Hari ya Dr. Olimboka ni kizungumkuti yadaiwa madaktari wanamtegemea Mungu kupona. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hari ya Dr. Olimboka ni kizungumkuti yadaiwa madaktari wanamtegemea Mungu kupona.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Return Of Undertaker, Jul 8, 2012.

 1. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,368
  Likes Received: 8,430
  Trophy Points: 280
  HALI ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari hapa nchini, Dk. Stephen Ulimboka, inazidi kuzorota na madaktari walio karibu naye wamelidokeza Tanzania Daima Jumapili, kuwa sasa wanasubiri ‘Kudra’ za Mwenyezi Mungu’

  Kiongozi huyo ambaye alitekwa, kuteswa na kutupwa katika msitu wa Mabwepande jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi uliopita anatibiwa katika hospitali moja nchini Afrika Kusini ambayo hadi sasa haijawekwa wazi.

  Mmoja wa madaktari ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini alisema kiongozi huyo aliyelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi yumo katika ‘koma’, ambayo ni hali ya nusu mfu - nusu hai, na anahitaji zaidi sala za Watanzania.

  “Huwezi kusema anaendelea vizuri, jambo muhimu hapa ni kumwomba Mungu awaongezee maarifa madaktari wale ili kupigania uhai wa mwenzetu.

  “Kwa hali aliyoondoka nayo hapa nchini na jinsi tunavyopokea taarifa kutoka huko, kwakweli hazileti matumaini,” alisema Dk. huyo.

  Dk. Ulimboka inadaiwa amepata madhara makubwa katika figo zake ambapo ilidaiwa moja ilipata ufa na nyingine iligoma kufanya kazi, baadhi ya mbavu zake zimepata majeraha.

  Kichwa cha daktari huyo pia kilipata hitilafu kutokana na kipigo hicho kinachodaiwa kufanywa na maofisa Usalama wa Taifa ingawa serikali imekana kuhusika na kitendo hicho cha kinyama.

  Baadhi ya madaktari waliozungumza na Tanzania Daima Jumapili jana jijini Dar es Salaam katika mkutano na viongozi wa dini wamesema ukweli wa kipigo cha kiongozi huyo hautawekwa wazi.

  Walibainisha kuwa hawana imani na tume itakayoundwa au iliyoundwa kushughulikia jambo hilo kwa sababu tayari viongozi wa serikali wamesema serikali haihusiki.

  “Rais, waziri wamesema serikali haihusiki na tukio hili, sasa kama tume ikibaini kuna mkono wa serikali ukweli utawekwa wazi hapo?” alihoji mmoja wa madaktari.

  Tanzania Daima Jumapili liliwasiliana na Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania, Namala Mkopi, kuhusu afya ya Dk. Ulimboka ambapo aligoma kuzungumzia suala hilo.

  Dk. Mkopi alisema jana walikuwa kwenye mazungumzo na viongozi wa dini kuhusu mgomo wa madaktari na si vinginevyo.

  Viongozi wa dini waingilia

  Wakati hali ya Dk. Ulimboka ikizidi kuwa tete, viongozi wa dini nchini wamemtaka Rais Jakaya Kikwete akutane nao pamoja na madaktari ili kuupatia ufumbuzi mgomo wa madaktari.

  Viongozi hao walisema mgomo wa madaktari unaoendelea hivi sasa unawatesa wananchi wasio na hatia.

  Kauli ya viongozi hao wa dini ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Sheikh Said Mwaipopo mara baada ya kikao chao na madaktari.

  Sheikh Mwaipopo alisema wamechukua hatua hiyo baada ya kubaini kuwa serikali inasuasua kulizungumzia jambo hilo kwa makini na kulipatia ufumbuzi ili kuokoa maisha ya watu wa kipato cha chini wanaotegemea hospitali za serikali.

  “Kuna mambo mbalimbali yanaweza kutokea, inawezekana taarifa sahihi hazimfikii Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, hivyo tunaomba kukutana naye kwa mazungumzo ya amani ili kurudisha hali ya amani nchini,” aliongeza Mwaipopo.

  Sheikh Mwaipopo alifafanua kuwa tamko lao limejigawa katika sehemu kuu tano, ambapo wanaamini kukutana huko kunaweza kuwa ishara ya kumaliza mgogoro unaowakabili na kutafutiwa ufumbuzi wa haraka.

  Alisema miongoni mwa mambo waliyoazimia ni kuitaka serikali ifute kesi iliyoifungua Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi, ambayo ilitoa zuio la mgomo huo.

  Aliongeza kuwa pia wameitaka iwarejeshe madaktari wote walioachishwa kazi pamoja na Rais Kikwete akubali kukutana na viongozi wa dini, wanaharakati wa haki za binadamu na madaktari.

  Naye Mchungaji wa EAGT Mabibo, Lawrence Mnzavaz, alisema hawahusiki na tuhuma zinazovumishwa kuhusu tukio lililotokea la Dk. Ulimboka, kwa sababu hakuna aliyeshuhudia uovu huo unavyofanyika.

