Hali yazidi kuwa tete kwa wakulima, mbolea kg 50 yafikia Tsh. 140,000

Hivi kitu gani kinatufanya tuendelee kutumia mbolea ya chumvichumvi,wakati kwa muda mrefu mikoa ilotumia mbolea hizo ardhi imeharibika i.e Iringa.Wakati wenzetu wanatumia mboji organic. Wataalamu mnieleweshe hapa.Nilichojifunza chumvichumvi inazuia ardhi kujitengenezea mbolea kwa njia ya asili.Yaani bacteria wanatoweka.Hii imekaaje wataalamu.
 
Dah hii nchi saizi haipo sawa kabisa kuna tatizo kubwa mahali na shida kubwa hatuna viongozi tuna watawala wapuuzi ikiwemo bi mdashi yani amn ata kuongelea chochte cha msingi ***** mbolea hadi 140,000 sijawai experience ujinga kama huu
 
Hivi kitu gani kinatufanya tuendelee kutumia mbolea ya chumvichumvi,wakati kwa muda mrefu mikoa ilotumia mbolea hizo ardhi imeharibika i.e Iringa.Wakati wenzetu wanatumia mboji organic. Wataalamu mnieleweshe hapa.Nilichojifunza chumvichumvi inazuia ardhi kujitengenezea mbolea kwa njia ya asili.Yaani bacteria wanatoweka.Hii imekaaje wataalamu.
Tatizo mbolea za chumvi zinaongeza kiwango cha Acid kwenye udongo wakati bacteria wanaitaji acid kwenda base ( 6-8 pH ) ili kuweza kufanya michakato mbali mbali kwenye udongo so unakuta bacteria wanakufa au kuwa dormant kutokana na kiwango Cha Acid kuwa kikubwa ( pungufu ya 5 pH )

Pia Mkuu kutumia mbolea za organic sio lahisi kwa nchi yetu kwasababu
✓ mifugo inakuwa njee ya zizi kwa muda zaidi ya masaa 12 kwaiyo mbolea aiwezi kutosha shambani
✓ maandalizi ya mbolea za organic kama vile mboji inahitaji elimu na maharifa ili kuweza kutengeneza mboji yenye ubora
✓ wakulima wengi hawaamini kwenye kilimo Cha organic kwa sababu matokeo yake sio ya haraka pia wengi wanafanya by default
 
Habari za kazi Wana JF/wadau/wananchi? Huku kwetu DAP ni laki na elfu arobaini.140,000/=hivi kwa Bei hii kilimo kitafanyika mwaka huu?

Hebu tupaze sauti, tuwasaidie wakulima hali ni Tete msimu huu.
Nahisi kuna makusudi hapa ili bei ya mahindi ipae kwa lazima!
 
Leo katika pitapita zangu za huko mashambani, kwakweli wakulima hawana hamu kabisa na kipindi hiki kutokana na bei za pembejeo.

Huyu huyu mkulima akinunua mbolea ya DAP kwa Tshs 105000 bado usafirishaji kuelekea huko pembezoni yaliko mashamba ambako mfuko mmoja wa mbolea unagharimu Kama 5000 mpaka 10000.

Upande wa pili wa shilingi, debe la mahindi ni Tshs 4000 mpaka 5000, yaani mtu akihudhuria kikao cha saa moja ambacho malipo ni Tshs 10000, tayari anaweza kupata debe mbili za mahindi, ambapo shughuli ya kuzalisha debe hizo mbili humchukua muda mwingi mkulima ambao huambatana na uchovu mkubwa.

Kusema kweli Kama taifa tunakoelekea siyo kuzuri, kwanini wakulima wanateseka namna hii?!!!
Yaani mkulima ni amekuwa mnyonge kwelikweli.

Mwisho, ukiongea na wakulima kumi kuhusiana na kilimo, nane watakwambia huyu mama Samia yaani ameshusha bei za mazao yetu hata hatumwelewi kabisa, Bora Magufuli alisema " Wakulima pandisheni bei za mazao yenu, asiyetaka akalime shamba lake " na alisema tutamkumbuka na kweli tumemkumbuka ndani ya muda mfupi sana.
 
Magufuli alivyowaambia mlime wenzenu wakiwa wamejifungia ndani kwa sababu ya corona haumkuelewa somo??
 
Nahisi kuna makusudi hapa ili bei ya mahindi ipae kwa lazima!
Hamna makusudi almost 2 years hakukuwa na uzalishaji duniani watu wamejifungia corona virus, what do you expect??kwamba mbolea na pembejeo zinajiotea tuu huko viwandani watu wamefungiwa wasitoke, mbona bado
 
Sisi SUKUMA GANG ndo tunakomolewa sisi KWA kutaka kuilinda legacy na Sasa ni mwendo wa tu TOZO,VIFURUSHI,MAFUTA,UMEME,MAJI,MBOLEA,MFUMUKO WA BEI n.k
Lazima nyie Sukuma gang tuwakomoe..Boss wenu alikuwa anaingilia sana mambo ya watanzania mfano angekuwa ametoa pesa kupunguza makali..Hiyo tunaita kuharibu mfumo wa masoko
 
Yaani kwa sasa shamba imekua changamoto. Mtu unahitaji DAP , bado UREA ongeza na CAN hapo madawa. Mafuta kwa ajili ya kumwagilia ! (Gharama za trekta na vibarua) Wengine mito tunayotumia imefikia hatua inabidi tupangiane siku za kumwagilia maana maji yamekua kidogo sana au labda uamke usiku sana. Na bei ya mazao kwa kweli haiendani na gharama za uendeshaji ona Nyanya mwaka huu, Pilipili hoho , Nyanya chungu afadhali Maharage yanatubeba.

Kwa nilivyowaza mimi Bustan naipumzisha yale mashamba nayarudisha kizamani nitatia samadi ya kutosha kisha yanakaa mpaka mwezi may ndo nayafufua tena. Vinginevyo hiki kilimo tutakichukia
labda wamefanya hivyo kuondoa hizo mbolea za sumu sokoni..
 
Habari za kazi Wana JF/wadau/wananchi? Huku kwetu DAP ni laki na elfu arobaini.140,000/=hivi kwa Bei hii kilimo kitafanyika mwaka huu?

Hebu tupaze sauti, tuwasaidie wakulima hali ni Tete msimu huu.
Mkuuu wameziba masikio kabisaaaa, wanaleta gonjera za kujenga kiwanda dodoma.

Mimi CAN nilikua nanunua 47 kwa 50kg sasa ni 630000/=.kimsingi wakulima tunapitia kipindi kigumu sanaaaa, NPK kutoka 63 hadi 100000
 
Hivi kitu gani kinatufanya tuendelee kutumia mbolea ya chumvichumvi,wakati kwa muda mrefu mikoa ilotumia mbolea hizo ardhi imeharibika i.e Iringa.Wakati wenzetu wanatumia mboji organic. Wataalamu mnieleweshe hapa.Nilichojifunza chumvichumvi inazuia ardhi kujitengenezea mbolea kwa njia ya asili.Yaani bacteria wanatoweka.Hii imekaaje wataalamu.
kabisa mkuu zinaharibu ardhi yetu ila sijui mamlaka haiwezi kusema hadharani!? maybe ni biashara za mabwana wakubwa..
 
Yaani kwa sasa shamba imekua changamoto. Mtu unahitaji DAP , bado UREA ongeza na CAN hapo madawa. Mafuta kwa ajili ya kumwagilia ! (Gharama za trekta na vibarua) Wengine mito tunayotumia imefikia hatua inabidi tupangiane siku za kumwagilia maana maji yamekua kidogo sana au labda uamke usiku sana. Na bei ya mazao kwa kweli haiendani na gharama za uendeshaji ona Nyanya mwaka huu, Pilipili hoho , Nyanya chungu afadhali Maharage yanatubeba.

Kwa nilivyowaza mimi Bustan naipumzisha yale mashamba nayarudisha kizamani nitatia samadi ya kutosha kisha yanakaa mpaka mwezi may ndo nayafufua tena. Vinginevyo hiki kilimo tutakichukia
Mkuu kama uko eneo ambalo samadi inapatikana kwa urahisi fanya hivyo.
 
Back
Top Bottom