Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,395
- 13,266
Kwanza hakutakiwa kusema chochote kwasababu bosi wake hakutoa kauli yoyote pale unless awe alimtuma vinginevyo ni utovu wa nidhamu na ulevi wa madaraka. Hii ni tabia ya serikali dhaifu kila mtu anatenda ki vyake hakuna uwajibikaji wa pamoja. Ukifuatilia sakata hilo utasikia RC ana maagizo yake, Lukuvi naye kaja na yake, maelekezo ya Jk ni tofauti na haya ya Lukuvi na Kova naye atakuwa na yake, basi mradi tu kila mtu anataka kuonesha kuwa yuko. Ukienda kwa Sitta naye utakuta anaishutumu serikali ambayo naye yumo ndani yake kiasi kwamba unaweza kudhani yupo serikali nyingine.