Hali ya Tanzania na Rwanda si Shwari-Benard Membe

Hali ya Tanzania na Rwanda si Shwari-Benard Membe

mleta mada msio mtz angalia jina Amavubi its tutsi name wabongo mnakulupuka tu kuchangia huu mtego tu wa kagame

uko makini kupita maelezo, lkn unajua maana ya Amavubi? nimecheka saana
 
hatu muongee vipi DRC tumewachapa m23 vijana wenu na FDLR hatuwapigi kamwe nani awasaidie kupiga adui zenu hiyo kitu haipo FDLR ni salama ktk mikono ya TZ

njoo nikupe darasa la uhakika ili baadae uwe na mukatdha
 
swadaktaaaaaaaaaaaa
Diplomatic huandaliwa na mara nyingi huwa wana lugha zao! I wish angeweza kudesa kwa yule Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov !! " Diplomat huwa hawana sifa za uropokaji, huwa wanaongea kwa utaratibu maalum wakati huo huo wanakuwa wamebeba missiles !!! Membe hafai kuwa Foreign Ministers iliyosheheni wanadiplomasia wa hali ya juu Duniani... BTW tunajua kuwa Kagame alikuwa anaiba kwa niaba ya wananchi wake! Sisi tunalinda kwaniaba ya wananchi wa Magharibi!!! Tusifumbe macho tukijifanya hatuoni kuwa kwa nyakati tofauti Uganda na Rwanda zilikuwa Western Darling na walikuwa wanatumiwa kukwapua madini ya Congo? Wao walipo anza kujigawia ndo mzozo ukaanza na sasa majumu yote tumepewa sisi wenye kupiga deal kwenye mishahara ya wapiganaji wetu... Africa tunatia aibu sana ...JK anatakiwa aanze kazi ya kumfunda Membe Udiplomasia ...
 
tuwekee jamvini mkuu
mimi nadhani wengi wetu humu, hatuna access ya yale yote yanayoendelea hivyo judgement zetu zinakuwa based na personal feelings tu, nadhani ni vyema tukaachia mambo mengine nyeti kwa wale tuliowaamini kutuongoza, sidhani kama viongozi wetu wanataka sana vita au wanahamu saana ya ugomvi, nature yetu sio migogoro hivyo sikubaliani na mitazamo ya wengi kwamba huu mgogoro umekaa kibinafsi zaidi ya national interest, naamini kabisa kuna mambo ambayo si sawa yanayoendelea ambayo wengi wetu hatuyafahamu hivyo, tuwe wazalendo kwa kuwasupport viongozi wetu, hawa ambao wapo karibu na vyombo vyetu vya usalama na wanajua yanayoendelea kuliko wengi wetu tunaotoa maoni kwa hisia
 
We nani kakwambia m23 wameondoka congo, unajua kuna vikundi vingapi vipo congo east vya waasi, kuweni wazalendo
 
Issue ni swala hili lilivyobebwa ovyo kidiplomasia......huwezi kuituhumu nchi jirani direct hivyo bila kuibua mgogoro......Kazi iliyotupeleka Congo inafahamika......maneno yale bungeni ya nini? Kama UN inahakika na report yake (hata mimi naamini Rwanda inahusika) kwanini hadi leo hawajaiadhibu Rwanda? Tumekosa lugha ya kidiplomasia kweli?

watu wengi mnabadilisha ishu hapa. Membe hakuingia bungeni akaanza kusema M23 ni Rwanda, WENJE ndie aliyesema kuwa M23 si Rwanda, Membe akaweka record straight kuwa M23 ni Rwanda, according to the UN report, ambayo ndio msimamo wa Tanzania.
vinginevyo wewe lete nchi moja tu besides Uganda, ambayo inapinga hii ripoti ya UN inayosema M23 sio wanyarwanda. Hivi unadhani leo bunge la kenya akiibuka mbunge akasema M23 sio Rwanda, unadhani waziri wa nje wa kenya atakubali "kidiplomasia"? la, lazima atasema ukweli tu.
 
Mbona enzi ya Mkapa hatukuwa na matatizo na Rwanda? Huu ni mgogoro binafsi wa huyu mkweree aliyeshindwa kuikwamua nchi yake kiuchumi/ pia ameshindwa kuipatia nchi katiba waitakayo wananchi na hivyo sasa anataka kudivert attenetion ya watu kwa mambo yasiyokuwa na tija kwa nchi!!

tulipoweka mazungumzo arusha kati ya MUASI KAGAME na wauaji wake wa RPA mbona hukuona tatizo? tatizo lije leo TUNAPOSHAURI mazungumzo kati ya RAIS KAGAME na waasi ambao juzi 94 ilikuwa kinyume chake, kagame alikuwa muasi na waasi walikuwa serikali?
 
