Harusi ni mipango yako binafsi, kwanini uninunie?

Harusi ni mipango yako binafsi, kwanini uninunie?

sinafungu

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2010
Posts
1,527
Reaction score
868
Nashangaa mtu anapanga kuoa, wakati huo hajui wewe umepanga nini? Sasa ukimwambia mimi sina hela kwa sasa kutokana na hali ilivyo, ananuna! Waswahili sisi tuna taabu.

Wanapokutana kwenye hivyo vikao vya harusi agenda ni mimi.

Jamani kila mtu ana majaaliwa yake katika kuzipata fedha, sasa mfuko wangu usiupangie matumizi.
 
Hata sifahamu mara ya mwisho kuchangia upuuzi wa harusi ni lini.


Hiyo hela afadhalia ukatoe sadaka isaidie yatima kuliko kuipoteza kwenye michango ya kipuuzi.
 
Kuchangia haruc si upuuzi bali ni kuonesha mshikamano na watu wengine ndani ya jamii,ukikataa kuchangia sasa kumbuka kua utakuja kua na watoto ambao watahitaji michango.
 
Hao wako wengi tena anafanya kukudai km vile alikukopesha. Ni ajabu unamnunia mtu kwakuwa hajachangia ndoa yah..hu si ux#¥e kabisa. papuchi ukale peke yako huko mm unijazie inzi na madeni. Sijachangisha harusi yangu wala si toi tena michango ya aina hii. jipange uowe basi...
 
@ Matola: kutembeza bakuli la ndoa si jambo geni kibaya hapa ni kumchukia mtu eti hajachangia harusi yakoama ya ndugu yako....huu ni upuuzi ndio mana nasema jipange kabla hujafikiria kuoa. Yaani tokea mnatongozana mnawaza michango yetu khe!..usipoelewa hapo we tena basi ii.
 
Utoto unawasumbuwa mkikuwa mtajitambuwa tu, mmeshavimbiwa makande mnaanza kubwabwaja tu.

Kuchangia ni jambo la hiyari kama wewe linakukera usichange haujavunja katiba ila kwa kifupi tu inaonesha bado hamjaijuwa vizuri dunia.



Wewe unayejielewa endelea kuchangia..
 
@ Matola: kutembeza bakuli la ndoa si jambo geni kibaya hapa ni kumchukia mtu eti hajachangia harusi yakoama ya ndugu yako....huu ni upuuzi ndio mana nasema jipange kabla ujafikiria kuoa..yaani tokea mnatongozana mnawaza michango yetu khe!..usipoelewa hapo we tena basi ii.

Msicomplicate mambo hata mimi siyo kama nachanga zote naangalia uzito wako kwangu. Otherwise mtu utafute dunia ya kuishi peke yako ili ukae mbali na jamii.
 
Hii ni culture ambayo inatutesa sana wabongo na hatuwezi imaliza mana imekua ni kama part ya maisha yetu"
 
Sasa utachangia nini wakati mtu mwenyewe mkata ufuta tu,kojoa ukalale tuache waajiri wa mkata ufuta tuchangie,eboo mchango tu mapovu hivo🙁
 
Nimeshagombana na marafiki 3 kisa sikuchanga kwenye harusi zao at that sikuwa na namna sababu nilikuwa na miezi miwili tangu niache kazi duuuh jamaa wakanuna hadi leo hatuongei
 
Mimi nimeoa miaka kadhaa iliyopita... Huu mfumo haukuwa kama ulivyo sasa.

Kuchangia ni jambo Jema sana, Linakuza mahusiano ya Kijamii... Pia unachangia chakula utakachokula siku ukija kwenye sherehe.

Fedha zote zinazochangwa zinatumika siku hiyo hiyo ya sherehe....
 
Usipochangia harusi,wabongo hawachangii msiba wako.

Mtaenda sawa tu,nae atakwambia ana mipango binafsi.
 
Cfanyagi huo ujinga,nachangiaga rambirambi kwenye misiba na michango mingne ambayo ni productive lakni sio harusi.
 
Back
Top Bottom