Maisha baada ya Chuo Kikuu

Mr What

JF-Expert Member
Oct 22, 2016
1,175
2,080
MAISHA BAADA YA UNIVERSITY

Mwanzo wa masomo katika chuo chochote kile hasa chuo kikuu huwa mzuri sana kwani wengi wanao pelekwa kusoma huwa na furaha na wengine wanahisi ndoto zao za mafanikio zimetimia. Ni Kipindi ambacho wanachuo uanza kuwasili vyuoni, ni kipindi cha Furaha kwa kila mwanachuo, hii ni kutoka na kuwa wengine upata fedha (BOOM) kutoka bodi ya mikopo, lkn wale wanaokosa mkopo huwa na Furaha kwani wanapata fungu kutoka kwa wazazi au wafadhiri wao, ni kipindi cha kupata marafiki, kubadilisha mazingira nk.

Kwa Leo sitazungumzia sana maisha ya chuoni bali maisha baada ya chuo. Hata hivyo ukweli ni kwamba maisha ya chuoni ni sawa na uwanja wa fujo, Wanachuo wengi wanapokaribia kumaliza masomo yao (Last year) wanakuwa na matarajio mengi, hata hivyo Vijana wengi wanaomaliza chuo upitia changamoto nyingi sana:-

Wengi wa wanachuo waliomaliza/wanaomaliza vyuo ambao hawapewi ajira ya moja kwa moja na serikali wamejiingiza katika michezo ya kubahatisha ambayo kamari inayoendeshwa kisasa kupitia mashine maalum au simu za mkononi.Idadi yao inazidi kuongezeka hasa maeneo ya mjini ambako wasomi wengi hukimbilia kwa kile wanachokiamini watapata ajira kwa urahisi.
Wanachuo wengi waliopo mtaani wanajihusisha na kazi tofauti na kile walichokisomea. Mmoja wa wanafunzi hao hivi sasa amekuwa dalali wa magari ili aweze kupata riziki yake ikiwa ni tofauti kabisa na kile alichokisomea chuoni, mfano nimeona kijana aliyemaliza shahada ya biashara lakini anafanyakazi ya ujenzi,Mwingine ni mwalimu wa masomo ya ziada ‘tution’ kazi ambayo ni tofauti kabisa na masuala ya uchumi aliyosomea chuoni.

Vijana wengi waliomaliza elimu ya juu bado ni tegemezi kutokana na ukweli kwamba hakuna ajira za moja kwa moja toka serikalini za kuweza kuwaajiri wanachuo wote, hali inayosababisha wengi wao kuendelea kuwa tegemezi, mfano mwanafunzi mhitimu mwingine wa karibu alimaliza chuo kikuu toka mwaka 2012/2013 akifaulu vyema katika masomo ya uhifadhi mazingira lakini mpaka sasa bado anawategemea wazazi wake pamoja na umri wake mkubwa wa miaka 32.Hii kiukweli haileti afya katika uhalisia wa maisha.

Zamani ilikuwa ni kitu cha ajabu kwa kijana msomi nchini kukamatwa kwa masuala ya wizi ama utapeli wa aina yoyote. Ilionekana mwizi au kibaka ni yule asiye na elimu. Hivi sas hali imekuwa tofauti, vijana wengi wamekuwa wezi kwa njia ya mtandao na baadhi kutumia elimu yao kujifanya maofisa wa serikali ili watimize dhamira yao.wengi walitarajia kupata maisha mazuri kwa haraka bila kujua kuwa maisha hayataki tamaa wala haraka.

Biashara ya umalaya, hili limekuwa janga kubwa zaidi nchini kwa sasa likiwaathiri zaidi watoto wa kike ambao walizoea maisha ya chuo kupewa pesa na serikali baada ya kumaliza chuo na kukosa ajira baadhi yao wamejiingiza kwenye biashara ya kuuza miili yao kwa watu wenye pesa ili wakidhi mahitaji yao muhimu na wengine wakiahidiwa kutafutiwa kazi.

