Hata wanaume hulia

Hata wanaume hulia

 
Sometimes I wish life had a delete button — for certain people, memories, and feelings.
 

Wanaume hulia mara 6 hadi 17 kwa mwaka​

Lini ilikuwa mara yako ya mwisho kulia? Tafiti za kisayansi zimeonyesha kuna utofauti wa kiwango cha kulia kati ya wanawake na wanaume.

Kufuatia utafiti uliofanywa na Ad Vingerhoets, mwanasaikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Tilburg nchini Uholanzi alibaini kuwa wanawake hulia mara nyingi zaidi kuliko wanaume.

Hata hivyo kulingana na matokeo ya tafiti mbalimbali yaliyokusanywa na wataalamu wa German Society of Ophthalmology yalithibitisha tofauti hiyo. Kwa mujibu wa utafiti wao ulionesha , wanawake hulia wastani wa mara 30 hadi 64 kwa mwaka, wakati wanaume hulia wastani wa mara 6 hadi 17 kwa mwaka.

Utafiti huo pia ulibaini kuwa muda wa kulia hutofautiana. Wanaume mara nyingi hulia kwa muda mfupi wa takribani dakika mbili hadi nne, ilhali wanawake wanaweza kulia kwa wastani wa dakika sita au zaidi kwa tukio moja.

Watafiti wameeleza sababu za utofauti huo ikiwemo kibaolojia, ambapo homoni kama prolactin inayopatikana kwa kiwango kikubwa zaidi kwa wanawake inaaminika kuhusika katika kuamsha machozi. Pili ni sababu za kijamii, kwani katika jamii nyingi wanawake huruhusiwa kuonyesha hisia zao zaidi kuliko wanaume.

Utafiti huo pia umeonyesha kwamba tofauti hizi hazionekani kipindi cha utoto.Na kabla ya kubalehe, wavulana na wasichana hulia karibu kwa kiwango kinachofanana. Tofauti huanza kuonekana kadiri wanavyokua na kuanza kuathiriwa na mabadiliko ya homoni pamoja na mazingira ya kijamii.

Kwa ujumla, tafiti hizi zinaonyesha kuwa kulia ni jambo la kawaida la kuonyesha hisia. Ingawa wanawake huonekana kulia mara nyingi zaidi, watafiti wanasisitiza kuwa kulia si ishara ya udhaifu bali ni njia ya asili ya mwili na akili kuonyesha hisia kama huzuni, furaha au msongo wa mawazo.

Kwa sababu hiyo, wataalamu wa saikolojia wanashauri jamii kuacha kuona kulia kama udhaifu hasa kwa wanaume, bali kutambua kwamba kuonyesha hisia ni sehemu ya afya ya kihisia kwa kila binadamu.
fr1b55c5c3a4cdb14367a3dce9307ab346c53255e5.jpeg
 
Back
Top Bottom