Handling finances in marriage.... advice

Kama mlivyofanya we na nyamayao?

hapana kaka ikiwa utajulishwa tu ili upate sehemu ya mahari lol

haha Mrs wangu uyo! bado tunacheza hide-and-seek chumbani, bado kidogo tuje sebuleni sasa...heheheheh apo hutasikia tena mambo ya pesa sijui HG wala house boy...lol
 
Ahsante shishi kwa hii thread, maana tunaweza kujifunza vizuri mambo ya financial, haswa jinsi ya kushare mnapokuwa kwenye ndoa.
Mie niko mbioni kuja huko ndoani, ila huyu mwenzangu hataki nichangie kitu chochote, ananiambia yeye atabeba majukumu yote kama mwanaume. Mie hadi woga unanishika, maana kama kipato cha kuchangia ninacho, ila yeye anataka kufanya kila kitu. Je yupo sawa hivi kweli? Maana baadhi ya rafiki zangu wanasema eti ndio mwanaume mzuri, maana nitakuwa huru na pesa zangu. Lakini mimi najiona kama vile kuna walakini.

...naam, tena ogopa kweli kweli!

Hamna kitu hiyo eti atabeba 'msalaba' wote! Sikiza moyo wako, jiwekee akiba siku ya siku utayokuja-itwa 'golikipa!'
 
Dada Pretty,
huyo mumeo mtarajiwa anakuvutia pumzi kwanza uingie kwenye pingu ya kutenganishwa na kifo. Ukishaingia humo utachangia hadi pesa ya kusomesha wadogo zake. Wewe wanaume unatujua au unatuona externally tu, tunabadilika mpaka unashika kichwa unajiuliza vipi hivi huyu ndio yuleyule au ni mwingine au amelogwa.
Husiifurahie sana hali hiyo ukafikiri itaendelea milele, ndoa ni safari jamani

Nawasilisha
 
Ayaaaaaa Pretty kumbe ulikuwa bado unasubili ndoa dah mpwa Yo Yo anaweza akakuhifadhi kwa vigezo maalumu. Duh kwa hiyo wewe pesa yako unayo pata unafanyia nini? Jiwekee akiba shemeji hujui kesho kitatokea nini.
 
basi jameniiii nimeshindwa mie tangu ugongwe na nyoka shost umekuwa mkali hata ubua unaogopa? lakini hapo si bure nyamayao ndio anakufundisha uninja..... maaana nae mhhhhh

Hehehe mwache mammy apumnzike jamani pata wine kidogo kisha urudi.
 
basi jameniiii nimeshindwa mie tangu ugongwe na nyoka shost umekuwa mkali hata ubua unaogopa? lakini hapo si bure nyamayao ndio anakufundisha uninja..... maaana nae mhhhhh

....... Ah mamii nyamayao simuwezi maana duh ile namba chafu. Sie wengine useminary umetuharibu sijui kwa nini hatukuamua kuingia kwenye usista tu ikajulikana moja. lol
 
Dada Pretty,
huyo mumeo mtarajiwa anakuvutia pumzi kwanza uingie kwenye pingu ya kutenganishwa na kifo. Ukishaingia humo utachangia hadi pesa ya kusomesha wadogo zake. Wewe wanaume unatujua au unatuona externally tu, tunabadilika mpaka unashika kichwa unajiuliza vipi hivi huyu ndio yuleyule au ni mwingine au amelogwa.
Husiifurahie sana hali hiyo ukafikiri itaendelea milele, ndoa ni safari jamani

Nawasilisha

Hongera sana kwa kusema ukweli ndugu yangu.Siyo wengi wanaweza kusema ukweli huu.Kubadilika ni kawaida lakini, siyo lazima kwenye mambo ya faranga tu.Hata hivyo haitegemewi kabisa mke kujifanya hawezi kuchangia kitu.Kuna wanaume huwa na mkakati wa kupumbaza wake zao kwa "kuwaruhusu" kujifurahisha na vipato vyao kwa mambo madogomadogo yasiyokuwa na impact kwa maendeleo ya familia.Lengo lakini linakuwa siyo jema na nakumbuka hapahapa JF kuna mtu alileta mada ya kusema kuwa ili kumdhibiti mke,atamfanya atumie pesa yake kwa kununua nguo, na vitu vingine ambavyo siyo assests za kweli!

Naomba nitoe maangalizo yafuatayo kwa wanawake:
1.Mume siyo baba atabaki kuwa mume.

2.Unapokuwa kwa wazazi, ukifikia umri wa utu uzima na una kipato utawajibika kuchangia na siyo kusubiri uhudumiwe kama mtoto au mlemavu au kikongwe.Kwanini ukubali kuwa tegemezi kwa mumeo?

3.Binadamu anaishi kwa kupambana.Utapambanaje kwa kusubiri tu mwenzio ahangaike kutwa kucha - akutumikie wewe kama nani?

Haya ndiyo maswali mwanamke yeyote anapaswa kujiuliza kabla ya kukubali ofa ya mume mtarajiwa kuwa ASICHANGIE CHOCHOTE - ATAMTUNZA.
 
Kama unataka kuwa partner ni vizuri uchangie. Najua wanawake wengi mnapenda mitelemko. Mwanaume akikuambia yeye atatoa kila kitu wewe unashangilia kwa sababu unajua kile cha kwako utatumia vile unavyopenda mwenyewe. It is true.

Hata hivyo angalia mbele. Ikitokea la kutokea huko mbele e.g. kutengana atakuambia ulicontribute zero, so go with zero. Hata hivyo akishakuambia ana cover everything anakunyima nafasi ya kumfuatilia mambo yake. Utafuatilia nini wakati kila kitu anahudumia.

Catch nyingine, kuna siku anaweza kukuambia hataki ufanye kazi. Hes is paying everything so kwa nini usitulie? Mara nyingi wanawake mnashauriana sana kuhusu mambo haya. Wengi mnapenda huu utaratibu wa chako chako, cha mwanaume chenu.
 
Sifatilii mambo ya wf wangu. Anapata mshahara wake na marupurupu yake siulizi. But I expect her to clear some bills, ingawa simlazimishi. Zamani tulishirikiana sana, baadaye akapata ushauri kwa wanawake wenzie kuwa mume anatakiwa kulipa kila kitu. Nikakubali, ila alipoteza haki ya kujua mshahara wangu, na account yangu ina nini. Najua ana sneak hapa na pale kuona my payslips, lakini hawezi kuniuliza chochote kwani halazimiki kuchangia. Akilalamika, namlipa. Good with me. Good with her. Ana maintain her own finances namaintain za kwangu.

Nadhani as long as wote tunaendelea kupata income, business as usual. Tatizo najua litatokea kama income ya mmoja wetu itakapopungua au kutoweka. I can see kuwa unaweza kuwa mwisho wa ndoa..... money is sensitive
 
Nina swali hivi ni lazima ku-entertain swala la kusomesha ndugu na kutoa misaada ya hapa na pale ambayo asilimia kubwa inaishia kununulia vitu visivyo na umuhimu?
 
Am impressed by the numerous very enlightening responses, the experiences shared and all the insights.... kumbe hili ni swala tata mno! am surprised we had not discussed this and yet ndio chanzo cha migogoro mingi katika ndoa. thanks ya'll who took time to read and contribute. tuko pamoja! hapa natengeneza JF manual for handlng finances!! lol
 
Nina swali hivi ni lazima ku-entertain swala la kusomesha ndugu na kutoa misaada ya hapa na pale ambayo asilimia kubwa inaishia kununulia vitu visivyo na umuhimu?

Huu ni uamuzi binfasi kutegemeana na mhusika anavyojisikia.Hakuna sheria au mwongozo kwenye hili.
 
...naam, tena ogopa kweli kweli!

Hamna kitu hiyo eti atabeba 'msalaba' wote! Sikiza moyo wako, jiwekee akiba siku ya siku utayokuja-itwa 'golikipa!'
Akiba muhimu ndugu yangu, tena nimejidhatiti kweli kweli, akibadilika tu, na mie tayari nina pakusimamia. Wanasema akili kumkichwa!!!
 
mmm Nyamayao, hebu tupe hiyo rafu ili tuone kama ilikuwa rafu kweli au ni ilikuwa challenge ya kawaida kwenye mchezo, si unajua wewe unaweza kuona rafu kumbe sheria za mpira zikasema hiyo 'imo'.. ee hebu tumuvuzishie isije ikawa unamblast tu Mr.....;)

alicheza rafu na ina imenisaidia yeye kuwa kwenye mstari bila kokoro wala kakara, kajinasa mwenyewe.....
 
alicheza rafu na ina imenisaidia yeye kuwa kwenye mstari bila kokoro wala kakara, kajinasa mwenyewe.....

...... Kwa kweli na ni lazima awe anatamani siku zirudi nyuma ili a-undo. kama rafu yenyewe ni mbaya!

Ila ole wako akunase na wewe, utalipia dada yangu
 
....... Ah mamii nyamayao simuwezi maana duh ile namba chafu. Sie wengine useminary umetuharibu sijui kwa nini hatukuamua kuingia kwenye usista tu ikajulikana moja. lol

haya maisha ni mafupi mami kwanini ukwazike kupitiliza? haaa hapo kwenye u sist umeniacha hoi...lol
 
...... Kwa kweli na ni lazima awe anatamani siku zirudi nyuma ili a-undo. kama rafu yenyewe ni mbaya!

Ila ole wako akunase na wewe, utalipia dada yangu

mie ataninasa kwa lipi na wapi? yaani hana cha kufanya, c kwamba namkomoa lakini kama nilivyokueleza ni zamu yake mwanzo mpaka mwisho na mie naona imesaidia mana utulivu/amani vipo kwenye mstari kwasasa.
 
Back
Top Bottom