Kushamiri kwa rushwa ya ngono,Ukosefu wa ajira nchini umepelekea kushamiri kwa kasi rushwa ya ngono na wahanga wakubwa wamekuwa ni watoto wa kike. Viongozi wengi hasa wenye nafasi au dhamana ya kuajiri wanatumia mwanya huo kuwarubuni watoto wa kike wenye uhitaji wa kazi kwa kisingizio cha kuwapa ajira wakitimiza masharti yao. Wengi ni wahanga wa suala hili hali inayopelekea kuenea kwa kasi kwa maambukizi ya UKIMWI na wengine kupata msongo wa mawazo na kuathirika kisaikolojia.

Vijana wa kiume kulelewa na wanawake matajiri. Huu ni mchwa mwingine mkubwa unaomaliza kizazi cha sasa cha vijana wasomi ambao kulingana na ugumu wa maisha wengi wao wanalelewa na akina mama wenye pesa akipewa kila kitu na yeye kumtimizia mahitaji yake ya ngono.Huu ni utumwa wa mapenzi ambapo vijana wengi wanaingia kwa kukosa pesa au mahitaji muhimu bila kujali afya zao.

Rafiki yangu mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe mtandaoni jana nilikuwa nilikuwa naongea aliwahi kuthibitisha akisema: “Kaka Audax ni kweli nipo na mama… kanipa gari na nyumba na kila siku analala kwangu, kuhusu afya sijali liwalo na liwe cha msingi siku zinaenda na ninafanya matanuzi nitakavyo na Noeli ameniahidi kwenda Mwanza kupumzika kidogo tukale raha" Kauli hii inathibitisha namna gani ugumu wa maisha unaua ndoto za vijana wengi wanaomaliza university.

Mzigo wa madeni.Pamoja na wengi wao kuamua kupambana na maisha ili waweze kusimama wenyewe kikwazo kikubwa kinakuwa mitaji hali inayowalazimu kuingia kwenye mikopo yenye riba kubwa na baadaye kujikuta wakiingia kwenye madeni makubwa. Dada mmoja nilimfundisha advance alinisimulia hivi majuzi “Kaka mimi nimekopa kwenye kikundi shilingi laki tano na natakiwa kurudisha elfu kumi kila siku kwa siku hamsini”, maana yake amekopa laki tatu anapaswa kurejesha laki tano. Ikumbukwe pia pamoja na kuwa hana ajira lakini deni lake alilokopeshwa na serikali wakati yuko chuo kadri muda unavyozidi kusonga mbele ndivyo riba inazidi kuongezeka.

✍🏽Ni ukweli usiopingika kuwa vijana wengi waliomaliza elimu ya juu wanapitia kipindi kigumu sana kwenye maisha yao kwa sababu ya tatizo sugu la ukosefu wa ajira nchini. Hivyo ni jukumu la kila Mtanzania mwenye uwezo au njia mbadala ya kuelekeza ni namna gani tunaweza kuwasaidia vijana wetu na hatimaye kuondokana na tatizo sugu la uhaba wa ajira.
Niwapongeze sana mliomaliza chuo mwaka huu na niwatahadharishe sana wale mnaotegemea kumaliza chuo miaka ya mbeleni, huku mtaani hakuna boom, hakuna kozi wala sup, cha ajabu zaidi unaweza kumaliza hata miaka mitano hujaulizwa cheti au GPA, huku kuna degree ya maisha tu.

Na, Audax M. Ikwataki
0765-090379
DAR ES SALAAM
 
Kwani ungeandika kichwa cha habari,MAISHA BAADA YA CHUO KIKUU tungekuona siyo msomi,hadi uchanganye kiswahili na kigeni?mnakwama wapi ninyi watoto wa kizazi hiki?
 
Kama huna point ya kuchangia we nyamaza tu mkuu.....
 
Uyo dalali wa magari ni jerrybanks

Ukweli mtupu umeandika.

Sent using Jamii Forums mobile app
dah wala sikutegemea,mkuu dah umenifanya nmecheka sana japo nlikuwa na huzuni.
Ni kweli nami ni mmoja wa wa hanga ndugu yangu maana nmehitimu hr toka 2016,ila mpka leo cheti kipo ndani nmehangaika sana na ajira hata ya kuosha vyombo mwisho nmeambulia zero.

