Hapo ndo kwetu! Mje Sasa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hapo ndo kwetu! Mje Sasa!

Discussion in 'Jamii Photos' started by Pukudu, Aug 10, 2012.

 1. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  ImageUploadedByJamiiForums1344571831.583546.jpg
  Tumewaambia kabisa mje Sasa tuone!
   
 2. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Hivi kweli waIslam mmedhamiria hili jambo? Kweli hili limepata 'kibali' mbele ya Allah? Tusubiri tuone...
   
 3. UncleUber

  UncleUber JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 4,945
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  upuuzi mtupu
   
 4. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  duh kali kuliko . je mawakala nao wamekataa au kwa vile kuna posho??
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Inamaanisha nini hii?
  Isn't this Insinuation?....kama hujachonga mwenyewe maandishi hayo sema umeyapata wapi!
   
 6. cmoney

  cmoney JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 1,224
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Si nilisikia ni kosa la jinai hili?duh basi makarani itabidi watembee na ffu
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  mtahesabiwa tu hata kwa viboko..
   
 8. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #8
  Aug 10, 2012
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,900
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Namuhurumia karani atakayepangiwa eneo hilo.....
   
 9. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Itabidi mpimwe akilizenu nyie.
   
 10. piper

  piper JF-Expert Member

  #10
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 3,260
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mmmmmmmmmmhhhhh!!!!!!!!!!! hii umejitengenezea, big up 4 trying
   
 11. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #11
  Aug 10, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Hapo ndani pakiingizwa up...u watoka na kuhesabiwa mmoja mmoja!
   
 12. happiness win

  happiness win JF-Expert Member

  #12
  Aug 10, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,478
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0


  Iko wapi? Nielekeze nataka kuja
   
 13. Mandown

  Mandown JF-Expert Member

  #13
  Aug 11, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 1,577
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  mie ni muislamu, lakini sijajua mantiki ya kugomea sensa.

  kwa ninavyo fahamu mimi, madhumuni ya sensa ni kusaidia kupanga maendeleo. mathalani, waweza kusonga ugali bila kujua idadi ya walaji? mfano mwingine dhahiri wa sensa nipale janga la njaa linapo tokea utajua mahitaji halisi ya wahanga, idadi kuamua pahala pa kuweka huduma muhimu kama soko, ama zahanati, ama vituo vya pollisi ama idara za mahakama, ni kutokana na idadi ya watu katika eneo husiki. maa muzi kama kugawa wilaya kuwa mkoa, na kuunda tarafa nyinine, ili kuharakisha maendeleo. mambo haya si dhani kama UISILAMU UNAKATAA
   
 14. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #14
  Aug 11, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  BRODA, hawa waislamu wenye ufinyu wa mawazo wanasikitisha sana.
  Ni bahati nzuri kuwa mpo baadhi wenye uelewa mzuri ambao bila shaka mtasaidia kuerevusha jamii yenye kutu kichwani.
  Nilitegemea Waislamu wagome kuwa hawahesabiwi hadi kesi zote za wezi wa mali ya umma zifanyiwe kazi, kumbe wao udini mbele.
   
