Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) taifa, Hashimu Rungwe ameitaka Serikali kutoa ruzuku kwa hospitali zote nchini pamoja shule zote za msingi na sekondari ili wagonjwa wasio na ndugu wapate chakula bure huku wanafunzi ambao wazazi wao hawana uwezo wa kuchangia chakula shuleni, watoto wao wapatiwe chakula bure ili kudhibiti tatizo za utoro pamoja na udumavu kwa wanafunzi.