kama hili ulishaelezwa kwenye uzi wako wa Usuluhishi kwa majedwali. Ukaambiwa usubiri wahusika wajibu tuhuma zao, leo unaibuka na hili.

Ebu rejea bandiko hili hapa tena (post namba 54) >>>>>https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...majedwali-ya-mapendekezo-ya-usuluhishi-3.html
Mkuu kila mara ninapata vitu vipya ambapo ninadhani kukaa navyo na wakati najua vinaweza kuleta madhara itakuwa ni usaliti (kwa mujibu wa mtazamo wangu lakini).Naomba kama nitakuwa nimekukwaza; basi unisamehe.
 
Watakaounga mkono hii hoja yako ni CCM, Zitto, Mkumbo pamoja na wengine wenye mtazamo kama wa hao. Huoni hata ZeMarcopolo amelike hoja yako........Zitto lazima apigwe chini once and for all....Hizi hekima, hekima za kupatana na wasaliti hazikubaliki !

Back
Top Bottom