 15. Achahasira

  Achahasira JF-Expert Member

  #15
  Aug 11, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  uislamu hau katazi sensa kama itakuwa ni ya kuridhisha,lkn tuna kata kuhesabiwa kwendana na serikali kuto kukubali madai yetu,  kama bado hujuwi basi soma hapa chini  KWA NINI WAISLAMU TUNAKATAA KUSHIRIKI KATIKA SENSA 2012
  Nchi yetu imefanya sensa sita hadi sasa, mbili wakati wa ukoloni (1948,
  1957) na nne katika Tanzania huru (1967, 1978, 1988 na 2002). Mara
  zote hizo, waislamu wameshiriki sensa wakiamini kwamba ni zoezi
  muhimu kwa maendeleo ya Taifa na hawakuwa na sababu ya kususia
  sensa kutokana na historia ya dini yetu kuhimiza sensa.
  Tatizo lililojitokeza mwaka huu na kupelekea waislamu kuamua kuisusia
  sensa ijayo mwaka huu lilianzia na taarifa ya TBC1 iliyotolewa tarehe 26
  Aprili, 2012 kwamba idadi ya wakristo nchini ni 52% na waislamu ni 32%.
  Takwimu hizi sasa zinatumika kuhalalisha mgawanyo mbovu wa nafasi
  za madaraka nnchini kwamba wakristo ni wengi katika nafasi mbali mbali
  kwa sababu wao ni wengi.
  Pamoja na Mkurugenzi wa TBC1 kukanusha mara kadhaa kwamba
  takwimu hizo si sahihi, tumeng’amua kwamba kuna udini katika zoezi
  zima la sensa na tayari kuna takwimu za idadi ya watanzania kwa dini
  zao ambazo zinaonesha kuwa wakristo ni wengi kuliko waislamu na pia
  kuna matumizi mabaya ya takwimu za sensa dhidi ya waislamu.
  Udini katika zoezi la Sensa.
  Mosi, Tumekuwa tukifuatilia zoezi la majaribio la sensa lililofanyika
  mwanzoni mwa mwaka huu na tulichogundua ni kwamba maafisa
  walioenesha zoezi hilo wengi wao walikuwa wakristo hadi dereva wa gari
  hata maeneo ambayo waislamu ni wengi.
  Katika mazingira haya na huku tayari kukiwa na takwimu zinazoonesha
  idadi ya watanzania kwa mujibu wa dini zao zinazotolewa kupitia vyombo
  vya habari vya serikali, ofisi na idara za serikali, tovuti mbali mbali za
  taasisi za Kikristo na za asasi nyingine zisizo za kiserikali za ndani na nje
  ya nchi, tukishiriki katika zoezi la sensa lijalo tutayapa nguvu tu madai
  yao kwamba wakristo nchini ni wengi kuliko waislamu.
  Mifano ya takwimu hizo
  Tovuti ya wakatoliki – Wakristo 44%, Waislamu 34%
  Kalenda Ofisi ya Serikali – Wakristo ,Waislamu
  Tovuti ya Mambo ya Nje Marekani – Wakristo 62%, Waislamu 32%
  Pili, viongozi wa Kikristo wamekuwa msitari wa mbele kupinga kutiwa
  kipengele cha dini katika dodoso la sensa. Katika mazingira ya takwimu
  tata ambazo hata Mkurugenzi wa idara ya takwimu anakiri kwamba si
  takwimu sahihi ombi letu la kuwekwa kipengele cha dini katika dodoso la
  sensa lingepokelewa kama ufumbuzi wa utata huo ili tuwe na takwimu
  sahihi za idadi ya watanzania kwa dini zao lakini serikali imekataa kata
  kata na inaunga mkono msimamo wa wakristo kutokuwekwa kipengele
  cha dini katika dodoso la sensa, wakristo ambao tayari wanadai wao
  wako wengi kuliko waislamu.
  Tatu, dodoso la sensa limeandaliwa kuja kunufaisha wakristo kwa sababu
  linauliza kuhusu idadi ya makanisa na misikiti wakati serikali imekataa
  kuhusisha sensa na dini. Tuna shaka kwamba huu ni mpango wa
  kuwawezesha wakristo kuchakachua takwimu hizo za majumba ya ibada
  kuthibitisha kwamba wao ni wengi kuliko waislamu kama ambavyo tayari
  wanadai.
  Izingatiwe kwamba idadi ya makanisa itakuwa kubwa kuliko misikiti
  kutokana na tofauti za kimadhehebu za wakristo hata pale ambapo wao
  si wengi kwani katika Ukristo waumini wa dhehebu moja hawawezi
  kufanya ibada katika Kanisa lisilo la dhehebu lao. Katika kijiji utakuta
  makanisa manne mpaka matano au zaidi lakini msikiti ni mmoja tu
  kutokana na ukweli kwamba waislamu huswali msikiti wowote hivyo
  hawawezi kuwa na misikiti mingi kama makanisa.
   
