Hamadi Rashidi bado hajaridhika anendeleza mapambano na CDM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hamadi Rashidi bado hajaridhika anendeleza mapambano na CDM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Dec 4, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  MKAKATI wa kukiengua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kushika nafasi za uongozi katika kamati za bunge unaandaliwa, imefahamika.

  Inadaiwa kuwa baadhi ya wabunge wachache wa CUF kwa pamoja na wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamewakamia wenzao wa CHADEMA kuhakikisha hawapati nafasi hizo.
  Mpango huo pia unadaiwa kutekelezwa nyuma ya pazia na vyama tajwa, kilieleza chanzo chetu.

  Vyanzo vyetu vya habari toka katika ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam, ndani ya Chama cha CUF na CCM, vililiambia gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa majina yao kuwa sababu ya mkakati huo kwanza ni hofu ya nguvu waliyonayo hivi sasa CHADEMA katika idadi ya wabunge.

  Sababu nyingine ni mgogoro wa kiuongozi ndani ya kambi ya upinzani baina ya CUF na CHADEMA.

  Kambi hii katika Bunge lililopita ilikuwa ikiongozwa na Hamad Rashid ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Wawi kupitia chama cha CUF.

  Inadaiwa kuwa CUF haijafurahia kambi hiyo kuongozwa na CHADEMA na hilo ndilo lililosababisha waungane na wenzao wa CCM katika kuwashughulikia wabunge wa CHADEMA kuhakikisha hawapati nafasi ya kuongoza kamati za Bunge pindi watakapowasilisha majina yao.

  Sababu nyingine inadaiwa ni kutaka kuwakata makali CHADEMA ambao wabunge wake wawili Dk. Willbrod Slaa na Zitto Kabwe katika Bunge lililopita waliokuwa ni miongoni mwa viongozi wa kamati na inadaiwa kushika kwao nafasi hizo kulisaidia kuongeza umaarufu wao na wa chama.

  "Wakati wakiwa viongozi wa kamati katika Bunge lililopita watu kama kina Dk. Slaa hawakuacha kutaja mabaya waliyoshuhudia katika kutekeleza majukumu yao.

  "Mara ya kwanza wakati walipopewa uongozi walifikiri kuwa wasingefurukuta tena, wangekuwa bize na majukumu ya kamati na kutatua mambo yanayoisibu lakini hali ilikuwa ni tofauti walitumia yale mabaya waliyoshuhudia yakifanywa na watendaji wa serikali kuwaeleza wananchi," kilieleza chanzo chetu.

  Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, Tanzania Daima imebaini kuwa mkakati huu wa sasa umeanza kufanywa chini kwa chini mara baada ya kuapishwa wabunge na kuundwa kwa kambi ya upinzani ambayo kwa sasa inaongozwa na Freeman Mbowe wa CHADEMA.

  Chanzo chetu kililidokeza gazeti hili kuwa wanaoshinikiza mkakati huo ni baadhi ya wabunge ambao wana uchu wa kimaslahi na madaraka.

  Hivi sasa wabunge wako katika utaratibu wa kuorodhesha maombi ya kamati wanazozitaka.

  Baada ya hatua hiyo, hatua inayofuata ni kupanga kamati na hili litafanyika wiki mbili kabla ya Bunge kuanza Februari 8 mwakani ambapo Spika Anne Makinda ataweka majina ya kamati mbalimbali kulingana na elimu na uzoefu na mwisho wa siku hizo kamati zitachagua wenyeviti.

  Alipotafutwa kuzungumzia suala hili, Katibu wa Bunge Dk. Thomas Kashililah hakuwa na nafasi kwani alipotafutwa kwa njia ya simu alimtaka mwandishi wa habari afike ofisini kwake.

  Lakini mwandishi alipofika ofisini kwake jana alielezwa na katibu muhtasi wake kuwa alikuwa ametoka kidogo kwa dharura za kiofisi.
   
 2. The Spit

  The Spit JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Your nightmare!
   
 3. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 3,589
  Likes Received: 2,972
  Trophy Points: 280
  Mwanamapinduzi hahitaji kuwa M/kiti wa kamati ndipo aibue mambo. Kama walivyofikiria hapo mwanzo kuwa kwa kuwaweka wabunge wa CHADEMA kwenye kamati fulani kungewaziba midomo, pia safari hii kwa kuwapa au kuwanyima Uongozi katika kamati hakutawazuia kusema. Wabunge wengine wote ni wa vyama lakini wabunge wa CHADEMA ni wa umma. Wasiposikilizwa ndani ya bunge na serikali, watasikilizwa na umma.
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,320
  Trophy Points: 280
  Hoja hii haina mashiko kwa sababu kwa mujibu wa kanuni, kamati za PAC, LAAC na POC ndizo huongozwa na kambi rasmi ya upinzani ambayo ni Chadema.
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Dec 4, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 417,238
  Trophy Points: 280
  We wish CCM and CUF a Merry X-Mas and a happy New year...............
   
