Halima Mdee: Bold and Beautiful!

Nani amekuambia kuvuta bangi ni jambo la kishetani? unamjua huyo shetani?:mad2:



MH !Namuona mwanachama wa jani huyo.Karibu kwetu mama, kwetu hata huulizwi wewe tu na roho yako kula kitu roho inapenda.Na kama huna lighter unamfuata polisi anakuwashia unaenda zako.
 
katika wapinzani wenye akili,, huyu pia namkubali, yaani kama nilivyokuwa namkubali Slaa alipokuwa Mbunge.
 
mimi ni mkazi wa kawe kura yangu na ya mke wangu amepata....anadeserve kwa kweli.....
ila kibarua kikubwa ni kummwaga mzee wa NCCR...naona amezindua matawi jimboni kawe na sio sehemu zingine kumbe alikuwa ana malengo binafsi sio ya kichama zaidi.....
 
ACHENI MAMBO YA SIASA NA DEBE,ningependa kujua ameolewa?
Na je kama ameolewa anaishi vipi na mumewe?Je anafamilia?
Baada ya hapo tujadili sasa uwezo wake kiuongozi
 
Hivi wale polisi wanaovuta jani na wanajeshi wetu nani awakamate?
 
Hawa ndio vijana wa CHADEMA wanaodumisha chachu ya mabadiliko.
Dada mpendwa, hata sie tulioko vijijini tunakupata vizuri.

Ushauri wangu, Wewe, Zitto Kabwe na John Mnyika, tafuteni muda wa kuzunguka pamoja wakati huu wa kampeni ili kuhamasisha vijana ambao bado wamelala waamke.


Kama mtahitaji msaada wa kihali na kimali, tuko tayari kusaidia.

Kwa sababu ukweli tumechoooooooooooka na CCM na tunahitaji mabadiliko

Keep up the HARDWORK
 
Huyu dada kushinda pale ni ndoto, najua wengi mtakasirika nikisema hivi ila ukweli ndio huo. Walipotaka kugawana kura na Mbatia hapo ndipo kosa limefanyika. Atachukua kidogo, Mbatia kidogo, na yule mrembo wa chama tawala atapata zaidi. Tukutane Oktoba nitawathibitishieni hili. Ila namkubali.
 

Mkuu umenena wazi na kweli kabisa. Wapinzani hapa ndipo wanapoudhi wapiga kura. Kwanza kila mpinzani ni lazima atizame maeneo ambayo comperative advantage kwa chama chake ipo. Kwa mantiki hii kama chama pinzani kina political comperative advantage jimbo fulani basi wakiachie ili kipambane na mmbadala wake ambao kwa sasa ni CCM. Kwa kawe ninaona Halima anafaa kuliko Mbatia hivyo Mbatia angemwacha Halima apambane na huyo msanii wa CCM na lazima angedondoka tu. Hata hivyo, bado mapema na Mbatia anaweza shauriwa ajitoe kwa sasa na kutangaza wafuasi wake wampe Halima. Kiukweli kama watabaki vijana hawa jua kabisa jimbo litachukuliwa na CCM. Upinzani ukitaka kufanikiwa ni lazima wakubali kufanya maamuzi magumu. Hii pia hata kwa wagombea urais sikuona mantiki ya kutoamua kumwachia yule ambaye tayari watu wana Imani naye na badala yake mnaweka wagombea ambao hata hawajawahi kusikika katika redio mbao na wengine ni wale wale ambao walishajaribu awamu zilizopita na kushindwa vibaya.

 
 
 
nnamshauri akishindwa ajaribu hata big brother anaweza kutuwakilisha vyema kule
 
Lile jimbo la CCM, na wamemwaga posters kila kona, kila mti mpaka kwenye mitaro ya maji machafu. Halima hawezi kushinda.

Kuweka post kila kona si hoja. Hoja ni kugawana kura na Mbatia. Hivi huyu Mbatia akili zake bado zinafanya kazi sawa kweli, hasomi alama za nyakati bwana ntoke vipi? Hii sio 1995 bana.
 
sijajua kwa nn wapinzani huwa hawataki kushirikiana
 

Mimi ninamkubali kwa upiganaji lakini sio beauty!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…