Hatari ya Kufanyika kwa Kosa kubwa la kihistoria: Viongozi CHADEMA kutaneni kwa dharura!

ovyo kabisa nenda lumumba ukapokee uijra wako wa buku saba, kamwe haturudi nyuma lazima masalia wote waishe na ndipo tutabaki salama VIVA CHADEMA. KAMA MNA MMPENDA MKARIBISHENI MPEENI UWAZIRI MKUU WA SERIKALI YA CCM, SHAME UPON THEM
mkuu, upo kaka!
 
Jamani ! chonde chonde! chonde! Viongozi wa CHADEMA,


  • Naomba kwa heshima kubwa Viongozi wa CHADEMA (waandamizi) wakutane kwa haraka kadiri iwezekanavyo, Waridhiane na kuita vyombo vya habari na kuwaeleza maeneno machache tu "Tumeyamaliza, yaliyopita yamepita, tuko pamoja na tunasonga mbele" au maneno yenye maudhui kama hayo.Ni muhimu kuwaona Mbowe, Dr.Slaa na Zitto wakiwa kwenye press conference kwa pamoja huku wakishikana mikono. Nivyema kufanya hivyo bila kupoteza hata dakika. tafadhali sana!
  • Wafute shutuma zote zinazomkabili Zitto bila masharti. Kuhusu wengine wanaokabiliwa na shutuma watumie busara tu kufikiri ni nini wanaweza kufanya.
  • Chonde chonde tafadhali; fanyeni hivyio ikiwezekana leo.Msisubiri zile siku kumi na nne zifike.Fanyeni hivyo kabla tuhuma hizo 11 hazijavuja kwa wananchi na kujadiliwa. Mkichukulia masikhara, Muda si mrefu linaweza kutokea kosa kubwa sana la kihistoria litakalobadilisha kabisa historia ya chama chetu na kukifanya kionekane kwa sura tofauti kabisa.Chonde chonde viongozi wa chama fanyeni hivyo kukinusuru chama tafadhali.
  • Mtu anaweza kusema hatuwezi kuwachagulia viongozi chakufanya: Tafadhali sana: naomba tusilaumiane, kuzozana au kuendelea kunyosheana vidole katika wakati huu.Tufanye hili kwanza halafu ndo tuendelee na mengine.Ni hatua ya dharura!
Tumieni busara kufikiri hili ninalolisema. Ninyi ndio mmeandika tuhuma 11, zinazowakabili Zitto na wenzake na mnazijua vizuri na mnafahamu mengi. Kadhalika nina uhakika mnapata idea ya ninachokisema.

Nawahakikishieni:
Nina akili timamu wakati huu naandika hapa, nina nia njema na nimefanya utafiti wa kutosha kabla ya kuongea ninachoongea. Ukali wa kichwa cha habari hapo juu ni halisia na sio kuigiza. Tafakarini kwa haraka na kuchukua hatua tafadhali sana sana!

Kwahiyo wewe unataka hayo mnayoyaita mabomu mbaki nayo au mmeanza kuhisi mpo kwenye nyumba ya vioo pia
 
Mkuu tatizo la msingi ndani ya CHADEMA kwa sasa ,ni tatizo la kutengenezwa na sio tatizo halisia.Kuridhiana ndio kujenga, ndio kuunganisha, ndio kupatana na kinyume chake ndio kugawanyika, kugombana kuzozana n.k mkuu kibanga usinisukume nikaongea kitu ambacho sitaki kukiongea. naomba kama unaniamini niamini.Maridhiano kwa sasa ni jambo muhimu kuliko kitu kingine chochote. Zaidi ya hapo kama tunaamua liwalo naliwe, basi dunia yetu, chaguo letu.
vipi mkuu ulishiriki kulitengeneza?
 
Back
Top Bottom