Handeni: Ajali mbaya ya magari imetokea, wanne wafariki, mashuhuda wa ajali nao wapitiwa na Coaster

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Ajali mbaya imetokea Sindeni, Handeni mkoani Tanga usiku wa kuamkia leo, idadi ya vifo na majeruhi haijatajwa, usiku wa kuamkia lo Machi 16, 2022.

“Coaster ilivamia Hiace ilivyokuwa imeharibika pembeni na kuwasomba abiria wote. Ajali ni mbaya kwa kweli,” amesema Siriel Mchembe, Mkuu wa Wilaya ya Handeni.

handeni.jpg

Taarifa kamili itafuata

=====================================================================================

Watu wanne wafa, 37 wajeruhiwa ajali ya Handeni

Watu wanne wamefariki dunia na wengine 37 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari mawili wilayani Handeni mkoani Tanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga (RPC), Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo ilitokea usiku wa kuamkia leo Jumatano Machi 16, 2022 katika Kijiji cha Sindeni.

Kamanda Jongo amesema kuwa basi ndogo la abiria aina ya Coaster iligonga Toyota Hiace na watembea kwa miguu na kusababisha vifo vya watu wanne na majeruhi 37.

"Chanzo cha ajali hii ni gari aina ya Isuzu Jorney ikitokea Tanga mjini kwenda Handeni, iligonga watembea kwa miguu na gari ambayo iliharibika njiani ambapo watu watatu walifariki hapohapo na mmoja alifariki hospitali akiwa anapatiwa matibabu huku saba wakijeruhiwa sana na wengine wamepata michubuko " amesema

Mganga mkuu Hospitali ya mji Handeni, Dkt Hudi Shehdadi amesema kuwa walipokewa majeruhi 38 ambapo mmoja alifariki dunia akiwa bado anapatiwa matibabu.

Shuhuda wa ajali hiyo Mustapha Bakari amesema walisikia kishindo barabarani na baada ya kwenda eneo la ajali walikuta majeruhi mmoja, wakati wanaendelea kumuhudumia ghafla alisikia kishindo na kukuta wameshagongwa na gari nyingine.

Wengi wa majeruhi wa ajali hiyo ni wananchi wa kijiji cha Sindeni ambao walijitokeza kwaajili ya kushuhudia ajali ya kwanza,ambapo lilitokea basi lingine na kuwagonga wakiwa eneo la tukio.


Source: Mwananchi

Handeni 1.jpg


Handeni.jpg


Handeni2.jpg
 
Ajali mbaya imetokea Sindeni, Handeni mkoani Tanga usiku wa kuamkia leo, idadi ya vifo na majeruhi haijatajwa, usiku wa kuamkia lo Machi 16, 2022.

“Coaster ilivamia Hiace ilivyokuwa imeharibika pembeni na kuwasomba abiria wote. Ajali ni mbaya kwa kweli,” amesema Siriel Mchembe, Mkuu wa Wilaya ya Handeni.

Taarifa kamili itafuata

=====================================================================================

Ajali yaua Handeni​

Watu ambao idadi yao haijafahamika wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa katika ajali iliyotokea katika eneo la Sindeni wilayani Handeni mkoani Tanga.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni (DC), Siriel Mchembe amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akisema kuwa idadi kamili ya vifo na majeruhi bado haijafahamika.

Amesema kuwa ajali hiyo imetokea usiku wa kuamki leo Jumatano Machi 16, 2022.

Mchembe amesema kuwa ajali hiyo imehusisha basi ndogo la abiria aina ya Coaster na Toyota Hiace.

"Taarifa za awali zinaeleza kuwa Hiace ndio ilipasuka tairi na kupotea njia baada ya hapo wananchi walijitokeza kuangalia ajali, ikatokea Coaster ikiwagonga wananchi ambao walikuwa kwenye ajali” amesema na kuongeza:

‘Watu ni wengi hospitali wanapatiwa matibabu, kuhusu vifo idadi kamili tutasema tukimaliza uokoaji", amesema Mchembe.

Source: Mwananchi

View attachment 2152516

View attachment 2152517

View attachment 2152518
Mbona wanaonekana kama ni wachaga wakienda na kutoka Moshi.
Pole kwa wahusika na familia zao.
 
Pole kwa majeruhi woteee na woote walioguswa na ajali hii
 
tunapoacha matumizi ya akili na kuamua lupuga ramli basi tutakuwa kila siku tunaokota maiti..

Tufanye mambo kitalaam, tufanye mambo kwa data, tufanye mambo kwa kuyapima nk...

utolewaji kiholela wa hizi drivingi licence unaleta hizi shida..
Rushwa kwa Traffic na polisi madhara yake ni makubwa sana just kwa 10K.
Magari mabovu ya abiria kuruhusiwa kutembea barabarani..
Kuruhusu Masikini wa kipato kufanya biashara zinazohitaji mitaji mikubwa..
 
Niliwahi kutoa wazo kwamba dereva wa gari lolote la abiria, isipokuwa daladala, taxi, na bajaji umri uanzie miaka 50 na kuendelea.
Itungwe sheria kabisa. Hizi accident za ajabuajabu zitapungua sana!
 
yaani nimeona iyo 1HZ nimesisimka
ukikanyaga mafuta, inakubali
kule mbele kama kunanesa nesa ivi, inazidi kuita kmmmk

majeruhi wapone haraka,
waliofariki walale kwa amani
 
Watanzania tuache tabia ya kushangaa ajali,hata juzi kuna gari imemgonga boda boda ila hakuumia sana lakini watu walijazana barabarani kushangaa
 
Tatizo la sisi watanzania kushangaa ajali ni kubwa sana utakuta watu wamejaa barabaran Kama vile Magar mengine hawaruhusiwi kupita... Hpo mwenye Kosta kajaribu kuwakwepa kaingia mtaroni dah
 
Duh!

Ukishaona mtu kasonsomola hivyo, ujue alikuwa anakimbia kugongana uso kwa uso...
 
Back
Top Bottom