Zero Hours
JF-Expert Member
- Apr 1, 2011
- 12,942
- 18,693
Naomba nianze kwa kudeclare interest kuwa hii sio Mada ya kukashfu dini.
Mi napenda kufikisha malalamiko kwa wahusika pitia JF.
Mwanza mtaa wa Lumumba imezuka hii tabia ya kufunga barabara muda wa ibada katika msikiti wa Lumumba. Binafsi sielewi sababu ya kuamua kufunga barabara ila ningependa kuzungumzia kero tunayopata baada ya barabara kufungwa.
Huu mtaa wa lumumba upo katikati ya mji wa mwanza na unabiashara mbalimbali zinazoendelea. Pale wenzetu wanapoamua kufunga barabara muda wao wa ibada kusema ukweli imekuwa kero kwa baadhi yetu maana hata biashara zetu husimama pia na hata kusababisha Traffic jam.
Mi ngependa kutoa ushauri kwa wahusika watafte njia mbadala ya kuhakikisha hii tabia ya kufunga barabara inakoma. Hivi kila msikiti na kanisa hapa mjini ukifunga barabara je itakuaje?
Na barabara kma iyo ina two ways. Kwanini msifunge one way na kuacha way nyingne ikitumika?