KERO Halmashauri zetu kugawa namba za Watumishi kwa Micro-finances sio sawa

KERO Halmashauri zetu kugawa namba za Watumishi kwa Micro-finances sio sawa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kumekuwepo na tabia ya watu kutoka taasisi za mikopo na baadhi ya benki (ambazo mtumishi sio mteja) kumtafuta mtumishi wa uma na kumuelezea masuala ya mikopo.

Maswali ya kujiuliza ni:

Je, taarifa za watumishi hawa haswa mawasiliano yao zipo salama?

Lakini kama hawa watu wanaweza kujua hadi mtumishi anapofanyia kazi, je ni chanzo kipi kinakosababisha taarifa hizi kujulikana?

Lakini pia kuna faida gani kwa wanaotoa taarifa hizo isije ikawa wapo watu wanaonufaika na kusambazwa kwa taarifa hizi?

Ni hivi:
Mimi ni mtumishi katika halmashauri mojawapo. Ni mwajiriwa mpya kabisa.

Ghafla tu nilianza kupokea meseji kutoka kwa micro-finance wakinitaka kukopa.

Imefikia muda hizi meseji sasa ninapokea kila siku! Kila iitwayo leo! Na zinakuja kwa namba tofauti kila siku.

Inakera sana…

Huu ni kutoheshimu faragha ya mtumishi.

IMG_1263.jpeg
IMG_1262.jpeg
IMG_1261.jpeg
IMG_1259.jpeg
IMG_1260.jpeg
 
Mtumishi hautaki kukopa kwenye mifumo rasmi?
unataka kukopa kwa washikaji halafu muanze kuzungushana kwenye kulipana.
 
Asilimia 3.5 kwa mwezi ni sawa na asilimia 42 kwa mwaka. Ni ngumu hao platinum kupata wateja ukizingatia siku hizi microfinance zinatoa riba mpaka asilimia 19 na wapo kwenye mfumo wa ESS
 
Asilimia 3.5 kwa mwezi ni sawa na asilimia 42 kwa mwaka. Ni ngumu hao platinum kupata wateja ukizingatia siku hizi microfinance zinatoa riba mpaka asilimia 19 na wapo kwenye mfumo wa ESS
Kuna watu hawajui hesabu vzr wataingia kwenye mtego
 
Back
Top Bottom