So nikaamua kujiongeza na biashara ya kuuza magari used yaliyotumika japan na hata kuwaagizia watu kutoka Japan,sijutii kazi ninayoifanya lakini nimegundua kazi ambayo inafanywa na msomi na ambaye siyo msomi inatofauti mno,kwani sifanyi kazi ili nipate fedha bali nafanya kazi ili kum retain mteja aje kesho tena na kila akihitaji gari anifikirie mimi.
Hyo ni kutokana na nidhamu na uwazi katika biashara yangu hii kama dalali nashukuru mungu katika ote niliyowauzia gari wanageuka na kuwa jamaa na marafiki na hata baadae kuleta wenzao niwatafutie,kwaiyo ndugu yangu October man tusilalamikie serikali kwa kutunyima ajira bali kipindi ambacho hatuna ajira tuangalie tunafanya nini kwa kutumia elimu tulizozipata ili maisha yasonge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MAISHA BAADA YA UNIVERSITY

Mwanzo wa masomo katika chuo chochote kile hasa chuo kikuu huwa mzuri sana kwani wengi wanao pelekwa kusoma huwa na furaha na wengine wanahisi ndoto zao za mafanikio zimetimia. Ni Kipindi ambacho wanachuo uanza kuwasili vyuoni, ni kipindi cha Furaha kwa kila mwanachuo, hii ni kutoka na kuwa wengine upata fedha (BOOM) kutoka bodi ya mikopo, lkn wale wanaokosa mkopo huwa na Furaha kwani wanapata fungu kutoka kwa wazazi au wafadhiri wao, ni kipindi cha kupata marafiki, kubadilisha mazingira nk.

Kwa Leo sitazungumzia sana maisha ya chuoni bali maisha baada ya chuo. Hata hivyo ukweli ni kwamba maisha ya chuoni ni sawa na uwanja wa fujo, Wanachuo wengi wanapokaribia kumaliza masomo yao (Last year) wanakuwa na matarajio mengi, hata hivyo Vijana wengi wanaomaliza chuo upitia changamoto nyingi sana:-

Wengi wa wanachuo waliomaliza/wanaomaliza vyuo ambao hawapewi ajira ya moja kwa moja na serikali wamejiingiza katika michezo ya kubahatisha ambayo kamari inayoendeshwa kisasa kupitia mashine maalum au simu za mkononi.Idadi yao inazidi kuongezeka hasa maeneo ya mjini ambako wasomi wengi hukimbilia kwa kile wanachokiamini watapata ajira kwa urahisi.
Wanachuo wengi waliopo mtaani wanajihusisha na kazi tofauti na kile walichokisomea. Mmoja wa wanafunzi hao hivi sasa amekuwa dalali wa magari ili aweze kupata riziki yake ikiwa ni tofauti kabisa na kile alichokisomea chuoni, mfano nimeona kijana aliyemaliza shahada ya biashara lakini anafanyakazi ya ujenzi,Mwingine ni mwalimu wa masomo ya ziada ‘tution’ kazi ambayo ni tofauti kabisa na masuala ya uchumi aliyosomea chuoni.

Vijana wengi waliomaliza elimu ya juu bado ni tegemezi kutokana na ukweli kwamba hakuna ajira za moja kwa moja toka serikalini za kuweza kuwaajiri wanachuo wote, hali inayosababisha wengi wao kuendelea kuwa tegemezi, mfano mwanafunzi mhitimu mwingine wa karibu alimaliza chuo kikuu toka mwaka 2012/2013 akifaulu vyema katika masomo ya uhifadhi mazingira lakini mpaka sasa bado anawategemea wazazi wake pamoja na umri wake mkubwa wa miaka 32.Hii kiukweli haileti afya katika uhalisia wa maisha.

Zamani ilikuwa ni kitu cha ajabu kwa kijana msomi nchini kukamatwa kwa masuala ya wizi ama utapeli wa aina yoyote. Ilionekana mwizi au kibaka ni yule asiye na elimu. Hivi sas hali imekuwa tofauti, vijana wengi wamekuwa wezi kwa njia ya mtandao na baadhi kutumia elimu yao kujifanya maofisa wa serikali ili watimize dhamira yao.wengi walitarajia kupata maisha mazuri kwa haraka bila kujua kuwa maisha hayataki tamaa wala haraka.

