Hamieni Pwani

AK-47

JF-Expert Member
Nov 12, 2009
1,373
199
Waziri George Mkuchika amewataka wafanyakazi wote wa serikali wanaofanyakazi katika Mkoa wa Pwani na kuishi Dar es Salaam wahamie Pwani ifikapo Aprili mosi mwaka huu ili kupunguza gharama za kiutendaji pamoja na kuwahi mapema kazini.

Mkuchika amesema kitendo cha kuishi Dar na kufanyakazi Pwani huchangia kushusha ufanisi na utendaji wa wafanyakazi hao kutokana na kuamka usiku sana ili kuwahi kazini. Amesema ingawa Aprili mosi ni siku ya wajinga duniani lakini agizo lake walichukulie kwa umakini kwani halina uhusiano wowote na siku hiyo.

Source: The Guardian.
 
Kwanza mtumishi wa serikali kwenda nje ya mkoa unao fanyia kazi ni lazima uwe na kibali, je hao wafanyakazi nani anawapa hicho kibali kilasiku? Kama hawana vibali hivyo haina mjadala wachukuliwe hatua za kisheria. Mafuta ya magari kilasiku mamia ya kilometa juu ya walipa kodi bila huruma! Khaaaa!
 
Back
Top Bottom