Hali ya utaifa inatisha

Hali ya utaifa inatisha

Sijui wengine wanaona kile kile ninachokiona mimi. Kama ni hivyo basi inatisha kwa kuwa sijawahi kuona hali hii ikijiri katika nchi yetu pendwa tangu ninakuwa mtu mzima miaka ile ya 1960s'. Katika historia ya taifa letu siku zote watanzania tumekuwa tunaunganika katika masuala yenye maslahi ya taifa. Lakini katika miaka ya hivi karibuni tunaanza kuona baadhi ya watu wakifurahia pale nchi yetu inapokuwa imeshikwa pabaya. Kwa mfano hivi sasa kuna hili suala la ndege yetu kuzuiliwa huko Afrika Kusini. Kuna watu wanashangilia. Kuna watu walishangilia pale IMF ilipotoa takwimu zake kuhusu kukua kwa uchumi kwa kuonyesha ukuaji wa 5% tofauti na takwimu za serikali zilizoonyesha ukuaji wa 7.1%. Hata kwenye mashindano ya Afcon yaliyoisha hivi karibuni huo Cairo kuna watu walioshangilia pale tulivyofungwa na Kenya! Kwa ufupi chochote kile kinachoonyesha Tanzania inafanya vibaya kinafanya baadhi ya watu wafanye sherehe. Kwa hakika hali hii haipendezi. Nini kimetokea hadi tukafika mahali watu wanafurahi nchi yao ikishikwa pabaya? Tutafakari na tufanye kile Waingereza wanasema "soul searching". Haipendezi tukiendelea hivi kama taifa.

Ukipanda chuki Na visasi utavuna chuki na visasi. Ukipanda wema Upendo utavuna Hivo hivo.Msababishi anajulikana aliyekuja vuruga taifa La Mungu Lkn atashindwa yeye.
 
Na mbona hii waionayo ni kidogo! Acheni mtu Fulani adondoke kama hamjashangaa mnapepea bendera nusu mlingoti wengine wanasakata dansi misili ya Wajaluo.
Sio kwamba watakuwa wanafurahia kudondoka Bali wanafurahia somo kueleweka ingawa ni kwa hardway.
CCM jifunzeni maisha ya kibinadamu, hayo ya kinyama mwisho ni kilio tuu.
 
1566837386572.jpeg

Tutawapendaje CCM wakati mikutano yetu polisi wanafanya ziara na vyombo vya moto
 
Sijui wengine wanaona kile kile ninachokiona mimi. Kama ni hivyo basi inatisha kwa kuwa sijawahi kuona hali hii ikijiri katika nchi yetu pendwa tangu ninakuwa mtu mzima miaka ile ya 1960s'. Katika historia ya taifa letu siku zote watanzania tumekuwa tunaunganika katika masuala yenye maslahi ya taifa. Lakini katika miaka ya hivi karibuni tunaanza kuona baadhi ya watu wakifurahia pale nchi yetu inapokuwa imeshikwa pabaya. Kwa mfano hivi sasa kuna hili suala la ndege yetu kuzuiliwa huko Afrika Kusini. Kuna watu wanashangilia. Kuna watu walishangilia pale IMF ilipotoa takwimu zake kuhusu kukua kwa uchumi kwa kuonyesha ukuaji wa 5% tofauti na takwimu za serikali zilizoonyesha ukuaji wa 7.1%. Hata kwenye mashindano ya Afcon yaliyoisha hivi karibuni huo Cairo kuna watu walioshangilia pale tulivyofungwa na Kenya! Kwa ufupi chochote kile kinachoonyesha Tanzania inafanya vibaya kinafanya baadhi ya watu wafanye sherehe. Kwa hakika hali hii haipendezi. Nini kimetokea hadi tukafika mahali watu wanafurahi nchi yao ikishikwa pabaya? Tutafakari na tufanye kile Waingereza wanasema "soul searching". Haipendezi tukiendelea hivi kama taifa.
Why don't you ask yourself WHY!???

Jiulize WHY!?

Ukipata majibu Rudi.
 
Serikali inafanya kosa dogo sana la kuunganisha na kutuaminisha kila jambo limefanywa na CCM sio serikali tena au kodi za wananchi.
Sijui wengine wanaona kile kile ninachokiona mimi. Kama ni hivyo basi inatisha kwa kuwa sijawahi kuona hali hii ikijiri katika nchi yetu pendwa tangu ninakuwa mtu mzima miaka ile ya 1960s'. Katika historia ya taifa letu siku zote watanzania tumekuwa tunaunganika katika masuala yenye maslahi ya taifa. Lakini katika miaka ya hivi karibuni tunaanza kuona baadhi ya watu wakifurahia pale nchi yetu inapokuwa imeshikwa pabaya. Kwa mfano hivi sasa kuna hili suala la ndege yetu kuzuiliwa huko Afrika Kusini. Kuna watu wanashangilia. Kuna watu walishangilia pale IMF ilipotoa takwimu zake kuhusu kukua kwa uchumi kwa kuonyesha ukuaji wa 5% tofauti na takwimu za serikali zilizoonyesha ukuaji wa 7.1%. Hata kwenye mashindano ya Afcon yaliyoisha hivi karibuni huo Cairo kuna watu walioshangilia pale tulivyofungwa na Kenya! Kwa ufupi chochote kile kinachoonyesha Tanzania inafanya vibaya kinafanya baadhi ya watu wafanye sherehe. Kwa hakika hali hii haipendezi. Nini kimetokea hadi tukafika mahali watu wanafurahi nchi yao ikishikwa pabaya? Tutafakari na tufanye kile Waingereza wanasema "soul searching". Haipendezi tukiendelea hivi kama taifa.
 
Ukipanda chuki Na visasi utavuna chuki na visasi. Ukipanda wema Upendo utavuna Hivo hivo.Msababishi anajulikana aliyekuja vuruga taifa La Mungu Lkn atashindwa yeye.
Hebu jiulize swala LA ubomoaji Kimara! Kweli unaharibia maisha ya watu (nasikia wengine walikufa kwa mashinikizo) bila fidia kwa vile hawakukupa kura kwa wingi lakini wenzao was Mwanza unasema usisikie wamebomolewa maana walikupa kura! Tena unatamka kwa matambo!
 
Kuna usemi unasema... muda siku zote huongea...

Watu wanamanung'unika mengi sana lakini hawasikilizwi, badala yake wanapotea au kupotezwa, wanazibwa midomo...

Mjumbe hauwawi...

Cc: mahondaw
 
Kwa hakika hali hii haipendezi. Nini kimetokea hadi tukafika mahali watu wanafurahi nchi yao ikishikwa pabaya? Tutafakari na tufanye kile Waingereza wanasema "soul searching". Haipendezi tukiendelea hivi kama taifa.

Hawajali..........

Na ndiyo maana walitaka kumuua Lissu mchana kweupe..............Kwasababu hawajali tena......
 
Yani saa hii akitokea mtu au kikundi kinataka fanya Jambo watanzania wengi sn watakiunga mkono.Ndo tumefikishwa hapo.

Kuua,kufokea,kukandamiza,kupokonya watu haki zao,kubambikiza kesi ndo kumetufikisha hapa.Na bado

RIP Alphonse mawazo,Akwelina
Where is Azory,Ben saanane
 
Hebu jiulize swala LA ubomoaji Kimara! Kweli unaharibia maisha ya watu (nasikia wengine walikufa kwa mashinikizo) bila fidia kwa vile hawakukupa kura kwa wingi lakini wenzao was Mwanza unasema usisikie wamebomolewa maana walikupa kura! Tena unatamka kwa matambo!

Vyote uondoa Upendo.Zipo taratibu za kuhamisha watu na zipo taratibu za kuhamisha wanyama. Au ukosefu wa utu hata shetani hawezi anashangaa hawa magaidi wasiojulikana wanawateka watu wanawatesa,wanawalawiti kisha wanauwa ndugu zetu,ni kiwango cha juu sana cha ukatili hata Hitler akufanya hivo.
 
Haya yote yanasababishwa na MTU mmoja tu kujifanya anajua kila kitu na kutesa watu,fikilia mtu kama lisu kapigwa risasi mchana kweupe,ila yeye hataki hata watuwaende kumuona,bado yuko kwenye matibabu unamdhulum ubunge, Leo wanatutaka tuwe wazalendo hicho ni kitu kisichowezekana
 
Vyote uondoa Upendo.Zipo taratibu za kuhamisha watu na zipo taratibu za kuhamisha wanyama. Au ukosefu wa utu hata shetani hawezi anashangaa hawa magaidi wasiojulikana wanawateka watu wanawatesa,wanawalawiti kisha wanauwa ndugu zetu,ni kiwango cha juu sana cha ukatili hata Hitler akufanya hivo.
Hili suala la kulawiti watu sasa hivi linazungumzwa sana kuwa agents was serikali hiyo ni njia moja wapo ya utesaji, lakini bado ushahidi. Lakini wiki hii mhariri wa Watetezi TV alikamatwa kwa kuandika habari za Polisi huko Njombe kuwalazimisha watuhumiwa kulawitiana, jee hapo ndio tumefika kama nchi?
Jee wapenzi wa CCM wanaweza kweli kuitetea serikalu yao inayowalawiti watu? Jee ndugu zao wakiwa mikononi mwa Polisi watafurahi wakilawitiwa?
CCM imejaa laana!
 
