Hasira kwa mtoto, huku baba tunamuogopa....

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,229
116,840
Mbona kama ukweli uko wazi kabisa...kila anachofanya mtoto kina baraka za baba yake..
Na pengine baba ndo anamtuma mtoto afanye anayoyafanya

Sasa mbona hasira ni nyingi sana kwa mtoto huku baba hatutaki kabisa kumuudhi?

wengine wanasema tunampenda na kumuombea 'baba mtu' huku wakizidi kumponda mtoto

huu unafiki unatusaidia nini?

Kwanini kama tunaona hatumuwezi baba mtu basi na mtoto tusimguse?
au haki na ukweli inatazama cheo?
 
au haki na ukweli inatazama cheo? Leo nakuunga mkono mkuu ni kweli kabisa,
Utamthubutu baba huku ana upinde na mishale kibao...bora umuonee mtoto, baba akikoroma ujifiche mbali kabla hajatoa silaha zake...lkn ndvyo tulivyo.
 
Uswahilini tukimshindwa Jirani kumtukana live kwa ukorofi wake tunatumia kitoto kidogo kumalizia hasira.

Unakaambia katoto Ka Miaka 7 kaliko keti karibu na jirani jeuri eti 'nyoo utaishia kuchapiwa na kuletewa watoto wa kulea'

Ujumbe unakuwa umefika lakin Kama Jirani mwenyewe Chizi fyatu hatoelewa!

Ukorofi wa Kambarage ulitulazimisha kumtukana kupitia Simba wa Vita Mzee Kawawa!

Mkapa tulimtukana kupitia Mr Zero

Mwinyi na Jk tuliwatukana live kwa kuwa walikuwa wanachukulia poa
 
Is-business-rational-or-emotional.jpg

Huu ni mlinganyo wa mapenzi vs akili! Ila ule usemi wa mchelea mwana kulia,hulia yeye naanza kuuelewa sasa!
 
Hata baba tuna hasira nae sana... ni vile inawezekana hakuna namna ya kumtungua kwa sasa.

Kama tunamuogpa bora wote tuwaache tu
huyu mtoto ni 'mtiifu' tu kwa baba yake
tunamuonea tukijifanya eti 'tunampenda na kumuombea baba yake huku yeye tunamponda
 
Bunge lina nguvu labda hata zaidi ya udhaniavyo. Tusubiri tuone April kitakachotokea.

Suala la JPM kusema kuwa wabunge wa CCM wanataka kumng'oa PM linanipa ukakasi sana. Hivi kwa akili ya kawaida, ni nani mwenye ugomvi na Kasimu, nani anachukizwa na Kasimu. Yani wamng'oe Kasimu kwa lipi. Kuna mtu anaficha identity yake chini ya mwamvuli wa jina la Kasimu.

Lkn sidhani kama baba anaogopwa, kuna kislogan kinapenya sahivi kuwa "IMPEACH HIM".

Bunge lijalo litatupa jibu mkuu.
 
Kama kuna wanaompenda na kumuombea Baba; mimi kiukweli namuomba Mungu baba asimtumbue mwanae anayependezewa nae!!!

Ombi hilo ndo muhimu kwangu kwa sababu; ni mtoto huyu mtukutu na jeuri ndie atakayefanikisha kuonesha tabia mbovu na ovu ya baba mtu!! Kadri muda unavyopita bila baba kuchukua hatua dhidi ya mtoto huyu fedhuli na jeuri; ndipo watu wengi zaidi na zaidi wanapopata fursa ya kufahamu huyu baba ni baba wa namna gani!!!

Bado kuna maelefu kwa maelfu kama sio malaki miongoni mwetu ambao bado hawaoni wala kusikia haidhuru hata kama macho na masikio wanayo!!!

Baba huyu ambae nae ni jeuri na kiburi; kuchelewa kwake kumwadibisha mtoto wake mpenzi; kutakuwa ni muujiza pekee utakaowafanya vipofu waweze kuona na viziwi kusikia!!!

Kadri wanavyoleana ndipo watakavyozidi kupakana vinyesi na hivyo; hata yule atakayekosa fadhila za kuona na kusikia; basi ataweza kuupata uvundo unaoendelea kupitia pua zake!!
 
Mbona kama ukweli uko wazi kabisa...kila anachofanya mtoto kina baraka za baba yake..
Na pengine baba ndo anamtuma mtoto afanye anayoyafanya

Sasa mbona hasira ni nyingi sana kwa mtoto huku baba hatutaki kabisa kumuudhi?

wengine wanasema tunampenda na kumuombea 'baba mtu' huku wakizidi kumponda mtoto

huu unafiki unatusaidia nini?

Kwanini kama tunaona hatumuwezi baba mtu basi na mtoto tusimguse?
au haki na ukweli inatazama cheo?
CC:
Gwajima
Ruge n the like
 
Kama kuna wanaompenda na kumuombea Baba; mimi kiukweli namuomba Mungu baba asimtumbue mwanae anayependezewa nae!!!

Ombi hilo ndo muhimu kwangu kwa sababu; ni mtoto huyu mtukutu na jeuri ndie atakayefanikisha kuonesha tabia mbovu na ovu ya baba mtu!! Kadri muda unavyopita bila baba kuchukua hatua; ndipo watu wengi zaidi na zaidi ndipo wanapopata fursa ya kufahamu huyu baba ni baba wa namna gani!!!

Mtoto ukiona anakutukana na baba yake hasemi kitu basi katumwa

Sasa ukijifanya eti 'namuombea na nampenda baba yake' huku huyo mtoto unamlaani una matatizo
 
Mbona kama ukweli uko wazi kabisa...kila anachofanya mtoto kina baraka za baba yake..
Na pengine baba ndo anamtuma mtoto afanye anayoyafanya

Sasa mbona hasira ni nyingi sana kwa mtoto huku baba hatutaki kabisa kumuudhi?

wengine wanasema tunampenda na kumuombea 'baba mtu' huku wakizidi kumponda mtoto

huu unafiki unatusaidia nini?

Kwanini kama tunaona hatumuwezi baba mtu basi na mtoto tusimguse?
au haki na ukweli inatazama cheo?
Pambaneni na Magufuli, hao ni wasaidizi wake tu -NI UNAFIKI KUJIFANYA UNAMSIFU MAGU WAKATI NDIE DEREVA
 
Back
Top Bottom