Halima Mdee anastahili tuzo ya heshima ya uzalendo

Team JPM

JF-Expert Member
Nov 11, 2018
1,074
1,608
Katika mchakato wa kupitisha Mkataba wa Bandari, Halima Mdee alisimama kidete kutetea Maslahi ya taifa katika uwekezaji bandarini.

Halima Mdee hakusimama kama Mpinzani au mwana CHADEMAA bali kama Mzalendo, Mtetezi na Mpenda Nchi na Mlinzi wa Rasilimali za Taifa.

Mchuano ulikuwa mkali baina ya Spika na Mdee pamoja na Mdee dhidi ya wabunge wetu wa CCM. Ukiisikiliza video clips ya mchuano kizalendo, utabaini kwanba Halima Mdee ni Mzalendo na Jasiri linapokuja suala la Maslahi ya Taifa.

Kwakuwa sina Taasisi inayoweza kutoa Tuzo, napendekeza kwenu kwamba tumpe maua yake dada Mdee kwa kumzawadia Tuzo ya Heshima ya Uzalendo.

Kama Taasisi zitaogopa mkono wa serikali, basi sisi wazalendo wa Jamii Forums tutoe Tuzo hii. Ni aibu na usaliti kumuacha Halima bila tuzo katika jambo hili.

Nationalist and Patriotic Award 2023 for Hon. Halima Mdee.

Naomba kuwasilisha.
 
Katika mchakato wa kupitisha Mkataba wa Bandari, Mh. Halima Mdee alisimama kidete kutetea Maslahi ya taifa katika uwrekezaji bandarini.
Halima Mdee hakusimama kama Mpinzani au mwana Chadema bali kama Mzalendo, Mtetezi na Mpenda Nchi na Mlinzi wa Rasilimali za Taifa
Mchuano ulikuwa mkali baina ya Spika na Mdee pamoja na Mdee dhidi ya wabunge wetu wa CCM.
Ukiisikiliza Video clips ya mchuano kizalendo, utabaini kwanba Halima Mdee ni Mzalendo na Jasiri linapokuja suala la Maslahi ya Taifa.
Kwakuwa Sina Taasisi inayoweza kutoa Tuzo, napendekeza kwenu kwamba Tumpe Maua yake Dada Mdee kwa kumzawadia Tuzo ya Heshima ya Uzalendo.
Kama Taasisi zitaogopa mkono wa serikali, basi sisi wazalendo wa Jamii Forum tutoe Tuzo hii.
Ni Aibu na Usaliti kumuacha Halima bila tuzo katika jambo hili.
NATIONALIST AND PATRIOTIC AWARD 2023 FOR HON. HALIMA MDEE.
Naomba kuwasilisha.
Anatokea chama gani huyu Halima Mdee?
 
Anatokea chama gani huyu Halima Mdee?
Good question, akikujibu mtoa mada hii, pls ni tag nami, middle class wa kitanzania ni shida, mtoa mada hujui kuwa mdee hakusitahili kuwemo bungeni?kodi yangu inapotea bure kulipa mshahara wake
 
Hakuna kitu pale, ule ulikuwa mchezo ulioratibiwa na kupangiliwa vizuri. Kumbuka wapo Bungeni kama "wapinzani" , kwahiyo ni lazima wapinge ili kuionesha jamii kuwa wapo wabunge waliopinga.
 
Hakuna kitu pale, ule ulikuwa mchezo ulioratibiwa na kupangiliwa vizuri. Kumbuka wapo Bungeni kama "wapinzani" , kwahiyo ni lazima wapinge ili kuionesha jamii kuwa wapo wabunge waliopinga.
Alitimiza wajibu wake kama Mtanzania, kama Mwanasheria. Kwani wengine uliwasilia?. Mara zote amesimama kwa Rasilimali za Taifa.
Ondoa chuki, tumpe Maua Yake
 
Good question, akikujibu mtoa mada hii, pls ni tag nami, middle class wa kitanzania ni shida, mtoa mada hujui kuwa mdee hakusitahili kuwemo bungeni?kodi yangu inapotea bure kulipa mshahara wake
Ni matatizo ya kufikiri.
Kwa namna yeyote ile, Chadema kilipaswa kuteua wabunge wa viti maalum kwenda bungeni. Ila kwa Mh. Halima kwenda Bungeni, anaitendea haki nchi yake. Haijalishi kama aliteuliwa au alijiteua lakini anachokifanya kinakidhi haja.
Hao wanaokula kodi zako kihalali ndio walioshindwa kuhoji vifungu vyenye ukakasi katika Mkataba.
Acha Roho mbaya, Mpe Mdee Maua Yake
 
Sawa JF expert since 2018,Nami ninaweza kujiteua na kuingia bungeni!wapi wajibu wa kisheria?kuna hotuba former President Magufuri anajiuliza hivi tumelogwa na nani?,pls mtu amjibu
 
Back
Top Bottom