  Alisema tamko lao halitakubaliana na kauli ya aina yoyote itakayowataka wananchi kuandamana, kwani wanaamini hiyo si njia sahihi ya kumaliza tatizo lililopo.

  Kiongozi huyo alisema iwapo rais atashauriwa vibaya na kukataa kukutana na umoja wa viongozi hao, hawatakuwa na la kufanya kwa sababu maamuzi hayo yatakuwa yamefanywa na kiongozi wa nchi.
   
 2. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Good movie,issue ni je serikali watakubaliana na hayo masharti na ukizingatia bajeti imeshapita bila mahitaji ya madr.Tatizo la serikali wanalichukulia hii suala kisiasa kwamba wakikubali kutekeleza matakwa ya maDr. Watakuwa looser.
   
 3. M

  Makupa JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Huyu mwaipopo nahisi ni msomi mzuri tofauti na viongozi wengine wa dini
   
 4. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2012
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,745
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Ee Mungu mponye mja wako
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Jul 8, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Ee Mwenyenzi Mungu tenda muujiza wako! Tunaomba umponye Dr. Ulimboka, si kwa mapenzi yetu, bali mapenzi yako yapate kutimizwa!
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  Jul 8, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Nafikiri labda wanatumia diplomacy kidogo kudai kuwa "waziri hapati taarifa sahihi" na "rais anashauriwa vibaya." taarifa zote Zilizoko hewani ni vigumu kwa waziri "kupewa taarifa sizizo sahihi" au kwa "rais kushauriwa vibaya" wakati kila kitu kiko wazi. Sababu ya yote ni neno moja tu: DHAIFU.

  Sasa hivi nimeanza kuamini kuwa Kikwete anbaweza kuua mtu kwa sababu binafsi tu. Kama kweli aliagiza au aliruhusu matendo aliyotendewa Dr. Ulimboka, basi si vigumu kwake kutengeneza mazingira yaliyompeleka Babu Seya pamoja na watoto wake wote jela kutumikia kifungo cha maisha kama ilivyowahi kudaiwa huko nyuma.
   
 7. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Zomba pingana Na Sheikh Mwaipopo umezoea sana kuwapinga madaktari
   
 8. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,740
  Trophy Points: 280
  Mungu saidia
   
 9. Z

  Zero One Two JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2012
  Joined: Sep 16, 2007
  Messages: 9,390
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Mawazo ya kidhaifu, Serikali dhaifu, Viongozi dhaifu mnategemea nini hapo?
   
 10. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Eti bado kuna watu wanasema kuna Usalama wa taifa,wameshindwa kazi hawa watu
   
 11. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mwaipopo ni mhadhiri wa kiislamu,mzaliwa na mkulia Kyela na kwingineko Tz, anayezunguka huko na kule kuushambulia ukristo. Elimu yake mmmh, atakwambia Rev Fr Masanilo, ukiwa na muda tembelea kijiwe chao pale K'koo karibu na kituo cha mabasi yanayokwenda Tandika.

  Historia yake ni kuwa alikuwa mkristo akabadili dini kwasababu ya mke.

  [/B]Ni majibu na ufafanuzi mdogo
   
 12. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #12
  Jul 8, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  tumwombea mwenzetu,Mungu amponye
   
 13. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #13
  Jul 8, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,823
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  Ukiona nchi inaua wataalam Wake ujue hiyo ni nchi iliyokufa!!!
   
 14. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Tutalipa kisasi akifa
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Jul 8, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  "Hari" ndio gari yake?
   
 16. Straight corner

  Straight corner JF-Expert Member

  #16
  Jul 8, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kila nisikiapo mkasa wako (Dr) nayahisi maumivu uliyoyapata, ila haya siku zote ni matokeo ya harakati za kudai haki ktk mfumo kandamizi. Pole sana!
   
 17. m

  mugumu Member

  #17
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Mbona maelezo na habari zinazotolewa kuhusu Dr ulimboka zinafanana sana na za Nyerere alipokuwa amelazwa uingereza?ni vizuri sasa tuwekane wazi.........Tanzania bwana!!
   
 18. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #18
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160

  Ameeeeen!

  Hakika MUNGU aliye hai anaweza yote juu na chini ya jua hili!
  Na hakika atafanya maajabu kwn tumeshamwambia ktk IMANI!
   
 19. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #19
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160

  Hivi wewe mtumwa,hauwezi hata kutambua wala kuona?
  Achana na ugamba kijana wetu!
  Utakuja jutia mawazo yako ulikoelekeza.

  Shtuka mapema mtumwa wee!
   
 20. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #20
  Jul 8, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,947
  Likes Received: 1,272
  Trophy Points: 280
  Mungu msaidie apone! Invisible weka namna ya kumchangia. Siyo zile namba za tusiowafahamu
   
Loading...