- kwa kuanza ninasema kwamba Rais, ameshindwa kuwachukulia hatua za kisheria wahusika wote wa ubaradhuli wa Richimond, ambao umeliletea hasara kubwa sana taifa letu, na haya yamethibitishwa na bunge letu kupitia kamati yake maalum ya Mwakyembe.
- Kamati hii ilifanya uchunguzi wa kisheria kwa mujibu wa katiba ya bunge laetu la jamhuri na kutoa mapendekezo kadhaa kuhusu watuhumiwa na adhabu wanazostahili, lakini mpaka leo serikali na hasa Rais, wameshindwa kuwachukulia hatua za kisheria, hasa zilizopendekezwa na bunge.
- Kwa kutowachukulia hatua wahusika, Rais amelidharau bunge la wananchi wa Tanzania na hata sisi wananchi tuliowachagua, na pia aamedharau sheria za jamhuri, hili ni tatizo lake Rais either anawaogopa watuhumiwa wa Richimond, au ni marafiki zake, au hajui wajibu wake kama Rais kwamba ndiye The Law Chief Enforcer wetu.
- Sasa hii ni moja ya sababu muhimu ya baadhi yetu wananchi kuamini kwamba serikali yake yaani Rais Kikwete, imeshindwa uongozi na ikibidi yeye na wenzake waachie ngazi, maana tunao wananchi wengi sana wenye uwezo wa kuongoza ipasavyo, ambao wataziheshimu sheria zetu badala ya kuzichezea kwa kutumia mahela yetu mengi sana kuigharamia kamati ya uchunguzi kama ya Mwakyembe na kuishia kuificha uvunguni ripoti yake.
Respect.