Hata wanaume hulia

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
138,638
2,000
Tough-Men-Cry.png


Chozi ama machozi ni ishara ya kuumia na maumivu yaliyoshindwa kuhimili hisia za kawaida za kibinadamu... Wanawake ni mabingwa kwenye hili. Wanaume huchukuliwa Kama shupavu wasiotoa machozi yao hovyo, kuonyesha machozi mbele ya kadamnasi kwa Mwanaume ni ishara ya Udhaifu na kushindwa kuhimili hisia hasi but men do cry.

Si machozi yale ya mapenzi ama kwenye misiba yale ni ya kawaida sana kufuatana na hisia za kawaida za kibinadamu. Kuna wanaume hulia mioyoni mwao Kimyakimya. They are so brave on their faces lakini rohoni wanabubujikwa machozi. Wana mengi sana wana magumu yanayowakabili. They may save you with bright smiles but internally they are crying.

Angalia ndani ya ofisi kwenye usafiri wa jumuiya na hata sehemu za starehe. they are secluded always very calm n quite don take them for granted. Wana maumivu makali rohoni sometimes unbearable.... Wanaume hulia Kimyakimya

R. I. P. Mwl. Frank...! A very dear friend... The moment knows the truth....

 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
15,912
2,000
Nakumbuka nikiwa chuoni nilikua Campaign Officer wa Mgombea, mgombea akaitwa na ambaye anatakiwa kuachia kiti akaambiwa "Wewe na mpinzani wako wote ni ccm, hivyo hamtakiwi kugombana kwakua mshindi ataenda kutuwakilisha tahliso ambayo nayo ina baraka za ccm. So stop huu userious"
Mgombea akaja kutupa hiyo taarifa campaign officers wake, mimi sina chama lakini sikuwahi kuikubali ccm, pale pale uchungu ukanishika kwamba inakuaje nimeicheza ngoma ya ccm bila kujua?
Mara ghafla machozi hayooo, wenzangu wananiuliza "Ebwana vipi mbona machozi?" Nikatunga uongo wa mafua nikarudi nyumbani na kampeni kwangu zikaishia hapo.

Hayo machozi yalikua ni baada ya miaka 6 kwakua mara ya mwisho kulia ilikua form one
 

Planett

JF-Expert Member
Mar 20, 2014
7,554
2,000
hivi kuna mwanamke anayeweza kumzidi yule mama wa bongo muvi katika sekta ya KULIA !!? kuna watu wanavipaji aisee
 

APEFACE

JF-Expert Member
Oct 1, 2016
3,387
2,000
Mwanaume akilia ujue ni jambo zito linalomsibu sio bure................mwanaume hutakiwi kulia, unatakiwa kububujikwa na machozi endapo yamekufika mazito,
 
Top Bottom