Kasi kubwa ya Rais Samia katika maendeleo yawavuruga na kuwasamabratisha viongozi wa CHADEMA

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,186
9,631
Ndugu zangu watanzania,

Rais Samia Ambaye ndiye kiongozi mwenye ushawishi zaidi Barani Afrika na ambaye anatazamwa Kama mtetezi wa Bara la Afrika na ambaye wengi wanamwita Sauti ya Afrika na waafrika, Komandoo wa Diplomasia na Jasusi wa kiuchumi, Ameendelea kutetemesha na kuteka siasa za Tanzania, Bara la Afrika na kuteka Dunia nzima kwa aina ya uongozi wake ulioteka hisia za watu wengi Sana.

CHADEMA kabla ya kuruhusiwa kwa mikutano ya hadhara walipiga Sana kelele za vitisho na mbwembwe nyingi Sana za kusema kuwa wanakwenda kuzungumza na watanzania mambo makubwa Sana ambayo yanakwenda kubadili upepo wa kisiasa wa Taifa letu, wakawa na mbwembwe za Hadi maandalizi ya kuwapokea viongozi wao kwa magharama makubwa Sana ambayo yangeweza kutosha hata kupaka rangi ofisi zao zilizochakaa Kama nyumba ambayo haikaliwi na mtu.

Walichokuwa hawakijuwi Ni kuwa mikutano ya siasa inaporuhusiwa Tayari serikali ya CCM chini ya Rais Samia ilikuwa imefanya kazi zote kubwa zilizokuwa zinagusa maisha ya watanzania,Rais Samia alikuwa Tayari ameteka hisia za watanzania na kuitawala mioyo ya watanzania,Tayari Rais Samia alikuwa amewakosha na kukonga nyoyo za watanzania kutokana na utendaji kazi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania,
Tayari Rais Samia alikuwa amefanya uwekezaji wa mabillioni ya pesa katika kila secta inayogusa maisha ya watanzania,Tayari Rais alikuwa amesikiliza sauti za watanzania,Tayari alikuwa amefanya maridhiano yaliyoleta umoja mshikamano upendo na umoja wa kitaifa.

Tayari Rais Samia alikuwa ameyateka makundi yote na Rika zote kutokana na kujibu kero za kila kundi,Tayari Rais Samia alikuwa Ameziteka ngome za upinzani na kuziweka upande wake,Tayari alikuwa anasonga mbele kwa Kasi ya rocket,Tayari alikuwa Amejenga uchumi unaomgusa kila mtu ,Tayari Rais Samia alikuwa anasonga mbele na watanzania wote bila kumuacha yeyote nyuma, Tayari kila mmoja alikuwa anajiona Anayo nafasi katika ujenzi wa Taifa letu.

CHADEMA wamejikuta hawana Sera za kuwaeleza watanzania,hawana kipya Cha kuweza kuwashawishi watanzania,wanatumia nguvu nyingi za maandalizi ya mikutano Yao pasipo kupata matunda, wamejikuta wanapuuzwa na watanzania,vijana waliokuwa ngome Yao wamewapa kisogo na hawana habari nao,kwa Sasa watu wanaelekeza sifa na pongezi kwa Rais Samia na serikali yake ya ccm kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa uzalendo na moyo wa kujitolea kuwatumikia watanzania, kwa Sasa CHADEMA hawaeleweki Wala kusikilizwa na watanzania.

Mikutano Yao ikawa kazi Kuendelea nayo ndio maana hata habari zao kwa Sasa hazisikiki Wala kueleweka Kama wapo au hawapo,wamejikuta wanashutumiana wao kwa wao juu ya kwanini huyu anampongeza Sana Mwenyekiti wa CCM na kwanini huyu kabadilika.

Sasa Chadema wamekata Moto,wameishiwa pumzi,wameishiwa hoja, hawana ushawishi, hawana dira Wala muelekeo,hawana Sera Wala ajenda, safu yao ya uongozi imejikatia Tamaa na kupoteza ushawishi mbele ya wafuasi wao wachache waliobakia.

Wakati hayo yakitokea huko kwa chadema Hali Ni tofauti kwa upande wa chama Tawala ,chama ambacho histori yake ndio historia ya Taifa letu, Chama ambacho Baba waTaifa alikuwa mwanachama wake na aliyekipenda mpaka anafariki Dunia, chama ambacho kimebeba matumaini ya watanzania,chama ambacho kina uchungu na Taifa letu na ambacho kimeonyesha uwezo ushupavu na umadhubuti wa kiuongozi, chama ambacho kinapigiwa mfano Barani Afrika

Hii ni CCM ambayo kwa Sasa imeendelea kuchanja mbuga katika mioyo ya watanzania na kuungwa mkono na mamillion ya watanzania kutokana na uchapa kazi wake na kuwatumikia watanzania kwa uzalendo mkubwa. Chama ambacho kwa muda wote kimekuwa na dira na muelekeo unaoeleweka pamoja na Sera na ajenda zinazogusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti kinaendelea kuwa mioyoni mwa watanzania.

