Handeni walimu wako bize na bodaboda na tigo-pesa

Handeni walimu wako bize na bodaboda na tigo-pesa

Sasa hivi iko timu inapitia kata zote za Handeni (Kwankonje, Kwachagga, kwalugulu, Kwamagome, Sindeni, kwabaya, mzundu, nk) kupata kanzidata ya walimu wote wasioonekana shuleni.
 
Unatetea upuuzi, acha kazi mkuu. Mtaji wa tigo-pesa na bodaboda wanaupata kwenye ualimu na ndiyo maana wanaonekana vijijini huko kama watu wenye hela kuliko wanavijiji. Lakini, darasa la wanafunzi zaidi 40 kupata wanafunzi wasiozidi 5 wenye ufaulu wa daraja B na waliobakia ni D, E na C chache kwenye mitihani ya darasa la saba, mfano ni kuonyesha kuwa walimu hawafanyi kazi yao. mwalimu lazima apate muda wa kujiandaa kufundisha, kuandaa somo, kufundisha, kupima uelewa wa mwanafunzi na kutoa mrejesho kwa wanafunzi. Kazi zote hizi haziwezekani kama mwalimu anafanya kazi ya bodaboda, tigo-pesa na kuonyesha video/tv mchana kutwa, hata usiku mwl anaamshwa kupeleka abiria sehemu.
Unauelewa mzuri
Ukitaka kujua kuna nafasi nyingi za walimu
Jiulize
Hivi unajua ktk darasa mwalimu 1 anatakiwa kufundisha wanafunzi wangapi?
Na wakizidi unajua anatakiwa alipwe vipi huyu unayemlaumu?, na unajua analipwaje?
 
uligundua lini kuwa kibong bong walimu wanadharaulika na kunynyasik? ulilazimishwa kusoma uwalimu? Mtu anayo hiari ya kuajiriwa au la, lakini akishaajiriwa hana hiari ya kufanyakazi. It is whether "ALL or NONE", not in between.
Ni kweli ila wana haki za kiutumishi ambazo nyingi zinakiukwa na ninyi wazazi mkifurahia. Jiandaeni kisaikolojia maana huwezi mshambulia mtu kwa bomu akakurudishia madorali
 
Nimejaribu kukusoma vizuri!
Ila hebu niambie mfano wa shahili zipi?
Maana Kwa mfano Ninachojua mishahara ya walimu miaka ya Siku hizi haichelewi au siyo?
Hapa hawazungumzii kuchelewa.
Utamu wa ngoma uingie uicheze.
Huwezi elewa
 
Hapa hawazungumzii kuchelewa.
Utamu wa ngoma uingie uicheze.
Huwezi elewa
Hebu niambie wewe ni kada ipi yenye elimu sawa na yako mwalimu inalipwa vizuri kuliko walimu?

Nijuavyo mimi watumishi wote wanachotewa chalula na mtu mmoja kutoka chungu kimoja hichohicho.nonsense!. Je, unataka madaktari, manesi, polisi, wanajeshi,nk nao waache kazi zao kama sehemu ya malalamiko ya maslahi madogo?. Walimu hawataki kusoma lakini wanataka malipo makubwa, tunafahamu kuwa wengi wao walikuwa division 4 na 3 za point mbaya zisizofaa kuendelea na masomo ya ngazi nyingine ya juu. Lakini sasa akishaajiliwa anafuata mkumbo (mob) ya kudai maslahi makubwa kwa elimu ndogo kabisa. Waliofika kule juu wengi wao walifanya hivyo kwa kuungaunga sana hadi tatare.

Heshima ya mtu hatokani na umri, cheo wala mshahara mkubwa anaopata bali huduma yake anayoitoa kwenye jamii inayomzunguuka. Kama mwalimu hufundishi kazi yako kulalamika nani atakuheshimu? kama mwl chule yako imekuwa ya mwisho ni nani atakuheshimu?
 
Sasa hivi iko timu inapitia kata zote za Handeni (Kwankonje, Kwachagga, kwalugulu, Kwamagome, Sindeni, kwabaya, mzundu, nk) kupata kanzidata ya walimu wote wasioonekana shuleni.

Afadhali aisee, wafike maeneo yote yakiwemo ya Msaje/kwaluwala, madebe, Kideleko, Msasa, magamba, Kwamkono n.k hamna jinsi!
Halafu hii inahusu pia Wilaya ya Kilindi!
Maeneo Kama vile Msente, Sangeni, Kwediboma , Mswaki n.k !
Kila ajue kutimiza wajibu wake stahiki!
 
wanakopa kwa dhamana ya uwalimu, wewe vepe? taasisi gani itamkopesha mtu asiyekuwa na uhakika wa kurejesha alichokopa? ni uwalimu tu unaomfanya aaminiwe. Aaache kazi basi aone nani atamkoposha
Kavulata hujanielewa hoja yangu
 
Hebu niambie wewe ni kada ipi yenye elimu sawa na yako mwalimu inalipwa vizuri kuliko walimu?

Nijuavyo mimi watumishi wote wanachotewa chalula na mtu mmoja kutoka chungu kimoja hichohicho.nonsense!. Je, unataka madaktari, manesi, polisi, wanajeshi,nk nao waache kazi zao kama sehemu ya malalamiko ya maslahi madogo?. Walimu hawataki kusoma lakini wanataka malipo makubwa, tunafahamu kuwa wengi wao walikuwa division 4 na 3 za point mbaya zisizofaa kuendelea na masomo ya ngazi nyingine ya juu. Lakini sasa akishaajiliwa anafuata mkumbo (mob) ya kudai maslahi makubwa kwa elimu ndogo kabisa. Waliofika kule juu wengi wao walifanya hivyo kwa kuungaunga sana hadi tatare.

Heshima ya mtu hatokani na umri, cheo wala mshahara mkubwa anaopata bali huduma yake anayoitoa kwenye jamii inayomzunguuka. Kama mwalimu hufundishi kazi yako kulalamika nani atakuheshimu? kama mwl chule yako imekuwa ya mwisho ni nani atakuheshimu?
Wewe una uelewa na madaraja ya utumishi?.
Mtumishi mwenye stashahada kada ya mahakama daraja lake na
Stashahada ya kada ya kilimo na
Stashahada ya elimu.
Unadhani wanalipwa sawa.
Nina shaka na upeo wako wa uelewa. Ndio maana umetanguliza matusi.
Lakini wewe ni mjinga tu ndiyo maana nimekufafanulia. Ungekuwa mpumbavu nisingekujibu
 
Walimu Handeni hawafundishi kabiiiisa, muda wao mwingi unamalizikia kwenye biashara ya bodaboda, tigo-pesa na kuonyesha TV/Video. Hii inasababisha taaluma Handeni kushuka sana.

Wakaguzi nendeni Handeni kimya kimya mkajionee walimu wanaokula pesa za bure bila kazi, biashara zote vijijini ni za walimu.
safi sana....... nimewakubali hao walimu
 
Kama mshahara hautoshi siuache Tu kazi au goma Kwa uwazi watu wote waelewe kuliko kugoma kimyakimya?
wagome ili iweje wakat wanaweza kufanya mambo yao?.........

nenda kawakamate kama una nguvu.......jinga kweli wewe!!!
 
nimesoma std1 hadi 7, f1 hadi f4, f5 hadi 6, plus chuo.........afu jitu linakuja na kusema nifanye kazi kwa mshahara mdogo?.....

naikubali kazi yako ila nakua mvivu kazin, shida iko wap?
 
Tanga, mtwara , lindi na zenji wazaz za wanafunzi hawanaga mpango na shule serikali inalazimisha tu,
 
Wewe una uelewa na madaraja ya utumishi?.
Mtumishi mwenye stashahada kada ya mahakama daraja lake na
Stashahada ya kada ya kilimo na
Stashahada ya elimu.
Unadhani wanalipwa sawa.
Nina shaka na upeo wako wa uelewa. Ndio maana umetanguliza matusi.
Lakini wewe ni mjinga tu ndiyo maana nimekufafanulia. Ungekuwa mpumbavu nisingekujibu
eti na wewe unajiita unajuwa!! ama kweli elimu imeshuka. haya bhana,
 
We naweee!! Nenda kafundishe wewe kama inakuuma.
 
Uloleta uzi kwanza ww inaonekana u have low thinking capacity ko unataka walale kwa darasa ama???ilihali mshahara mwisho wa mwez daraja E take home n lak nn sasa vp wa daraje D na wengine inshort mshahara haukidhi mahitaj na kaz inayofanywa n kubwa binafs kama n mm nmepangiwa kitua maduka kama yote yananihusu sku hz na wazaz wanajua kujiongea ko ambao hawajiongez shaur yao s elmu bure bhana
 
Walimu hawataki kusoma lakini wanataka malipo makubwa, tunafahamu kuwa wengi wao walikuwa division 4 na 3 za point mbaya zisizofaa kuendelea na masomo ya ngazi nyingine ya juu. Lakini sasa akishaajiliwa anafuata mkumbo (mob) ya kudai maslahi makubwa kwa elimu ndogo kabisa.
Acha uongo, waheshimu walimu wako waliokuwezesha ujue kusoma na kuandika.


Heshima ya mtu hatokani na umri, cheo wala mshahara mkubwa anaopata bali huduma yake anayoitoa kwenye jamii inayomzunguuka.
Kwani walimu hawatoi huduma kwa jamii? Mnaongea vitu rubbish.


Kama mwalimu hufundishi kazi yako kulalamika nani atakuheshimu?

Kwani wamekwambia hawafundishi?

kama mwl chule yako imekuwa ya mwisho ni nani atakuheshimu?
Sasa chule ndiyo nini?
 
Walimu Handeni hawafundishi kabiiiisa, muda wao mwingi unamalizikia kwenye biashara ya bodaboda, tigo-pesa na kuonyesha TV/Video. Hii inasababisha taaluma Handeni kushuka sana.

Wakaguzi nendeni Handeni kimya kimya mkajionee walimu wanaokula pesa za bure bila kazi, biashara zote vijijini ni za walimu.
Safi sana. maana mwajiri wao hawathamini kila siku porojo
 
Back
Top Bottom