 16. Mangaline

  Mangaline JF-Expert Member

  #16
  Aug 11, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nimependa msimamo huo. Big up!!!!!
   
 17. Mandown

  Mandown JF-Expert Member

  #17
  Aug 11, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 1,577
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  nime kuelewa,

  lakini nadhani hizo takwimu ni sampuli tu ambazo zinaweza kuwa sahihi ama sio sahihi, ndio maana zina tofautiana kutaka taasisi moja na nyingine. mathalani, wakati wa uchaguzi mkuu taasisi ya REDET na SYNOVET walitoa takwimu za ushindi wa raisi KIKWETE , makadirio ya kitafiti ambayo hayakuwa ya sahihi ( accuracy) kwa asilimia mia kwa mia lakini yalikuwa yanakaribiana na kutupa picha ya mwelekeo wa matoke wa uchaguzi mkuu mwaka 2010. makanisa na balozi walichukua sampuli na kutoa makario ya idadi ya waisilamu na wakristo, lakini hakuna sensa iliyo fanyika ndio maana takwimu zao zina tofautiana , kama ilifanyika basi walisahau kunihesabu.

  kwanini makanisa yana hitaji takwimu za idadi ya waisilamu na wakristo

  • tuwaachie wenyewe wanajua ndio maana wanazo

  kwanini Bakwata itahitaji takwimu za idadi ya wakristo na waisilamu:
  • kwasababu uisalamu ni dini ya kweli lazima dunia ikombolewe, dhima hii kwa tanzania wanayo BAKWATA na nilazima wajue wana watu wangapi na ipo kazi kiasi gani kuongeza ushawishi kwa makafiri (au walio kufuru) ili KUSILIMU
  • kwasababu bakwata inahitaji kupanga maendeleo ya waisilamu, ikiwa ni misikiti, madrasa, shule, vyuo vikuu . hivi ukienda bakwata ukiuliza Tanzania ina waisilimu wangapi, kati yao wanawake ni wangapi, na wanaume ni wangapi, na kati ya hao wana elimu kiasi gani (elimu dunia na akhera). takwimu hizi ni za msingi bakwata kuwa nazo ili kupanga maendeleo ya muisilamu mmoja mmoja na kwa makundi

  hili la TBC kuwa na Takwimu hizo , labda watakuwa wamechukulia huko huko kwa makanisa na sioni tatizo la matumizi ya takwimu hizo kwa shirika hilo la utangazaji

  hitimisho

   
 18. kamwendo

  kamwendo JF-Expert Member

  #18
  Aug 11, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 80
  Nimewaelewa na ninakubaliana nanyi Bw.Achahasira na Mandown ila sidhani kama ni jambo jema kususia sensa tukumbuke hao wakristo ni makafiri ambao malipo yao ni hapa hapa duniani si vyema kubishana na makafiri kwa kuwa tunapoteza muda na nguvu ambazo tungezitumia kuimarisha uislamu.
   
 19. Achahasira

  Achahasira JF-Expert Member

  #19
  Aug 11, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  kamwendo,


  kwa uchunguzi nilioufanya kwa majamaa na marafiki wote wanao susia sensa ni kuwa hawapendezwi na njia hiyo lkn hawana njia nyingine ya kuonesha msimamo wao juu ya serikali.

  serikali mara nyingi imekuwa ikiwachukulia waislamu ni bakwata hata kama wakijuwa bakwata HAIPENDWI NA HAIKUBALIKI na waislamu wengi.hii ndio moja ya sababu kuu ya kususia sensa inaweza kuonekana ni ndogo lkn hii tatizo ndio linalo zaa matatizo mengine yoooote ya leo na ya kesho.

  uislam sio dini ya kuingia msikitini na kutoka tu,uislam ni mfumo kamili wa maisha ya mwanadamu.

