kibogo
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 9,739
- 4,732
Pinda atembelea eneo la tukio
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alifika eneo hilo saa 3:41 asubuhi, kujionea hali ilivyo, lakini hakutoa tamko lolote. Sina la kusema, alisema Waziri Mkuu alipoulizwa na waandishi wa habari kutoa kauli ya serikali kuhusiana na tukio hilo.
Hata hivyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi aliyefuatana na Pinda, alisikika akimwagiza Kamanda Kova kuhakikisha mchora ramani wa jengo hilo naye anatiwa nguvuni kwa kuwa jengo hilo lilikuwa la ghorofa 10, lakini likajengwa hadi 16. Mtu mwingine ambaye anatafutwa na jeshi la polisi kukamatwa ni Mhandisi Mshauri.
Lukuvi alimwagiza Kova kuwa watu waliokuwa karibu na jengo jingine la ghorofa 15 lililojengwa na mkandarasi huyo, kuhama mara moja na ubomoaji ufanyike bila kuleta madhara.
Hoja yangu inasimama hapo kwenye RED jengo hilo ameamua libomolewe ni kwa sababu limejengwa na huyo mkandarasi au kuna sababu zingine za kitaalamu zilizoainishwa? nina mashaka na tamko hili kama limezingatia utendaji unaofuata sheria na taratibu.
Taarifa hii ipo kwenye Gazeti la Mwananchi la leo.