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana Mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
 
SIku hizi umeanza kukumbuka kuweka namba za simu baada ya sisi kukumbusha.
Hiyo kasi unayoiongelea ni hii ya kutumia shilingi bilioni 7 kukarabati Kuvuko cha shilingi bilioni 8.5?
 
Ukatae ukubali chadema ndio baba lao CCM haina uhai bila Chadema. Ahsante sana luca kazana tunakuona muda si mrefu na wewe tutakupa nafasi.
 
Sijui kwa nini kila uzi ukiandika kuhusu kumsifia Rais Dk Samia unaonekana Chawa hata ukiandika ukweli mkuu Lucas mwashambwa
Ukweli Ni ukweli tu hata watu wangapi wapinge lakini uweli utasimama tu,Hata Galileo alipingwa Sana na watu wengi na mwisho ikaja kufahamika kuwa alikuwa sahihi,Nami nasema kuwa kwa Sasa Chadema Imepoteza ushawishi kwa watanzania na Wala haina Sera Wala ajenda zenye kugusa maisha ya Bibi wa kule kijijini kuweza kuwaunga mkono,Huo ndio ukweli,chadema Ni genge la wasaka tonge
 
Hapana Mimi naeleza ukweli japo Ni mchungu,Embu nikuulize Hivi unaelewa Sera na ajenda za chadema zinazogusa maisha ya Bibi yako kule kijijini Ni zipi? Umewahi kuzisikia?
Kwakua bibi yako anaishi kijijini unadhani wote bibi zao wapo Kijijini. Very idiot ndio maana unashabikia ccm
 
Ukatae ukubali chadema ndio baba lao CCM haina uhai bila Chadema. Ahsante sana luca kazana tunakuona muda si mrefu na wewe tutakupa nafasi.
Chadema kwa Sasa haina ubavu Wala uwezo wa kuweza kushindana na CCM kisera na hata kiajenda,kwa Sasa CCM Ina ushawishi kwa makundi yote wakati chadema wamepoteza muelekeo na ushawishi kwa makundi yote hawakubaliki, kwa Sasa vijana wanajionaa fahari kujiunga CCM wakati mtu akisema yupo chadema inaonekana Kama mbabaishaji tu na aliyekosa muelekeo
 
Wanakulipa sh ngap dogo? Au umeahidiwa kaubalozi kamtaa!!?
Silipwi chochote kuandika ukweli hapa jukwaani Bali Ni uzalendo wangu kwa chama changu Cha ccm, serikali ya CCM na Taifa langu la Tanzania, usijiulize Tanzania itakufanyia Nini Bali jiulize utaifanyia Nini Tanzania
 
Kwenye billion 10
Billion 8 ufisadi
Billion 2 zinafanyiwa maendeleo.
Hakuna atakaye bakia salama Wala kusalimika katika serikali ya Rais Samia akibainika kugusa pesa za umma kwa maslahi yake binafai,Hakika atakiona Cha Moto ,atajuta sana maana watanzania tunafahamu namna mh Rais wetu mpendwa mama Samia asivyo na Subira kwa wabadhirifu wa fedha za umma
 
2020 hamkujiamini, mkaona bora muibe uchaguzi wote...

Watu hawataki ngonjera eti
 
Hakuna atakaye bakia salama Wala kusalimika katika serikali ya Rais Samia akibainika kugusa pesa za umma kwa maslahi yake binafai,Hakika atakiona Cha Moto ,atajuta sana maana watanzania tunafahamu namna mh Rais wetu mpendwa mama Samia asivyo na Subira kwa wabadhirifu wa fedha za umma
Hivi kuna kiongozi alie kuwa ajaiba hela ya umma?.
 
2020 hamkujiamini, mkaona bora muibe uchaguzi wote...

Watu hawataki ngonjera eti
Sera Bora na ajenda zinazogusa maisha ya watanzania pamoja na ilani Bora inayokuwa imebeba mambo yote yanayokata kiu ya watanzania Ndio imekuwa ikiipatia CCM ushindi wa kishondo. Sasa Cham Kama chadema hata tu kuandaa ilani take Hakiwezi, Sasa je Ni mtanzania yupi mwenye Akili Timamu anayeweza kuwaunga mkono CHADEMA?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom