Wahitimu wa vyuo na maisha ya utaftaji mtaani

Theb

JF-Expert Member
Jan 25, 2019
3,929
7,268
Habari zenu wana jamii forums? Hususani jukwaaa hili la stories of change Nitumaini langu nyote ni wazima.

Andiko hili litaangazia maisha ya vijana wahitimu vyuo waliotegemea kuajiriwa na hali imekua tofauti na matarajio yao. Naanza kwa kuelezea maisha ya mtaani na baadhi ya fursa zenye kuhitaji.mitaji na zisizo hitaji mitaji na changamoto zake na vipi tunaweza kuzikabili changamoto na kutuwezesha kupita katika baadhi ya hizo fursa na tuweze kujikwamua.

Maisha ya mtaani katika jamii zetu karibia kote yana mfanano kwa asilimia kubwa. Kuanzia ngazi ya familia za wahitimu walio wengi zinafanana kichumi kitamaduni na hata kimalengo. Familia nyingi za jamii zetu Tanzania tunasoma ili tuajiriwe na sio kujiajiri kwa waliowengi, hali iliyopo kwa sasa sio siri imeenda kinyume na malengo na matarijio ya vijana waliokuwa wanasoma na wanaoendelea kusoma mashuleni mpaka vyuoni.

Nitaanza na kuelezea changamoto zinazokabili vijana wahitimu wa vyuo kwa ujumla kama ifuatavyo:-

1. Kutokujiamini na kutokubaliana na ukosefu wa ajira kwa vijana wengi, nidhahiri kuwa vijana wahitimu wa vyuo ni ngumu kukubali kuwa ajira ni chache hivyo inawawia ngumu kufanya maamuzi ya kuanza kitu kipya katika fursa zilizopo mtaani.

2. Mazingira yanoyowazunguka wahitimu, jamii inawahukumu wahitimu bila kuwapa motisha au kuwashika mkono kifedha au kiushauri. Ni kawaida mtaani kusikia mtu akimwambia muhitimu umesoma una nini zaidi kunizidi..? Hizi kauli hukatisha tamaa na kuwaongezea sonona na paniki.

3. Kukosa kampani au muunganiko na watu waliotangulia kwenye mitaa, hapa unakuta wahitimu hawana muunganiko na waliotangulia kwenye mitaa kiutaftaji. Japo hio sio sana.(lack of support)

4. Kutokua na mitaji, hususani kwenye biashara au fursa zinazohitaji mitaji.

5. Kutokua na uelewa wa mitaa na utaftaji wenyewe. Yaani kutozijua fursa au kutozitambua biashara na majira yake. Maana kila biashara ina majira yake.

6. Kuchagua kazi. Hii inahusika saana baadhi ya wahitimu hii changamoto kubwa kwao. Hawako tayari kubeba hata gunia wanaona aibu au wanaona haiba yao hawastahili kubeba gunia.

Jinsi gani wanaweza kupambana na hizi changamoto:-

1. Kujikubali na kujichanganya na wataftaji wengine mitaani bila kuwaza au kujutia muda uliopoteza shuleni na vyuoni.

2. Kukubali hali halisi hususani kuwa tayari kwa kazi yoyote bila kuchagua kazi. Mfano baadhi ya wahitimu ina muwia ngumu kufanya kazi kama kuuza mkaa au kununua chupa za plastiki zilizotumika kwa kuhofia taaluma yake au watu watamuonaje.

3. Kuzitambua fursa na kuwa tayari kupambana nazo maana utaftaji mtaani ni ushindani.

4. Kuyajua mazingira ya biashara unayotaka kwenda kuanzisha, hapa itahitaji muunganiko na wanaoitambua biashara husika unayotaka kuanzisha kwenye mazingira unayopanga.

5. Kupunguza matumizi yale yasiyo muhimu, hapa matumizi yale yasiyomuhimu ambayo yanafuja pesa hainabudi kuyaacha. Mfano unywaji wa pombe, kubet, uvutaji wa sigara au ulevi wowote na anasa zingine zinazo hitaji pesa.

6. Kufanya uchaguzi sahihi wa kile unachoweza kukifanya mtaani na sio kufwata mkumbo. Je mhitimu unaweza kitu gani kama ni kilimo basi fanya kilimo kama ni ufundi fanya ufundi.

Fursa zilizopo katika jamii zetu ambazo wahitimu au mtaftaji yeyote anaweza kuzitazama na kuamua kuanza kujipatia kipato kupitia hizo fursa. Nitataja ambazo nimeziona na nazifahamu na watu wanafanya nitaanza na zisizo hitaji mitaji mikubwa au zisizo hitaji.mitaji kabisa na baada ya hizo nitaangazia zenye uhitaji wa mitaji angalau mikubwa kiasi.

1. Fursa zisizo hitaji mitaji na zisizo hitaji mitaji mikubwa sana.

(i) Vibarua viwandani.
Kwa wale wahitimu waliopo mijini kuliko na viwanda kuna upatikanaji wa vibarua wa kutwa na wale wanaolipwa kwa wiki kwenye viwanda. Kuna kubeba mizigo viwandani kupakia na kupakua mizigo inayoningia na inayotoka na kazi zingine kulingana na kiwanda husika.

(ii) Fursa kwenye standi za mabasi ya abiria.
Pia kwenye standi za mabasi kuna baadhi ya fursa zisizohitaji mitaji au zinazohitaji mitaji midgo, mafano kubeba mizigo ya abiria kuwa wakala wa kukata tiketi na kuunza bidhaa ndogo ndogo kama karanga maji na juisi pia.

(iii) Kununua chupa za plastiki na kwenda kuziuza.
Hapa kuna hii fursa ya kununua au hata kuokota chupa za plastiki na kwenda kuuza mfano kilo moja unanunua kuanzia 300 hadi mia 400 na kuuza iliyosagwa ni kuanzia 800 hadi 1200 isiyo sagwa ni 800 bei ya kuuza. Hii ni fursa japo inadharauliwa.

(iv) Kuwa dalali wa mazao shambani au magari ya kusafurisha mizigo au dalali wa nyumba viwanja nk.
Hii nayo haihitaji mtaji kwenye kuanza uaminifu wako na kujua chimbo za unachofanya ndio mtaji wako.

(v) Kuanzisha tuition mtaani kwenu.
Hii pia saa zingine haihitaji mtaji itajitaji tu utayari wako na uwepo wa wanafunzi wanaosoma na kuitangaza. Japo maemeo mengine hii haina nafasi maana muitiko unakua mdogo.

(vi) Kubeba mizigo kwenye masoko kupakua na kupakia mazao na bidhaa mbalimbali.
Tunaweza kuidharau lakini ni fursa ukibeba mizigo 25 yenye kulipwa 1000 kila mzigo kwa siku una shilingi 25000. Inafaa japo haitaki mtu mwenye aibu na usharobaro.

(v). Kipaji kiwe cha uandishi, uimbaji, ususi, uchoraji, na michezo.
Kipaji pia ni fursa kubwa tena isiyo hitaji mtaji ila itataka utayari wako kujituma na ubunifu zaidi na uvumilivu uliomithilika.

Hizo ni baadhi ya fursa zisizo hitaji mitaji mikubwa au zinazohitaji mtaji mdogo.

2. Fursa zinazohitaji mitaji mikubwa au ya kiasi. Nitataja baadhi na ambazo ni rahisi kujichanganya kama ifuatavyi:-

(i). Kununua mazao mashambani na kuleta mjini kwenye masoko. Hapa kuna mazao mfano mboga mboga kama nyanya, mchicha, na mboga mboga zoote zinazolimwa nchini na mazao ya nafaka kama mahindi, mchele, viazi, ndizi mbivu na za kupika, machungwa na matunda mengine hizi zinataka mitaji yaweza kuwa laki kadhaa mpaka milioni kadhaa kutegemea na biashara unayotaka mana mfano huwezi linganisha anaepeleka mchicha sokoni na anaepeleka viazi mviringo mitaji itatofautiana na kinwa zaidi kutambua misimu mizuri ya hiyo biashara unayotaka kuanzisha.

(ii). Umachinga wa kuuza vitu mtaani kando ya barabara au kutembeza au kutengenexa banda lako sehemu inayoonekana kwa wateja. Hii inahitaji mtaji nayo inategemea na biashara husika.

(iii). Kilimo, uvuvi na ufugaji. Hizi nazo ni fursa lakn zinahitaji mtaji maana kilimo lazima uwe na shamba, mbegu, pembejeo za kilimo kama mbolea na dawa za kupulia kuua vijidudu hatarishi kwa mazao nacho kilimo kitategemea na aina ya mazao unayolima. Uvuvi pia utahitaji mtaji kuninua nyavu nk ufugaji pia kama ni kuku lazima uwe na mtaji wa kununua kuku, pumba, uduvi na mifupa. Hii ni baadhi ya mifano.

(iv). Udereva boda boda au bajaji huu nao utahitaji uwe na mtaji kama utahitaji boda boda yako mwenyewe lakini kama utapata boda boda ya mtu itakubidi ujifunze kuemdesha pikipiki au bajaji.

(v). Kuanzisha saloon zote za kunyoa nywele na kusuka nywele. Hapa kwa wanaume na kwa wanawake kuna kunyoa na kusuka hivyo sehemu uliyopo kama panauhitaji hii ni fursa.

(vi). Zipo zingine kama kutuma pesa yani (m pesa, airtel money, tigo pesa na halopesa) ndio makato mmmhh yameongezwa lakini ni fursa.

Zipo fursa nyingi na nyingi hizo ni baaadhi nikizitaja na kuelezea zote andiko halitatosha.

Hitimisho.
Nimetoa baadhi ya fursa na nilianza kwa kutoa changamoto zinazowakabili wahitimu ni baadhi sio zote. Ila ushauri wangu kwa vijana wasaka tonge wahanga wa ajira na vijana woote kwa ujumla napenda kutoa ushauri kama ufuatao:-

(i). Uvumilivu kwenye hizo fursa tunazoenda kuanzisha maana nako pia tutakutana na changamoto za kudondoka kukwama nakadhalika ila tusivunjike moyo na tusikate tamaa mapambano yaendelee.

(ii). Tuzijue hizo fursa na kutambua majira ya hizo fursa itasaidia kutambua muda gani muafaka wa kuanza tusikurupuke kuna kuanguka pia.

(iii). Kama unamtaji usianze na pesa yote ya mtaji maana hauna uhakika 100% kuwa itaenda sawa hivyo kujipanga kwa hilo ni muhimu.

(iv). Kupata ushauri kwa waliofanikiwa ni muhimu itakuongezea maarifa kwa yale usiyo yakua.

(v). Usimwamini kila mtu katika kufanya utaftaji wako wengine watakukwamisha. Mfano wanao kopa hawa ni sumu kwako uaneanza utaftaji.

(vi). Tambua hitaji la jamii ikizungukayo. Kama jamii inataka mahindi wapelekee mahindi na sio mchele. (Hitaji la wateja).

(vii). Ishi vizuri na watu na waheshimu watu kwa imani zao makabila yao na rangi zao.

Hapa nimefikia mwisho wa topiki yangu. Natumaini kidogo kitaeleweka kwa wengi haijaelezea kila.kitu ila nimeelezea kwa uchache kwa yale niliyojionea na kujifunza mtaani
 
Habari zenu wana jamii forums hususani jukwaa hili la stories of change. Nitumaini langu nyote ni wazima.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umejitahidi sana kuandika kwa ajili ya uzi kua kwenye jukwa la Stories of Change
 
Mtu kakaa darasani for more than 15yrs akijiandaa kwa ajira then unataka within months afute imani hiyo sio kiturahisi kwa kweli.

Wape muda kubadilisha imani. Maana sio rahisi kubadilisha imani.
 
Tujitajidi kuifuta kidogo kidogo japo ni ngumu ila lazma tukubali ukweli ndipo tupige hatua nyingine
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom