Hali ya wanachuo mtaani

Well, lakini pia mfumo wa kujiajiri nao haupo favourable kabisa, ili ujiajiri bongo kisha uje kutoboa ie. Business lazima uwe na mtaji mkubwa at least from 3M, niambie kijana alietoka chuo anapata wapi hiyo pesa, pesa chini ya hapo kutoboa ni ngumu sana, lakini pia tukumbuke hizi kazi za kujiajiri hazijawahi kumtoa mtu, huwa tunajipa moyo pambana ila kiuhalisia mafanikio yake mara nyingi ni hela ya kula na kulipa kodi ndio inayopatikana,
Mimi ni mhanga nimemaliza chuo mwaka jana sijui nini kitakachotokea huko mbele japokua kurudi nyumbani nimekaza japo maisha bado yanagonga kwenye mshono
 
uliruka kiunzi ki1 hataree sanaaa. Uwiiiiih
 
Tatizo lenu mnadharau biashara.
Kuna wadau hapo juu wanawashangaa graduates mmoja anauza kande, mwingine vitumbua.

Cha ajabu hapo ni kipi hasa?? Ndivyo biashara inavyoanza kiugumu, siku mtaji ukikua akafanya makubwa mnaanza kusema anadanga. Akili mgando kabisa hizi
 
Bora hata wewe unayepambana,,, Kuna raia washajikatia tamaa kabisa.
 
Siyo mchezo
Vijana watafutiwe namna wezeshi,, ukikutana na mtu aliyehitimu hivi karibuni atakwambia ideas nzuri sana, mawazo Bora na yenye ubunifu wa hali ya juu, na unaona kabisa huyu kijana kwa namna anavyowaza anaenda kuleta mabadiliko makubwa sana kwenye jamii, familia na taifa kwa ujumla. Lakini baada ya mda kidogo mtaani kila kitu kinayeyuka.........! Daah
.
 
Anakuwa Afsa usafirishaji (Bodaboda)
 
lakini pia tukumbuke hizi kazi za kujiajiri hazijawahi kumtoa mtu, huwa tunajipa moyo pambana ila kiuhalisia mafanikio yake mara nyingi ni hela ya kula na kulipa kodi ndio inayopatikana,
Nani aliyekudanganya mdogo wangu kuwa kujiajiri hakujawahi kumtoa mtu?
Shida bado haujajikubali; akili yako imelenga status job ndio kila kitu.. umeamka asubuhi umechomekea umevaa tai unaenda kwa office unapigwa kiyoyozi.
Kuna watu wamejiajiri pesa wanayoingiza kwa mwezi mbunge akasome
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…