Hali ya utaifa inatisha

mafutamingi

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
2,772
2,171
Sijui wengine wanaona kile kile ninachokiona mimi. Kama ni hivyo basi inatisha kwa kuwa sijawahi kuona hali hii ikijiri katika nchi yetu pendwa tangu ninakuwa mtu mzima miaka ile ya 1960s'.

Katika historia ya taifa letu siku zote watanzania tumekuwa tunaunganika katika masuala yenye maslahi ya taifa. Lakini katika miaka ya hivi karibuni tunaanza kuona baadhi ya watu wakifurahia pale nchi yetu inapokuwa imeshikwa pabaya.

Kwa mfano hivi sasa kuna hili suala la ndege yetu kuzuiliwa huko Afrika Kusini. Kuna watu wanashangilia. Kuna watu walishangilia pale IMF ilipotoa takwimu zake kuhusu kukua kwa uchumi kwa kuonyesha ukuaji wa 5% tofauti na takwimu za serikali zilizoonyesha ukuaji wa 7.1%.

Hata kwenye mashindano ya Afcon yaliyoisha hivi karibuni huo Cairo kuna watu walioshangilia pale tulivyofungwa na Kenya!

Kwa ufupi chochote kile kinachoonyesha Tanzania inafanya vibaya kinafanya baadhi ya watu wafanye sherehe. Kwa hakika hali hii haipendezi.

Nini kimetokea hadi tukafika mahali watu wanafurahi nchi yao ikishikwa pabaya? Tutafakari na tufanye kile Waingereza wanasema "soul searching". Haipendezi tukiendelea hivi kama taifa.
 
Mbona wakati Tundu Lissu kapigwa risasi, Azory kupotea, Ben Saanane n.k n.k hamkutuunga mkono tulivyokuwa tunalia kuulizia wapo wapi? ya kwenu mnataka tuwaunge mkono, ya kwetu ya utaifa hamuyaoni eheee
emoji26.png
emoji26.png
emoji26.png
 
..kuna waTz wanajiita wazalendo wanafurahia na kusherehekeakea wakiona wenzao wakitekwa, wakiteswa, wakibambikiwa kesi za hovyo-hovyo, na hata wakipigwa risasi.
La kusikitisha ni kwamba hao "wazalendo" hawayaoni hayo. Na wala hawataki kujiuliza kwa nini hali iwe hivi!

Wanachokijua wao ni kwamba watu wakitiwa hofu na woga mwingi wataacha kuhoji lolote walitendalo, hapo watakuwa wamefanikiwa sana kujenga 'uzalendo' wanaoutaka, na Tanzania itaendelea kwa haraka sana.
 
Inatisha sana, Watu wanatekwa na wanapotea alafu kiongozi mwenye dhamana badala ya kueleza mambo ya msingi analeta mipasho.

Alafu wanahubiri Uzalendo,hivi wanafikiri Watanzania hawasikii au kuona yanayoendelea nchini.
Tunayaona sana Mkuu. Wao wanashangilia na kutubeza pale mmoja wao anapotuumiza. Lkn wao wakiguswa tu kidogo basi hukimbilia suala la Uzalendo.
Uzalendo kwa sasa ni ndoto. Utarudi pale awamu ya tano itakapomaliza muda wake wa uonevu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom