harusi bila kupimwa vvu......

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,502
Reaction score
911,255
Wachumba wengi hili hawataki kusikia
Lakini ukweli lazima tuuanike hadharani
Dunia yenu siyo ila ya enzi zetu kabisa
Utetezi wenu kuwa mbona hatukupimwa
Siyo utetezi kabisa, hiyo siyo busara lol!
Harusi bila kupimwa vvu, ni majuto ya mjukuu!

Harusi nimehudhuria nyingi mno, ama!
Kila harusi siku hizi minong'ono haiishi!
Eti mbona kapigwa, hivi naye vipi haoni?
Eti mbona dalili zote anazo, lakini kicheko!
Jibu hapo ni kupimwa ili ujiondolee shaka,
Harusi bila kupimwa vvu, ni majuto ya mjukuu!

Miaka michache tu baada ya nderemo
Utasikia eti anatupa mimba kila kukicha
Khofu hutanda kwa wanafamilia, kulikoni!
Lawama huanza kuzagaa kila mahala!
Vikohozi visivyo na tiba kuwagubika!
Harusi bila kupimwa vvu, ni majuto ya mjukuu!

Wanandugu hudai warithi wao wa kesho
Lakini hapa kitanda hata haramu hakizai!
Kisa ni mgeni kashamiri ndani ya miili yao.
Kila mmoja humtupia lawama mwenzio
Endapo wangelipima kabla ya shari hii..
Harusi bila kupimwa vvu, ni majuto ya mjukuu!

Kupima siyo kutokuaminiana ila ni kukiri
Kwa kutambua dunia tuliyopo siyo mchezo
Changamoto zake nazo siyo masihara kamwe
Msipopima kila mmoja rukhsa kulaumu mwenzie
Mchafuzi naye kupewa ahueni bila ya shubiri
Harusi bila kupimwa vvu, ni majuto ya mjukuu!

NB.:- In the memory of a passionate friend who noisily passed away last week
......leaving the loser to enjoy it all..............how sad as it lasts!

 
watu wapime nini wakati washabanjuana kavukavu siku nyiiingi.

On a serious note, kupima muhimu sana basi tu ni uzembe.

Kuna dada mmoja alifoji cheti cha HIV wakati anajifahamu ni HIV+, akaolewa na kijana wa watu.

Matokeo yake, wote kwa sasa wameshatangulia mbele ya haki.

Hata mtu anayejifahamu ni HIV+ alinde wanamzunguka, kuwaambukiza watu kusudi it's very unfair jamani.
 

Kongosho point taken........................hata kabla hawajaanza kubanjuana inabidi wajipimie kuona kama kina watakiweza...............na hili gonjwa lina laana fulani aliyenao furaha yake ni kusambaza sijui kwanini?
 
ni kweli

afu kupima hata dk 5 haziishi ila watu wabishi kweli
wakati ni kwa faida ya wote

mtu mwingine anaweza kuwa HIV+ na hajijui, ila anaposhauri kupima anaonekana 'mnoko'

kweli nadhani huu upimaji kabla ya mahusiano upewe msisitizo zaidi.

Kongosho point taken........................hata kabla hawajaanza kubanjuana inabidi wajipimie kuona kama kina watakiweza...............na hili gonjwa lina laana fulani aliyenao furaha yake ni kusambaza sijui kwanini?
 
Mkuu ruttashubanyuma pole sana na msiba mzito uliokupata wa rafiki yako. Umesema ukweli sana lakini kinachowasymbua watu wengi ni hofu ya mapito yao. Inafikia stage mtu kupima ni kama kumwambia akabiliane na kifo na hivyo kutokuwa tayari kwa tendo hilo huku akiendelea kugegeda watu kavu kavu na kupelekea hatari hata kama hajaathirika!!!!

Kikweli hali inatisha na ukifanya utafiti ndoa nyingi za siku hizi zinafungwa baada ya kuwa wahusika wameshagegedana sana na hata matunda kuonekana na kukimbilia kuzima moto kwa kufunga ndoa haraka haraka. Kama walipima inakuwa ni siri yao ila mama ndiyo hutumika kama deep stick akienda clinic,
 
Last edited by a moderator:
ni kweli

afu kupima hata dk 5 haziishi ila watu wabishi kweli
wakati ni kwa faida ya wote

mtu mwingine anaweza kuwa HIV+ na hajijui, ila anaposhauri kupima anaonekana 'mnoko'

kweli nadhani huu upimaji kabla ya mahusiano upewe msisitizo zaidi.

Kongosho kwenye mahaba khofu kubwa kwenye hili ni kutemwa..................baada ya kugundulika afya imegoma na kuonekana pengine ulizidisha kipimo.......lakini akupendaye si anatakiwa aone mapungufu yako ni chongo? Kama ni kudu mibadala si ipo kibao ya kuwafariji na hata kujipatia mtoto kwa njia ya salama. Na anayekupenda kiukweliukweli hawezi kukuficha na atakulinda...............................huyo asiyetaka umjue undani wake huyo ana lake jambo........
 

Mzee wa Rula nimependa hii ya mama akienda kliniki ndiyo inakuwa "deep stick" yao..................at that time the plane has left the airport.......................it is a case of too little too late........elimu ya nasha bado yahitajika na kututia matumaini badala ya kuukimbia ukweli wa afya zetu.........ukweli tusipoukubali utatuua.......
 
Hi Konnie, hi uncle Ruta...
Mapenzi yakiwa bado mabichi kabisa,kabla hawajavuliana nguo,inabidi washauriane,wakapime.
Na ni woga wa bure kwani kule kuna qualified counsellors,hupimwi tu na kupewa majibu. Mi nimesoma counselling ya Ukimwi. Kuna hatua zake..mpaka mteja hatua ya mwisho anaulizwa kama yuko tayari kuyapokea majibu,na je yakiwa pos atachukuliaje,na yakiwa neg pia,atayachukuliaje.
Couple nayo ina namna yake,kila mmoja kivyake,kisha wakati wa majibu pamoja.
Process ya dk 15 hivi kwa kichwa.
 
kaka umeenda mbali sana watu wanatakiwa wapewe elimu ya kupima wenyewe
na ikiwezekana badala ya kuweka ndomu kwenye magest waweke vipimo kabla ya
watu kudo wapimane wao wenyewe.
maana vijana wengi wanakua wanachakachuana kabla yandoa.
 
Mpaka ndoa ndio kupima? That's too late inabidi wapime baada ya kukubaliana kuwa wapenzi na baada ya kukuta wapo -ve wanendelee kuwa waaminifu ktk relationship yao.
 
Tatizo ukipima siyo mwisho wa maambukizi! Au ukimwi uliopatikana kabla ya ndoa unatesa zaidi ya ule wa ndani ya ndoa?

Issue kubwa ni kubadilika!
 

Hili ndilo tatizo kubwa sana, wengi wanakuwa weshabanjuana miaka kadhaa nyuma hivyo hawaoni sababu ya kupima tena.
It is very serious kwakweli.
 

Kwa bongo hii, wenye uelewa na mapenzi ya hivyo wachache sana. Nimeshuhudia couple moja au mbili tu.
 
Kwa bongo hii, wenye uelewa na mapenzi ya hivyo wachache sana. Nimeshuhudia couple moja au mbili tu.

Kaunga ni lazima uwe umebarikiwa kuwa na mapenzi ya kweli ..............hayo siyo ya kila mtu ....wengi ni "mtumikie kafiri upate mradi wako........."
 
Kwa kweli kupima kabla ya ku do ni vizuri sana but life after HIV TEST na ukigundulika ni positive ni mtihani mkubwa!
 
Hili ndilo tatizo kubwa sana, wengi wanakuwa weshabanjuana miaka kadhaa nyuma hivyo hawaoni sababu ya kupima tena.
It is very serious kwakweli.


Kaunga ili iwe isiwe serious ni kujipitisha kwenye king'amuzi
 
Tatizo ukipima siyo mwisho wa maambukizi! Au ukimwi uliopatikana kabla ya ndoa unatesa zaidi ya ule wa ndani ya ndoa?

Issue kubwa ni kubadilika!

MESTOD waswahili husema kheri nusu ya shari kuliko shari kamili. Atabadilikaje leo? Jua afya yako na mengineyo hayategemei maamuzi yako tu bali ya yule ambaye umeamua kumwamini naye yukoje...........huyu jamaa yangu yeye alikuwa hajishughulishi na alikuwa anapima mara kwa mara lakini hakuwa na ubavu wa kumwomba mwenzie kujua khali halisi ikoje upande wa pili.......................hadi pale alipoona ngozi yake imeanza kubadilika.....................he was getting darker and darker............................ndipo alipomkokota mwenzie......................na alishangazwa kuona....it was a done deal............................akashangaa mbona mwaka jana nilipimwa pekee yangu na matokeo ni haya.......................negative?
 
Kwa kweli kupima kabla ya ku do ni vizuri sana but life after HIV TEST na ukigundulika ni positive ni mtihani mkubwa!

NATA hata asipopimwa ni kuwa mhusika ataendelea kujidanganya kuwa mambo ni shwari hadi pale atakapoanza kuumwa na dawa zigomee kumtibu ndipo ataanza kujiuliza maswali ya msingi na hata kuishi kwa matumaini iinakuwa ngumu kama khofu imetanda kila mahali............
 
Life is full of suprise..

Kusema kweli sijawahi kushuhudia harusi ambayo bibi harusi anaolewa hana mimba au hajazaaa..

Sasa kama mtu anaolewa tayari ameshazalishwa au na mimba ya nini kupima vvu wakati mzigo wameshapeana sana hadi kuzalishana?

Kizazi cha dot com na mdogo wake digitali Mungu atuhurumie kwa kweli
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…