 6. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #6
  Dec 4, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hebu tuyaache madaraka kwa waroho ili kuturahisishia kazi.
  Sisi tujikite kutatua matatizo ya msingi yanayowasibu wananchi kila siku ili kupunguza machungu ya maisha.
  Anybody can borrow me a tomorrow's bread???
   
 7. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #7
  Dec 4, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Its too late for CUF and CCM kuanza kufanya fitina kama hizo, wakati mifano tunaiweka kwenye halmashauri tutakazoziongoza.
  Wakiamua kutuiga ndo furaha yetu watanzania wote kwani watakuwa wamepata unafuu wa maisha. Kazi imeshaanza na kwa kuanza na jiji la Mwanza, wataona nini tulikuwa tunamaanisha kwenye kampeni.
   
 8. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #8
  Dec 4, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwambieni Hamad kuwa Mdaharo uliisha, na Freeman Mbowe akiibuka mshindi kwa mbali!! Kama anataka kukata rufaa anaruhusiwa lakini namhakikishia kuwa hata ukifanyikia Zanzaibar na kurushwa na TVZ kwa kusimamiwa na Maalim Seif ataendelea kushindwa kwa kuwa chama chake hakina rekodi nzuri machoni mwa Watanzania.
   
 9. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #9
  Dec 4, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hii kali kweli,tutafika lakini
   
 10. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #10
  Dec 4, 2010
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Mkuu Pasco, Kirefu tafadhali maana nimeachwa kombo hapo
   
 11. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #11
  Dec 4, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Nani anatunga kanuni?
   
 12. C

  Calipso JF-Expert Member

  #12
  Dec 4, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Source: chanzo chetu. duh pole sana halafu inaonekana hata kanuni za bunge huzijui,ukitaka kupanga uongo atleast kwanza ungejifunza zile kanuni za bunge ili uongo wako uelekee kidogo. PASCO UPO? hebu mfundishe kanuni bwana mdogo.asiongee pumba hapa
   
 13. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #13
  Dec 4, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Tanzania Parliament possesses an organised system of committees which comprises standing committees and Select Committees.

  1. Finance and Economic Affairs
  2. Public Accounts
  3. Social Services
  4. Social Welfare & Community Development
  5. Constitutional, Legal and Public Administration
  6. Standing Orders
  7. Parliamentary Privileges, Ethics and Powers
  8. Energy and Minerals
  9. HIV/AIDS Affairs
  10. Infrastructure
  11. Public Corporation Accounts
  12. Miscellaneous Amendments
  13. Land, Natural Resources and Environment
  14. Agriculture, Livestock and Water
  15. Foreign Affairs, Defence and Security
  16. Industries and Trade
  17. Local Government Accounts
  Nadhan hii itasaidia wakuu
   
 14. n

  ngoko JF-Expert Member

  #14
  Dec 4, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Inamaana wengine kazi yao ni kuficha maovu yanayofanywa ? kama ni hivyo safari tuliyonayo haina mwelekeo
   
 15. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #15
  Dec 4, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Ulichokisahau kingine ni mgogoro wa chini kwa chini ndani ya CHADEMA! siku si nyingi utasikia madiwani wa CDM wamefukuzwa au kujiuzulu... hapo sijawasema wabunge. Okaaay wacha tusubiri!
   
 16. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #16
  Dec 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Sidhani kama Hamad atafanikiwa katika ilo
   
 17. F

  Froida JF-Expert Member

  #17
  Dec 4, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Unalala na kupumua harufu ya CDM ni dalili nzuri kwa chama hiki kwamba watu kama wewe unainterests nacho kwa kukitabiliaa mazuri na mabaya yote tisa ,kwa kiasi cha kwamba toka ulivyojiunga sat octber 2010 hujawahi kupost kwenye thread nyingine yeyote zaidi ya post zinazohusu CDM wewe na rafiki zako munazoanzisha kulaani CDM,ni nzuri kwani hii inaonyesha jinsi gani CDM ni tishio kwamba kuna genge hapa JF kazi yao ni kuinaga CDM a baadhi ya viongozi wao ,wewe unachokijua maishani mwaka ni issues za CDM tuu ,lazima utakuwa unapata mshiko mzuri sana
   
 18. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #18
  Dec 4, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  tena kweli maana cuf kina rekodi nzuri pemba tu, nako misikitini huku bara kina harufu mbaya
  maana kinatumiwa kama laptop na ccm kuwakandamiza wananchi wanyonge
   
 19. E

  Ebony Guest

  #19
  Dec 4, 2010
  Joined:
  Messages: 0
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ningeshauri hao KAFU warudi kwao Unguuja na watuachie CDM yetu huku kwetu...maana hawana msaada wowote zaidi ya kuharibu tu!
   
 20. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #20
  Dec 4, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  you'll never get asleep because of this real man, Mbowe.
   
Loading...