Sijui wengine wanaona kile kile ninachokiona mimi. Kama ni hivyo basi inatisha kwa kuwa sijawahi kuona hali hii ikijiri katika nchi yetu pendwa tangu ninakuwa mtu mzima miaka ile ya 1960s'. Katika historia ya taifa letu siku zote watanzania tumekuwa tunaunganika katika masuala yenye maslahi ya taifa. Lakini katika miaka ya hivi karibuni tunaanza kuona baadhi ya watu wakifurahia pale nchi yetu inapokuwa imeshikwa pabaya. Kwa mfano hivi sasa kuna hili suala la ndege yetu kuzuiliwa huko Afrika Kusini. Kuna watu wanashangilia. Kuna watu walishangilia pale IMF ilipotoa takwimu zake kuhusu kukua kwa uchumi kwa kuonyesha ukuaji wa 5% tofauti na takwimu za serikali zilizoonyesha ukuaji wa 7.1%. Hata kwenye mashindano ya Afcon yaliyoisha hivi karibuni huo Cairo kuna watu walioshangilia pale tulivyofungwa na Kenya! Kwa ufupi chochote kile kinachoonyesha Tanzania inafanya vibaya kinafanya baadhi ya watu wafanye sherehe. Kwa hakika hali hii haipendezi. Nini kimetokea hadi tukafika mahali watu wanafurahi nchi yao ikishikwa pabaya? Tutafakari na tufanye kile Waingereza wanasema "soul searching". Haipendezi tukiendelea hivi kama taifa.
Katika Fizikia, moja ya sheria za msingi kabisa ya ulimwengu ni "The Second Law of Thermodynamics".

Mwanasayansi maarufu wa Uingereza, Sir Arthur Eddington, ananukuliwa akisema, cheza na sheria zote za Fizikia, lakini ukiona majaribio yako yanapingana na The Second Law of Thermodynamics, fanyia kazi upya majaribio yako.

Hii sheria inasemaje?

Kifupi, kwa lugha isiyo ya kitaalamu sana, sheria hii inasema kwamba, kadiri muda unavyozidi kwenda mbele, katika closed systems zozote, mambo kwa kawaida huwa yanatoka kuwa simple kwenda complicated, entropy inaongezeka. Yani hata ukisema ufunge mlango wa chumba ukiache kiwe kisafi, ukakaa miaka miwili, utakuta chumba kina vumbi, kinahitaji kufagiliwa ili kiwe kisafi. Unaweza kukuta utando wa buibui.

Kwa hivyo, ili kukifanya chumba kiwe kisafi, inabidi kazi ifanyike kila mara kukisafisha. Ukisema tu "nilifagia wiki iliyopita, chumba changu safi" wakati watu wanaingia na kutoka, utajikuta una chumba kichafu.

Kwa nini naongelea "The Second Law of Thermodynamics" na habari za entropy na usafi wa chumba hapa?

Tuna tatizo la kufikiri kwamba kazi ya kujenga umoja wa kitaifa ilishamalizwa enzi za Nyerere. Sisi ni wamoja.

Nyerere mwenyewe katika uhai wake mwishoni alilalamikia kuchipuka kwa ukabila, akielewa kwamba kazi aliyoanza haikuisha. Na kwa kweli kazi hii haiishi. Ni sawa na kazi ya kufagia chumba niliyosema awali hapo. Ni kazi endelevu kizazi hata kizazi. Ukifikiri umemaliza hapo hapo ulichojenga kinaanza kuanguka.

Sasa basi, katika muktadha huu, watu wanapoona viongozi hawaishi kama wananchi wengine, wanapoona upendeleo, wanapoona hakuna ushirikishwaji umma katika maamuzi, wanaona hizi habari za umoja wa kitaifa ni ujinga. Wanaona sisi ni watumwa katika nchi yetu wenyewe, tunawatumikia mabwana wachache wanaofaidi matunda ya nchi hii kivulini, wakati sisi tunapigwa na jua.

Wengine wakiumwa wanapelekwa Ulaya, India na South Africa. Wengine hata hospitali za Wilaya hawamudu matibabu.

Sasa katika mfumo huu, utategemea vipi umoja wa kitaifa na uzalendo?
 
Back
Top Bottom