Biashara ya umalaya, hili limekuwa janga kubwa zaidi nchini kwa sasa likiwaathiri zaidi watoto wa kike ambao walizoea maisha ya chuo kupewa pesa na serikali baada ya kumaliza chuo na kukosa ajira baadhi yao wamejiingiza kwenye biashara ya kuuza miili yao kwa watu wenye pesa ili wakidhi mahitaji yao muhimu na wengine wakiahidiwa kutafutiwa kazi.

Kushamiri kwa rushwa ya ngono,Ukosefu wa ajira nchini umepelekea kushamiri kwa kasi rushwa ya ngono na wahanga wakubwa wamekuwa ni watoto wa kike. Viongozi wengi hasa wenye nafasi au dhamana ya kuajiri wanatumia mwanya huo kuwarubuni watoto wa kike wenye uhitaji wa kazi kwa kisingizio cha kuwapa ajira wakitimiza masharti yao. Wengi ni wahanga wa suala hili hali inayopelekea kuenea kwa kasi kwa maambukizi ya UKIMWI na wengine kupata msongo wa mawazo na kuathirika kisaikolojia.

Vijana wa kiume kulelewa na wanawake matajiri. Huu ni mchwa mwingine mkubwa unaomaliza kizazi cha sasa cha vijana wasomi ambao kulingana na ugumu wa maisha wengi wao wanalelewa na akina mama wenye pesa akipewa kila kitu na yeye kumtimizia mahitaji yake ya ngono.Huu ni utumwa wa mapenzi ambapo vijana wengi wanaingia kwa kukosa pesa au mahitaji muhimu bila kujali afya zao.

Rafiki yangu mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe mtandaoni jana nilikuwa nilikuwa naongea aliwahi kuthibitisha akisema: “Kaka Audax ni kweli nipo na mama… kanipa gari na nyumba na kila siku analala kwangu, kuhusu afya sijali liwalo na liwe cha msingi siku zinaenda na ninafanya matanuzi nitakavyo na Noeli ameniahidi kwenda Mwanza kupumzika kidogo tukale raha" Kauli hii inathibitisha namna gani ugumu wa maisha unaua ndoto za vijana wengi wanaomaliza university.

Mzigo wa madeni.Pamoja na wengi wao kuamua kupambana na maisha ili waweze kusimama wenyewe kikwazo kikubwa kinakuwa mitaji hali inayowalazimu kuingia kwenye mikopo yenye riba kubwa na baadaye kujikuta wakiingia kwenye madeni makubwa. Dada mmoja nilimfundisha advance alinisimulia hivi majuzi “Kaka mimi nimekopa kwenye kikundi shilingi laki tano na natakiwa kurudisha elfu kumi kila siku kwa siku hamsini”, maana yake amekopa laki tatu anapaswa kurejesha laki tano. Ikumbukwe pia pamoja na kuwa hana ajira lakini deni lake alilokopeshwa na serikali wakati yuko chuo kadri muda unavyozidi kusonga mbele ndivyo riba inazidi kuongezeka.

✍🏽Ni ukweli usiopingika kuwa vijana wengi waliomaliza elimu ya juu wanapitia kipindi kigumu sana kwenye maisha yao kwa sababu ya tatizo sugu la ukosefu wa ajira nchini. Hivyo ni jukumu la kila Mtanzania mwenye uwezo au njia mbadala ya kuelekeza ni namna gani tunaweza kuwasaidia vijana wetu na hatimaye kuondokana na tatizo sugu la uhaba wa ajira.
Niwapongeze sana mliomaliza chuo mwaka huu na niwatahadharishe sana wale mnaotegemea kumaliza chuo miaka ya mbeleni, huku mtaani hakuna boom, hakuna kozi wala sup, cha ajabu zaidi unaweza kumaliza hata miaka mitano hujaulizwa cheti au GPA, huku kuna degree ya maisha tu.

Na, Audax M. Ikwataki
0765-090379
DAR ES SALAAM
Asante
 
Kama kijana aliyemaliza darasa la saba aweza jitegemea kwa konda wa daladala machinga nk akaoa akawa na chumba chake cha kupsnga halafu mtu kamaliza degree miaka 32 bado tegemezi kwa wazazi tunachotakiwa kuhoji si ubora wa elimu yetu hali ubora wa huyo mwenye digrii.Kama pamoja na digrii anaitwa kimaisha na darasa la saba
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom