Handaki kubwa lagunduliwa kitanzini Iringa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Handaki kubwa lagunduliwa kitanzini Iringa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magesi, Oct 24, 2012.

 1. M

  Magesi JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Handaki kubwa limegunduliwa katika eneo la KITANZINI MKOANI IRINGA MUDA HUU WAKATI KAMPUNI YA UCHIMBAJ WA BARABARA YA JR IKIENDELEA NA UJENZ SOURCE ITV BREAKING NEWZ MUDA HUU
   
 2. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,474
  Likes Received: 5,858
  Trophy Points: 280
  Duh hivi yule KIYEYEU hajatulia tu huko kuzimu?
   
 3. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  picha tafadariiii
   
 4. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hebu funguka zaidi mkuu!
   
 5. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Weka Picha bwana sie wenyewe tumeona hyo breaknews hatujaanzisha uzi coz hatuna picha sasa na wewe unaanzisha bila kuleta picha its really boring......
   
 6. M

  Made aw kubofya Member

  #6
  Oct 24, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lina nini Hilo handaki
   
 7. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Mwaka huu tutasikia mengi.
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,367
  Likes Received: 22,228
  Trophy Points: 280
  Kaburi lake lilihamishwa kilainiiii, kama kumtongoza malaya
   
 9. n

  naroka Member

  #9
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  This is good news,its a great opportunity for tourism!!!
   
 10. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #10
  Oct 24, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,755
  Likes Received: 8,024
  Trophy Points: 280
  Sasa yeye picha azitoe wapi kama wewe na yeye wote mmesikia tu?

  Ni vyema ameanzisha uzi kwa kuwa JF ni funika mbaya, upo uwezekano kuna mtu ana taarifa ya uwepo wa kitu kama hicho akatupa details au hata hizo picha. Au wewe unaonaje?
   
 11. Mwitongo

  Mwitongo JF-Expert Member

  #11
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 30, 2009
  Messages: 311
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Au la Mkwawa wakati akiwakwepa wajerumani?
   
 12. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #12
  Oct 24, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,755
  Likes Received: 8,024
  Trophy Points: 280
  Halina kwa kweli. Nini huwa ipo kwenye machimbo tu
   
 13. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #13
  Oct 24, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  ha ha ha! yani aina ya majibu na maswali yako humu jamvini unaniachaga hoi..sikutarajia ungeuliza hilo swali
   
 14. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #14
  Oct 24, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Kaburi la Kiyeyeu lang’oka [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Thursday, 30 December 2010 21:17 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Tumain Msowoya, Iringa
  HATIMAYE kaburi la kihistoria la Martine Kiyeyeu lililokuwa katika eneo la Isimila, kijiji cha Ugwachanya limeondolewa katika hifadhi ya barabara ya Tanzania-Zambia, Mkoani Iringa kwa ajili ya kupisha upanuzi wa barabara hiyo.

  Kaburi hilo ambalo lilikuwa pembezoni mwa barabara hiyo, limeondolewa katika oparesheni iliyoendeshwa na Wakala wa barabara (Tanroads) kwa akiwashirikisha wananchi wa kijiji hicho.

  Kaburi la Kiyeyeu linalokadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 40 hadi 50, lina historia ndefu kutokana majaribio ya kuliondoa mara kadhaa kushindikana.

  Moja ya maajabu ya kaburi hilo ni kushindwa kupitishwa kwa umeme kupita juu ya yake na pia linadaiwa kushindikana kuondolewa mara mbili na kusababisha vifo vya watu wawili akiwemo aliyeuawa kwa nyuki na mwingine kufariki ghafla akiendesha tingatinga alipokuwa akijaribu kuling’oa.

  Lakini jana kaburi hilo na mengine 21 yaliyokuwa kwenye eneo hilo yaliondolewa na kuhamishiwa upande wa pili wa barabara, ambako kulikuwa na kaburi moja la mtoto wa kike wa Kiyeyeu, ambaye hakuzikwa katika eneo lililokuwa na makaburi ya ndugu zake.

  Wakizungumza na Mwananchi, baadhi ya watu walioshiriki katika zoezi la kuondoa kaburi hilo walisema kazi haikuwa ngumu kama walivyodhani.

  “Tumeondoa ‘kiulaini’, hakuna mila wala desturi iliyofanywa kabla ya kuliondoa, na ndugu wa Kiyeyeu wanasema watakuja kazi ikimalizika kwa ajili ya kumaliza mila zao,” alisema Gaitan Utenga.
  Alisema kazi hiyo imefanikiwa kutokana na ushirikiano walioupata kutoka Tanroads ambao waligharamia shughuli nzima ya kuondoa kaburi hilo ilyowashirikisha vijana zaidi ya 30.

  “Tumelipwa pesa yetu vizuri, wamenunua sanda na masanduku kwa ajili ya mazishi na hatimaye kaburi limeondolewa tofauti na imani iliyokuwa imezagaa miongoni mwa wengi kwamba ingeshindikana,” alisema.
  Mwenyekiti wa kamati ya kuondoa kaburi hilo ambaye ni mmoja wa wanafamilia wa Kiyeyeu, Pulo Kikoti alisema hakuna tatizo lililotokea wakati wa kuondoa kaburi hilo. Kazi hiyo alizanza jana saa nne asubuhi na kumalizika majira ya jioni.

  Alisema ugumu ulikuwa katika kulibomoa kutokana na aina ya ujenzi wake, lakini baada ya kubomolewa kazi ya kulihamishia upande wa pili wa barabara haikuwa ngumu.
  Hata hivyo walisema tayari makaburi yote 22 yaliyokuwa katika eneo hilo yameondolewa na kwamba kazi ya kuzika mafuvu ya marehemu ambao wote ni familia ya Kiyeyeu inatarajiwa kumalizika leo mchana.

  “Ndugu wanasema mwishoni baada ya mazishi kukamilika na makaburi mapya kujengwa, watakuja kufanya mila zao, lakini mpaka sasa tumemaliza shughuli nzima ya kuondoa kwa kaburi hilo ambalo lilikuwa gumzo kwa miaka mingi,” alisema.
  Mzee huyo alisema wengi waliamini kuwa eneo hilo lilikuwa la maajabu, kutokana na ukweli kwamba lilishawahi kujaribiwa kuondolewa zaidi ya mara mbili na ikashindikana.

  “Kulikuwa na imani nyingi hapa, lakini tulijitosa kuhamisha na kweli hakuna kilichotokea hapa, naweza kusema imani hizi hazikuwa za kweli, mbona tumefanikiwa?” alihoji Kikoti.

  Kuondolewa kwa kaburi la Kiyeyeu kumekuwa gumzo kwa watu wengi wakiwemo abiria wanaopita katika barabara hiyo ambapo kila mmoja amekuwa akishangaa jinsi kazi hiyo ilivyofanyika.

  Awali mkazi wa Mafinga, Sadick Mhomanzi alijitokeza akidai kuwa anaweza kuliondoa kaburi hilo la Kiyeyeu na kwamba hakuna madhara yoyote ambayo yangeweza kumpata.

  Hata hivyo mapema jana, Mhandisi aliyeshiriki operesheni ya kupitisha umeme kwenye kaburi hilo mwaka 2006, Eliasante Mwakalinga, alionya kuwa Sadick asithubutu kwani angeweza kupatwa na balaa.

  Akizungumza na gazeti hili kutoka mkoani Mtwara jana, Mwakalinga ambaye sasa ni mwalimu wa Chuo Cha Mafunzo Stadi Veta mkoani Mtwara, alisema maajabu yanayofanyika kwenye kaburi hilo, yanatisha na yanaweza kuwa hatari kwake.

  "Mimi sijui atatumia mbinu gani lakini lazima iwe ushirikina au nguvu za kiroho. Hata hivyo ni vema akatafakari kwa kina uamuzi huo kwani unaweza kumgharimu na akaongeza historia ya kaburi hilo kwamba sasa, wamekufa watu watatu badala ya wawili," alisema Mwakalinga.

  Alisema wakati wanatengeneza laini ya umeme eneo la kaburi hilo mwaka 2006, umeme uligoma kupita juu yake na wakalazimika kuhamisha njia ndipo walipofanikiwa.

  Mwakalinga alipendekeza serikali kulifanyia uchunguzi kaburi hilo na ikiwezekana litangazwe kivutio cha watalii kwani kuna mambo mengi ya ajabu mbali na watu wawili kufariki dunia walipokuwa wanajaribu kuliondoa.

  "Ukiwa huku Iringa utapata maelezo mengi kuhusu wazee wetu hawa, wengine walikuwa wanazikwa na vitu vyao, wengine walizikwa wakiwa wamekalishwa chini na hata baadhi yao walikuwa wanazikwa kwa kupakatwa na vijana wenye nguvu. Hayo yote ni historia yetu ambayo ni vyema tukaienzi,"alisema

  Siku moja baada ya gazeti hili kuripoti maajabu ya kaburi hilo mkazi wa Mafinga, Sadick lijitokeza na kusema anaweza kuliondoa bila wasiwasi wala madhara yeyote tofauti na maelezo ya watu kwamba watu kadhaa wameshapoteza maisha kwa kujaribu kufanya hivyo.

  Mhomanzi alitoa kauli hiyo wakati ambapo taarifa za uhakika kutoka katika eneo la kijiji hicho zikidai juhudi za kuliondoa kaburi hilo ili kupitisha barabara eneo hilo zimekuwa zikishindikana hata pale ilipotumika familia ya Marehemu Martin Kiyeyeu mwenyewe.

  Lakini Mhomanzi kwa kujiamini alisema atakwenda yeye mwenyewe na kutumia jembe lake la mikono kuchimba na kuondoa udongo huo hadi mifupa ya marehemu Kiyeyeu na kuihamisha bila ya kudhurika.

  "Amini maneno yangu kuona kaburi linashindikana kuondolewa, hakuna mtu anayeweza kushindwa, kaka mimi niko tayari nitafanya kazi hiyo kwa mkono wangu kabisa,"alisema Mhomanzi.

  Mhomanzi alihoji "Kama ndugu wa marehemu wameridhia kuondolewa kwa kaburi hilo na kupatiwa eneo mbadala ni kitu gani kinaweza kuzuia? mimi siamini hivyo,Tanrods waniwezeshe mimi kuifanya kazi hiyo, nitakwenda na jembe langu pamoja na koleo kuifanya kazi hiyo nitakachokosa ni trekta la kubebea udongo na mifupa"alisema .
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 15. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #15
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,978
  Likes Received: 6,621
  Trophy Points: 280
  handaki kubwa kiasi gani? mbona hata hapa dar maeneo ya gerzani pale majani ya chai kuna handaki kubwa linalo pita chini ya nyumba za watu hatusemi? tupe kwanza ukubwa wake kama ulivyo liona kwenye tv. mia
   
 16. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #16
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,474
  Likes Received: 5,858
  Trophy Points: 280
  Hili hapa

  [​IMG]

  Handaki la ajabu limeonekana katika eneo la kata ya kitanzini mtaa wa sokoni
  Katika tukio hilo lililokuwa gumzo kubwa katika eneo hilo huku kila mmoja akisema lake
  Mtandao huu ulipokutana na mmiliki wa nyumba hiyo hakuweza kuwa na majibu yakuridhisha huku akisema yeye hafahamu shimo hilo limetokea wapi.


  Handaki hilo ambalo lilionekana jana na wachimbaji wa mitaro wa JR wanaoshuhulika na uwekwaji wa mabomba mapya ya maji safi wanaeleza katika kuchimba ndipo walipokutana na chemba hiyo ikiwa imefunikwa na kudhani kuwa inatumika kama shimo la choo ya nje lakini haikuwa hivyo maana lilikuwa wazi limejengewa na hakuna dalili ya kutumika kama choo.


  Akizungumza mmoja wa wananchi aliyeingia katika handaki hilo Abdukareem ameeleza kuwa yeye ni mkazi wa eneo hilo na alipopata taarifa alifika akiwa na mwenzake aliyefahamika kwa jina la Salehe na kukubaliana kuingia ndani ili kufahamu kilichopo.


  Ameeleza kutokana na shimo hilo kuwa refu walitafuta ngazi lakini hawakufanikiwa kwani ngazi hiyo ilikuwa pana na kuamua kutafuta fimbo kubwa ya muanzi na kamba na ndipo walipofanikiwa kuingia ndani.


  Anazidi kueleza kuwa walipofika ndani walikuta chumba ambacho ni kama futi tatu na kuona vidirisha vidogo kwa mbele huku bado kukiwa kumejengewa kwa zege na kubainisha kuna muendelezo wa chemba nyingine ambapo hawakuweza kuendelea kutokana na kuzibwa.


  mkuu wa Wilaya afika eneo la tukio


  Mkuu wa wilaya ya Iringa Dkt Leticia Warioba akafika katika eneo la tukio huku akiwa na wa wafanyakazi wa Kampuni ya JR pamoja na afisa wa usalama ambao waliishia kuangalia njia hiyo pasipo kuingia ndani ya handaki hilo.


  nini maoni ya wakazi waliofika katika eneo hilo?


  Wengi wa wakazi waliofika katika eneo hilo hawakusita kueleza hisia zao huku wengine wakieleza labda ni mahandaki yaliyokuwa yakitumiwa na Wajerumani enzi za ukoloni, huku wengine wakieleza labda handaki hilo limekuwa likitumiwa na majambazi kama sehemu za kujificha na kuhifadhia mali walizoiba japo hapakuonekana na mali aina yeyote.
   
 17. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #17
  Oct 24, 2012
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Utasikia Chadema hao.

  Afu huo mkuu wa wilaya hana kazi za maana ofisini?
   
 18. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #18
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,474
  Likes Received: 5,858
  Trophy Points: 280
  Toka lini wakawa na kazi?

  [​IMG]

  HATA POLISI HWANA KAZI PIA

  [​IMG]
   
 19. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #19
  Oct 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,753
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  kivutio kingine hicho_changamkien deal
   
 20. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #20
  Oct 24, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,813
  Likes Received: 36,858
  Trophy Points: 280
  Kipato kinachopatikana kwenye tourism kinaishia kwenye matumbo ya wapuuzi flani.


  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
Loading...