Hata mwaka 1992, tungeongozwa na hofu, vyama vingi visingekuwepo

DATAZ

JF-Expert Member
May 25, 2012
2,453
5,987
Hofu ni Hali tu na Wala sio hoja. Watanzania tumeendelea kuwa mahodari wa hofu wasio na hoja.

Nakumbuka mwaka 1992 wakati wa mjadala wa Nchi kuwa na mfumo wa vyama vingi, wengi sana walipinga kwa kujazwa hofu. Wachache walioelewa wakiongozwa na Baba wa Taifa, wakaunga mkono KWA HOJA, kuwa Nchi yetu iikubali Mfumo wa Vyama vingi.

Hofu Ilikuwepo pia tulipotoa mashirika yetu kama ya mawasiliano kwa wawekezaji, Embu niambie tungeendelea na TTCL tungekuwa wapi. Lazima tukubali Kuna mambo wenzetu wanaweza zaidi, hakuna dhambi kushirikiana nao.

Watanzania tuna mazoea ya kutojishughulisha kujua (ku -STUDY) mambo, pengine hatuna uwezo wa ku foresee mambo ya mbeleni. Pengine ndio maana haishangazi kuwa hata masoko yetu, yamejaa ubunifu wa watu wa nchi nyingine na sisi timebaki wa kuiga tu. Tunachojua kubuni ni majungu, uzushi na umbeya.

Tuipe serikali yetu nafasi ya kufanya mambo na tuikosoe kwa hoja zenye facts na figures
 
Back
Top Bottom