Hali yazidi kuwa tete kwa wakulima, mbolea kg 50 yafikia Tsh. 140,000

Yaani kwa sasa shamba imekua changamoto. Mtu unahitaji DAP , bado UREA ongeza na CAN hapo madawa. Mafuta kwa ajili ya kumwagilia ! (Gharama za trekta na vibarua) Wengine mito tunayotumia imefikia hatua inabidi tupangiane siku za kumwagilia maana maji yamekua kidogo sana au labda uamke usiku sana. Na bei ya mazao kwa kweli haiendani na gharama za uendeshaji ona Nyanya mwaka huu, Pilipili hoho , Nyanya chungu afadhali Maharage yanatubeba.

Kwa nilivyowaza mimi Bustan naipumzisha yale mashamba nayarudisha kizamani nitatia samadi ya kutosha kisha yanakaa mpaka mwezi may ndo nayafufua tena. Vinginevyo hiki kilimo tutakichukia
 
Tumieni NPS na minjingu..sokuhizi zimeboleshwa
 
Hivi mbona hamuelewi, puuzeni huo uzushi wa bei ya mbolea🐒
3007985_Screenshot_20211120-213411_Drive.jpg
 
Habari za kazi Wana JF/wadau/wananchi? Huku kwetu DAP ni laki na elfu arobaini.140,000/=hivi kwa Bei hii kilimo kitafanyika mwaka huu?

Hebu tupaze sauti, tuwasaidie wakulima hali ni Tete msimu huu.
Nakwambia kila sekta kitu kinapanda, vioo vya madirisha vilikuwa vinauzwa 75000 sasa ni 170000, yani nikisikia akina mwigulu nabaki kushangaa mambo wanayosema na uhalisia mtaani.
Leo nimemskia waziri anasema eti wastaafu hawalipwi mafao yao kisa kuna waajiri walikuwa hawapeleki michango.
Nikajiuliza kuna wastaafu wengine mwaka wa 5 hawajalipwa.
 
Back
Top Bottom