  mtume muhamad salalahu aleyhi wasalam alijenga taifa la kiislamu madina,ikumbukwe taifa lake lilikuwa na mayahudi na wapagani wengi tu.hakufundisha waislamu kusali msikitini na kuto kuleta mabadiliko katika yale wanayo yaona si sawa.

  uislamu upo kwaajili ya kupigania haki kwa wote,hii inaweza kuwa ni kitu kigeni kwenye macho ya baadhi ya waislamu na wakristu.kama nchi inakandamiza sehemu mmoja basi tuna WAJIBU wakukemea kwa vitendo au hata kuonesha kuwa tumechukizwa.

  serikali imekuwa ikiwapa nafasi kubwa makanisa kuliko waislamu kwa madai ya makanisa kuwa wao wapo wengi,na wakirusha takwimu za makanisa kwenye vyombo vya habari na wakijua kuwa takwimu hizo sio za ukweli kabisa.

  ni kitu cha wazi kabisa kuwa nchi hii imegawanywa na makundi mawili ya kidini,na serikali kunyamazia haisaidi chochote bali huleta maafa tu mbeleni,serikali ina wajibu wakusikiliza madai ya waislamu na kuyafanyia kazi,hii itasaidia katika maendeleo ya nchi kwa badae,


  ndugu kamwendo na imani kuwa umesoma hata kidogo siraa ya dini yako basi ningekuomba upitie.
   
 20. Bamukunda

  Bamukunda JF-Expert Member

  #20
  Aug 12, 2012
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Achahasira Ulichoandika ni hatari. Ukumbuke Kuwa huwezi kulazimisha mawazo Yako yakubaliwe na Watu wote. Mtoa takwimu katika nchi yeyote ni mtakwimu mkuu wa Serikali. Achana na takwimu za tovuti hata vyombo vya habari. Umeambiwa Kuwa tangu uhuru Serikali iliamua kuachana na maswali mawili yaani dini na kabila ili kujenga mshikamano. Nadhani ulijionea matatizo ya ukabila yalivyotaka kuisambaratisha Kenya wakati wa uchaguzi. Huko Nigeria unaona udini unavyowatafuna. Kwa maoni yangu Huku ni kuondoa umaskini kwa kutumia mgongo wa dini hasa pale unaposema .........Tumekuwa tukifuatilia zoezi la majaribio la sensa lililofanyika
  mwanzoni mwa mwaka huu na tulichogundua ni kwamba maafisa
  walioenesha zoezi hilo wengi wao walikuwa wakristo hadi dereva wa gari
  hata maeneo ambayo waislamu ni wengi........
  naomba nikujuze Kuwa ingawa Mimi ni binti wa kiisilamu siliungi mkono maana nisingependa nipate kazi kwa vile ati pengine kwa sababu ya ujinsi au imani yangu.

  Pia umenena........

  dodoso la sensa limeandaliwa kuja kunufaisha wakristo kwa sababu
  linauliza kuhusu idadi ya makanisa na misikiti wakati serikali imekataa
  kuhusisha sensa na dini. Tuna shaka kwamba huu ni mpango wa
  kuwawezesha wakristo kuchakachua takwimu hizo za majumba ya ibada
  kuthibitisha kwamba wao ni wengi kuliko waislamu kama ambavyo tayari
  wanadai........

  Hapa pia Nadhani hujafanya utafiti wa kutosha. Ni Kweli Kuwa wakati wa sensa ya majaribio kulikuwa na section iliyohusu huduma za jamii ikijumuisha Shule, hospitali, upatikanaji wa maji, matukio yaliyotokea katika Jumuia, matundu ya vyoo katika Shule, idadi ya waalimu n.k. Kama ujuavyo ile ilikuwa ni pilot na baada ya kufanya uchambuzi ikaonekana section Hii haikuwa na tija ikaondolewa. Naomba nikuthibitishie mwislamu mwenzangu Kuwa swali linalohusu idadi ya makanisa au misikiti halipo katika dodoso la sensa.
   
Loading...