Hata kama ni kuswali, ila huu si Ustaarabu jamani

Hata kama ni kuswali, ila huu si Ustaarabu jamani

Status
Not open for further replies.
kama unaona njia imefungwa badilisha pita kwingine. simple!
 
242cc4e08ffb7bb18aacd87a4240cb1a.jpg
d835916bdd7b27df5e343252badd8c70.jpg
104e5ceb7d9b4cfb2ba593fc56d4527d.jpg


Naomba nianze kwa kudeclare interest kuwa hii sio Mada ya kukashfu dini.

Mi napenda kufikisha malalamiko kwa wahusika pitia JF.

Mwanza mtaa wa Lumumba imezuka hii tabia ya kufunga barabara muda wa ibada katika msikiti wa Lumumba. Binafsi sielewi sababu ya kuamua kufunga barabara ila ningependa kuzungumzia kero tunayopata baada ya barabara kufungwa.

Huu mtaa wa lumumba upo katikati ya mji wa mwanza na unabiashara mbalimbali zinazoendelea. Pale wenzetu wanapoamua kufunga barabara muda wao wa ibada kusema ukweli imekuwa kero kwa baadhi yetu maana hata biashara zetu husimama pia na hata kusababisha Traffic jam.

Mi ngependa kutoa ushauri kwa wahusika watafte njia mbadala ya kuhakikisha hii tabia ya kufunga barabara inakoma. Hivi kila msikiti na kanisa hapa mjini ukifunga barabara je itakuaje?
Kwsni huwa wanafunga kutwa nzima au masaa mangapi,navojua waisilam wakitumia muda mwingi kuswali ni dkk 30 tu haizidi hapo.
 
Kwa kweli watu naona wemishindwa kuvumiliana, hao watu wanaoswali nje ya misikiti si kuwa wanapenda bali ni idadi ya wanaoswali ni kubwa kuliko uwezo wa msikiti, na hufanya hivyo si kila siku bali ni siku maalum hasa siku za Ijumaa na za idi, ikiwa watanzania tumefika hapa hii ni hatari kubwa sana. Naomba tuvumiliane hapa duniani tunapita tu hujui nani atakufaa na kuna mambo mengi mazuri ya kuweza kujadiliana na kushirikiana tusigawanywe kwa imani zetu.
 
Mbona wengine watupigia makelele kwenye mabasi htaongei. Huenda hatupendi lakini tunavymiliana
 
Kwa kweli watu naona wemishindwa kuvumiliana, hao watu wanaoswali nje ya misikiti si kuwa wanapenda bali ni idadi ya wanaoswali ni kubwa kuliko uwezo wa msikiti, na hufanya hivyo si kila siku bali ni siku maalum hasa siku za Ijumaa na za idi, ikiwa watanzania tumefika hapa hii ni hatari kubwa sana. Naomba tuvumiliane hapa duniani tunapita tu hujui nani atakufaa na kuna mambo mengi mazuri ya kuweza kujadiliana na kushirikiana tusigawanywe kwa imani zetu.
Kwahiyo kila mtu akitindikiwa na tatizo basi anaweza kufanya lolote tu?

Hakuna viwanja au kumbi kubwa mkafanyie hizo ibada huko?

Au kwanini msiweke utaratibu wa kupokezana muda wa kuabudu?
 
Kuna uhuru wa kuabudu ni kweli kabisa. Lakini kuna uhuru pia wa kutumia barabara na lengo la kujenga barabara si kwa matumizi ya ibada ni kwaajili ya kutoa huduma ya usafiri.
Mtu anaona nusu saa ni muda mfupi sana ni mrefu sana kama una mambo ya muhimu ya kufanya na watu wakakublock.
Kama nyumba ya ibada ndogo waombe eneo jingine wapewe wasali huko.
Ipo siku watu wataanza kukusanyika barabarani wakitumia reference mbona wale wanaachwa wafunge barabara.
Tusizibebe dini zetu zikatulevya tukaanza kuwa kero kwa wengine.
Hapa kwangu kuna nyumba ya pili ni ya makazi lakini naona limefunguliwa kanisa la watu wa 3 na wameweka spika nnje huwezi kulala, kusoma na ukiumwa ni kero zaidi.
Serikali iangalie uhuru unaoingilia uhuru wa wengine si sawa.
Uhuru wako unaishia unapoanzia uhuru wako
 
Kupanua msikiti unadhani haiwezekani kwa sababu ya eneo dogo. Kuna mskanisa mijini yana eneo dogo ila wametumia akili wakayapanua kwa kujenga gorofa.

Mijini kuna kumbi kibao za mikutano. Wawe wanakodi pia.

Wakristu mbna wanasali kwa zamu. Waislamu wanashindwa nini ijumaa juwa na ratiba kusawali kwa zamu bila siku kupita?
Kuswali kwa zamu,ili nikueleweshe nijibu hili kwanza. Waislam wapiga adhana sasa wakristo wanashindwa nn na wao kuitana kwa adhana badala ya kupiga kengele?
 
Kwani huwa wanaifunga kila siku hiyo barabara ama ni kwa ajili ya Siku ya Ijumaa tu pale waumini wanapokuwa wengi kuliko uwezo wa Msikiti? Pamoja na hilo Ijumaa yenyewe ni Wastani wa Nusu SAA hadi SAA 1 kweli ndo iwe Nongwa kiasi hicho Jamani? Hapana, tupunguze kuzoza Waungwana!!!
Haijalishi hata kama ni dakika 2,mnakera sana,na kujiona nyinyi ndo bora zaidi na na dini yenu. Hivi,unajua mtu anapoenda unapomzuia?mnataka muifanye kuwa ndo dini ya taifa?
 
Kwani huwa wanaifunga kila siku hiyo barabara ama ni kwa ajili ya Siku ya Ijumaa tu pale waumini wanapokuwa wengi kuliko uwezo wa Msikiti? Pamoja na hilo Ijumaa yenyewe ni Wastani wa Nusu SAA hadi SAA 1 kweli ndo iwe Nongwa kiasi hicho Jamani? Hapana, tupunguze kuzoza Waungwana!!!
Kwa upeo wako unaona ni Sawa? Jengeni nyumba za ibada za kuwatosha barabara zetu zibaki wazi
 
Kwanini wafunge barabara aisee so wakasali ndani ya maikiti mbona sheria hairuhusu kwa nn wahusika hawakemei mpaka mtu aje jf ni aibu kwa watawala wa eneo husika kama eneo ni dogo watafute mahala pengine pa kuabudia hiyo ni barabara sio msikiti
 
Nimekaa UK na mitaa ya Brune tulikuwa tunaswali na waenyeji wanatuelewa ni muda mfupi tu. Na ni kutokana na ufinyu wa eneo. Siku zingine usipende kutoa ushahidi wa uongo, eti wazungu hawafungi barabara wakati huko nje kwenyewe hukafika
Weka picha, mzungu hawezi kkuta mambo ya ujima kama huu mnaofanya karne hii.
 
Kwahiyo kila mtu akitindikiwa na tatizo basi anaweza kufanya lolote tu?

Hakuna viwanja au kumbi kubwa mkafanyie hizo ibada huko?

Au kwanini msiweke utaratibu wa kupokezana muda wa kuabudu?
Kwa taarifa yako hilo tatizo haliko Tanzania pekee bali sehemu nyingi za dunia huwa hivyo na watu wengi wanalielewa kama mtu anaona akakwazika kwa hilo apeleke malalamiko yake sehemu husika ili ufumbuzi upatikane kama si hivyo hakuna haja ya kulalamika.
matatizo si kumbi kubwa za ibada au viwanja, tatizo Ijumaa ni siku ya kazi kwa huku kwetu na watu huwa makazini hivyo waislamu hupata ruhusa ya masaa machacha ili waswali na warudi makazini wanajikuta wanakwenda kwenye msikiti uliyokaribu nao ili waweze kuswali ili warudi kuwajibika.
Ijumaa huswaliwa mara moja kwa wakati maalum katika sehemu husika, kuna ibada (swala) nyingine tunaweza kupokezana ikiwa sehemu ni ndogo lakini kwa Ijumaa ni vigumu.
 
Unapoangalia chini badala ya mvele huachi kujikwaa ,anaelia akakamata mguu badala ya kichwa ni sawa na guu lake mwenyewe.
 
Hii mimi sioni kama ni kero,kinachonikera ni yale ma spika ya makanisani na yale yanayotumiwa na masheikh kutoa mawaidha, kuswali acha waswali tu hata road ifungwe masaa3
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom