Pwani: Maafisa Uhamiaji wakamata Raia wa kigeni wenye mitambo ya kuchapisha noti

FbUser

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
431
626
Maofisa Uhamiaji mkoa wa Pwani wamewakamata raia wawili wa Afrika Magharibi wakiwa na karatasi za kuchapisha pesa bandia, kemikali na kasiki (safe) la kutunzia fedha.

Watu hao wamekutwa pia na hati za kusafiria 34 za nchi za Nigeria na Ghana. Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa huo, Abubakar Kunenge, amewataja watu hao waliokamatwa eneo la Mapinga, Bagamoyo, kuwa ni Livingstone Ese Onayomake (raia wa Nigeria) na Bertrand Noubissie (raia wa Cameroon).

Kunenge amesema kuwa walipokea taarifa za kiintelijensia kuhusu watu wanaotiliwa mashaka na siku iliyofuata ulifanyika upekuzi na kuwakamata raia hao.

Amesema wakati wa upekuzi mtuhumiwa Onayomake alikutwa na paspoti 34 ambazo si zake, kati yake 32 ni za Nigeria na mbili za Ghana.

Kunenge alisema alipohojiwa, mnaijeria huyo alidai alichukua paspoti hizo kwa lengo la kuwatafutia wahusika viza ya Uturuki.

"Jambo la kusikitisha raia hao walikutwa wakihifadhiwa na mtanzania, na mbaya zaidi mmoja alishaanza kujihusisha na utengenezaji wa fedha bandia maana alikutwa karatasi zilizoandaliwa kwa ajili ya kuchapisha noti bandia, kemikali pamoja na kasiki (safe) la kutunzia fedha," alisema Kunenge.

Afisa uhamiaji Mkoani Pwani, Omary Hassan amesema baada ya kupata taarifa walienda kufanya upekuzi maungoni na kwenye makazi waliokua wakiishi.

Hassan ameeleza wahamiaji hao walikua wakiishi nyumbani kwa New Era Nyirembe ambaye alikua mke wa mtuhumiwa Noubissie, kwa sasa marehemu.

Amesema wamebaini kufuatia uchunguzi wa awali kuwa Onayomake aliingia nchini Februari 11 mwaka 2020 kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na kupewa viza ya matembezi ya siku 90 hadi Mei 05 mwaka 2020 lakini baada ya hapo ameendelea kuishi nchini kinyume na sheria hadi alipokamatwa

"Kuhusu Noubissie raia wa Cameroon yeye amekutwa na paspoti yenye namba 0441270 iliyotolewa Cameroon April 12, 2016 na iliisha muda Aprili 12 2021 na aliingia nchini mara ya mwisho Novemba 2, 2019 kupitia uwanja huo huo na alipewa viza ya matembezi iliyoisha Februari 01, 2020," amesema Hassan

Kufuatia tukio hilo, Kunenge ametoa rai kwa wananchi mkoani Pwani kutoa taarifa kwa mamlaka husika pindi waonapo watu wanaowatilia mashaka.

Pia amewataka raia wa kigeni kuhakikisha uwepo wao nchini unazingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi
 
Fanya biashara yoyote na mtu yeyote ila sio mnigeria.

Ni waongo, wanafiki na wezi
 
Ina bidi wawe wana fatilia taarifa za visa,

Wale wote walio pewa visa za muda mrefu Au mfupi basi data base zao zioneshe wame ondoka nchini na kwa njia waliyo ondokea kama mipaka ya ardhini Au meli/majini Au anha/viwanja vya ndege

Ili waweze kufahamu kama raia wa kigeni alipewa visa kuingia ya Muda fulani na mpaka visa ina isha hakuna taarifa za Uhamiaji toka mpka wowote ule kuwa ameondoka nchini wala kuongeza muda wa kukaa nchini

Basi ni vyema taarifa zao ziweze kutolewa na mamlaka husika ili jamii iweze kuwa tambua kama watu wanao tafutwa ili tuweze kuwa report

Ukiangalia wageni wapo wengi sana wana dhurura tu na wengine wana vioksi na wengine wana kuwa mawakala wa uhalifu, hivyo waweke utaratibu mzuri tu ili jamii tuweze kutoa taarifa

Wawekwe ata katika website yao ya Uhamiaji kuwa huyu ni mualifu kwa kuongeza muda wa kukaa nchini kinyume na sheria

Yumeona yule mboswana aliye kamatwa katikati ya jiji

Tuna endelea kuwa ona hawa wanigeria na wengine kibao

Lakini kumbe yawezekana wapo wengi sana
 
Maofisa Uhamiaji mkoa wa Pwani wamewakamata raia wawili wa Afrika Magharibi wakiwa na karatasi za kuchapisha pesa bandia, kemikali na kasiki (safe) la kutunzia fedha.

Watu hao wamekutwa pia na hati za kusafiria 34 za nchi za Nigeria na Ghana. Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa huo, Abubakar Kunenge, amewataja watu hao waliokamatwa eneo la Mapinga, Bagamoyo, kuwa ni Livingstone Ese Onayomake (raia wa Nigeria) na Bertrand Noubissie (raia wa Cameroon).

Kunenge amesema kuwa walipokea taarifa za kiintelijensia kuhusu watu wanaotiliwa mashaka na siku iliyofuata ulifanyika upekuzi na kuwakamata raia hao.

Amesema wakati wa upekuzi mtuhumiwa Onayomake alikutwa na paspoti 34 ambazo si zake, kati yake 32 ni za Nigeria na mbili za Ghana.

Kunenge alisema alipohojiwa, mnaijeria huyo alidai alichukua paspoti hizo kwa lengo la kuwatafutia wahusika viza ya Uturuki.

"Jambo la kusikitisha raia hao walikutwa wakihifadhiwa na mtanzania, na mbaya zaidi mmoja alishaanza kujihusisha na utengenezaji wa fedha bandia maana alikutwa karatasi zilizoandaliwa kwa ajili ya kuchapisha noti bandia, kemikali pamoja na kasiki (safe) la kutunzia fedha," alisema Kunenge.

Afisa uhamiaji Mkoani Pwani, Omary Hassan amesema baada ya kupata taarifa walienda kufanya upekuzi maungoni na kwenye makazi waliokua wakiishi.

Hassan ameeleza wahamiaji hao walikua wakiishi nyumbani kwa New Era Nyirembe ambaye alikua mke wa mtuhumiwa Noubissie, kwa sasa marehemu.

Amesema wamebaini kufuatia uchunguzi wa awali kuwa Onayomake aliingia nchini Februari 11 mwaka 2020 kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na kupewa viza ya matembezi ya siku 90 hadi Mei 05 mwaka 2020 lakini baada ya hapo ameendelea kuishi nchini kinyume na sheria hadi alipokamatwa

"Kuhusu Noubissie raia wa Cameroon yeye amekutwa na paspoti yenye namba 0441270 iliyotolewa Cameroon April 12, 2016 na iliisha muda Aprili 12 2021 na aliingia nchini mara ya mwisho Novemba 2, 2019 kupitia uwanja huo huo na alipewa viza ya matembezi iliyoisha Februari 01, 2020," amesema Hassan

Kufuatia tukio hilo, Kunenge ametoa rai kwa wananchi mkoani Pwani kutoa taarifa kwa mamlaka husika pindi waonapo watu wanaowatilia mashaka.

Pia amewataka raia wa kigeni kuhakikisha uwepo wao nchini unazingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi
Daaah, hivi waNigeria utapeli wanafundishwaga na nani?
 
Back
Top Bottom