Happy birthday Mwaka Mpya: Nimemwagiwa maji kitandani

Mkogoti

TAPELI Mkubwa
May 3, 2020
2,416
3,911
Sina zaidi ya salaam maana naona ata uvivu kuandika, nasema haiwezekani

Leo nipo nimelala zangu kitandani mara naskia Mwaaaaa nakurupuka ni nini nakutana na kitu maji yamejaa kitandani sio godolo sio shuka vyote chapa chap, nauliza kulikoni eti siku yangu ya kuzaliwa,

Tena angalau wangechukua kikombe angalau vi maji vya kuzugia ndoo nzima haki ya nani hawa walikuwa wanataka kuniua, leo niliona nivute mpaka saa nne hivi maana kuna ka ubaridi na mvua kidogo hawa wameharibu kabisa utaratibu.🤒

Nilikuwa nimelala na nguo yangu ya sikukuu pembeni nayo imeloana na yani waombe jua liwake leo lisipowaka haki ya nani leo naua, sijui ata usiku wa leo nalalaje nilale chini kweli kwa ajili ya hawa wehu?

Nipo nimejaa hasira nimefutuka nimevimba karibia nataka kupasuka nazunguka tu chumba kizima sijui ata mlango wamefungua funguaje? Awa kazi yao nyingine nahisi ni wezi, majambazi, majizi, ma vibaka, mavuta bangi, ni bora kuwatukana tu😡

Yani da! Mwaka huu nimeanza hivi na huko mbeleni MUNGU TUSAIDIE HERI YA MWAKA MPYA 2021 WANA JF

🤦🤪🏃
 
Mimi huu ujinga wa kumwagiana maji sijawahi ufanya na sitaki kufanyiwa.
 
Haya mambo ya kufurahia birthdays kwenye mitandao ndiyo yaliwarahisishia polisi kumkamata Hushpuppy Dubai.
 
Ulitumwa utaje Siku yako ya kuzaliwa?,ungemwagiwa maji ya ukoko wa ugali ingependeza zaidi
 
Sina zaidi ya salaam maana naona ata uvivu kuandika, nasema haiwezekani

Leo nipo nimelala zangu kitandani mara naskia Mwaaaaa nakurupuka ni nini nakutana na kitu maji yamejaa kitandani sio godolo sio shuka vyote chapa chap, nauliza kulikoni eti siku yangu ya kuzaliwa,

Tena angalau wangechukua kikombe angalau vi maji vya kuzugia ndoo nzima haki ya nani hawa walikuwa wanataka kuniua, leo niliona nivute mpaka saa nne hivi maana kuna ka ubaridi na mvua kidogo hawa wameharibu kabisa utaratibu.🤒

Nilikuwa nimelala na nguo yangu ya sikukuu pembeni nayo imeloana na yani waombe jua liwake leo lisipowaka haki ya nani leo naua, sijui ata usiku wa leo nalalaje nilale chini kweli kwa ajili ya hawa wehu?

Nipo nimejaa hasira nimefutuka nimevimba karibia nataka kupasuka nazunguka tu chumba kizima sijui ata mlango wamefungua funguaje? Awa kazi yao nyingine nahisi ni wezi, majambazi, majizi, ma vibaka, mavuta bangi, ni bora kuwatukana tu😡

Yani da! Mwaka huu nimeanza hivi na huko mbeleni MUNGU TUSAIDIE HERI YA MWAKA MPYA 2021 WANA JF

🤦🤪🏃
Heri ya kuzaliwa na Mungu akujalie mafanikio mema.
 
Back
Top Bottom