Asha Abdala
JF-Expert Member
- Mar 21, 2007
- 1,130
- 44
Halima Mdee, Msemaji wa kambi ya upinzani bungeni wizara ya sheria na katiba leo ameuchambua mswada wa mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa uliowasilishwa bungeni. Mbunge huyo ameeleza wazi kwamba serikali ya CCM haina nia ya kuongeza demokrasia nchini badala yake imeonyesha woga wa kiasiasa. Maoni yake hayo yametokana na Serikali kuwasilisha bungeni mswada ambao umetoa nafasi kwa vyama vya siasa kuungana lakini wakati huo huo ukitamka kwamba kama vyama hivyo vikiungana rais, wabunge, madiwani na viongozi wote wa kuchaguliwa watapoteza nafasi zao na uchaguzi kurudiwa. Ametaka sheria iruhusu pia aina zingine za ushirikiano kama alliance na coalition, badala ya kulazimisha kuungana pekee.
Halima Mdee amekwenda mbali zaidi na kuchambua kuwa kikwazo kikubwa ni baadhi ya vifungu vya kikatiba ambavyo vinatamka kwamba mbunge akihama chama anapoteza nafasi yake. Lakini ameeleza kuwa katiba hiyo hiyo inajichanganya kwa kuwa upande wa Rais hakuna sharti la Rais kupoteza nafasi kama atahama chama. Mdee ameitaka serikali ya CCM ikubali mabadiliko ya katiba kwa ajili ya kupanua demokrasia nchini.
Mbunge huyo ametaka vilevile, msajili wa vyama kutangaza kwenye vyombo vya habari ripoti za fedha za vyama zinazoonyesha mapato na matumizi.
Akichangia mswada huo, mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ameipongeza serikali kutaja katika mswada huo kwamba mahesabu ya vyama sasa yatakaguliwa na Mkaguzi Mkuu wa Serikali(CAG) hasa fedha zinazotokana na ruzuku. Amesema hatua hiyo itasidia pia kudhibiti vyanzo vichafu vya fedha za kuendesha vyama ambapo kwa kiasi kikubwa chama tawala kimekuwa kikiendeshwa kwa fedha nyingi za namna hiyo ikiwemo katika uchaguzi.
Zitto ametaka pia sheria hiyo ya vyama vya siasa itoe fursa ya kupatikana kwa National Consesus ama muafaka wa kitaifa. Amesema hatua hiyo itawezesha kuwa na tunu za kitaifa pamoja na utofauti wa vyama vya siasa. Ametoa mifano ya nchi duniani ambazo zina mfumo wa kuwa na national consesus
Asha