mbona wachonganishi kama
news of rwanda na rwanda time hamyataji acheni ujinga wenu asa sie
tutukanwe afu tukae kimya

mkuu haya nayo unaita magazeti haya hata kuku rwanda ikitaga yanaandika ni maendeleo
 
tuwaogope rwanda, wanatisha wale jamaa, wana akili sana

cha ajabu wanaishi maporini TZ kama wakimbizi haramu, akili zao kwa nini haziwapi amani kila siku kuchinjana tu.
 
tulipoweka mazungumzo arusha kati ya MUASI KAGAME na wauaji wake wa RPA mbona hukuona tatizo? tatizo lije leo TUNAPOSHAURI mazungumzo kati ya RAIS KAGAME na waasi ambao juzi 94 ilikuwa kinyume chake, kagame alikuwa muasi na waasi walikuwa serikali?

Context ya mazungumzo yale ya Arusha ni tofauti kabisa na ya sasa kwani wakati ule ilikuwa kabla ya mauaji ya kimbali kutokea!!! Athali za genocide kwa waathirika sio rahisi kuzisahau kihivyo na kumbuka itikadi ya hao mnaotaka Kagame azungumze nao ni kuexterminate watusi wote duniani!! Ni mjinga tu anayeweza kukaa meza moja ili hali akijua aliyekaa naye nia yake ni kumuangamiza!!
 
Atasemaje ni wachonganishi wanasababisha mgogoro kati ya Tz na Rwanda na wakati hapo hapo anasisitizia kuwa Rwanda wanawaunga mkono m23?

Je sisi hatumuungi mkono Kabila? Na pia nasikia FDLR? Sasa uchonganishi unatoka wapi hapo?

Hii maneno tuiachie serikali. Hata Wenje ni mchonganishi.
 
Context ya mazungumzo yale ya Arusha ni tofauti kabisa na ya sasa kwani wakati ule ilikuwa kabla ya mauaji ya kimbali kutokea!!! Athali za genocide kwa waathirika sio rahisi kuzisahau kihivyo na kumbuka itikadi ya hao mnaotaka Kagame azungumze nao ni kuexterminate watusi wote duniani!! Ni mjinga tu anayeweza kukaa meza moja ili hali akijua aliyekaa naye nia yake ni kumuangamiza!!

hayo mauaji ya kimbari nani mwenye uhalali wa kuyazungumzia? sio kagame wala serikali ya habyarimana, maana hao wote walikuwa wahusika, bali international community.
international community mpaka leo haijui kabila gani liliuawawa zaidi kati ya watu zaidi millioni 1, na hivyo mauaji ya Rwanda yanakuwa referred as "Rwandan genocide" kwa kutambua kuwa waliuana wote wahutu na watutsi.
Kagame amegeuza hilo mwaka 2004 miaka 10 baadae kuwa "genocide against tutsis"! lakini dunia nzima including kikwete tunajua ukweli wa complexities za mauaji yale, ndio maana hutapata kiongozi yoyote yule nchi yoyote anayempinga kikwete kwa ushauri ule.
Hayo mengine kwa nini uchukue toka kwa kagame, when did FDLR say they want to exterminate all tutsis? hizo ni propaganda za kipuuzi za kagame. Rwanda majority ni wahutu, na wahutu hao hao FDLR ambao walikuwa serikali tayari walishakubali mkataba wa maridhiano wa Arusha. Kama wahutu wangetaka ku-exterminate all tutsis si wangefanya hivyo toka walivyopindua nchi 1958? tena wakati huo 1958 wahutu walikuwa extremists kweli kweli.
Leo hii FdLR wenyewe wako tayari kwa mazungumzo na kagame, lakini kagame si tu kuwa hataki bali bado anaendelea kuwaua DRC kwa kutumia proxy armies.
 
Hii maneno tuiachie serikali. Hata Wenje ni mchonganishi.
Fafanua uchonganishi wa Wenje ulipo.

Serikali Iachiwe mara ngapi, kwani haijapeleka wapiganaji kupambana huko DRC dhidinya m23? Sioni uchonganishii wowote, labda ndiyo uonyeshe huo uchonganishi ulipo na wengine tuone.
 
Fafanua uchonganishi wa Wenje ulipo.

Serikali Iachiwe mara ngapi, kwani haijapeleka wapiganaji kupambana huko DRC dhidinya m23? Sioni uchonganishii wowote, labda ndiyo uonyeshe huo uchonganishi ulipo na wengine tuone.

Mkuu Tanzania haikujipeleka yenyewe iliombwa na UN na haikombwa yenyewe uliona akina Malawi na SA wakiwemo. Baada ya serikali kukubali kupeleka majeshi huko hatupaswi kuanza kuilaumu serikali wakati huu. wabunge kama walikuwa hawataki wasingesubiri hdi leo wangelizuia majeshi kabla ya kuondoka kwenye ardhi ya tanzania. kuanza kuilaumu serikali hadharani ni kuichochea serikali ya Rwanda izidi kuichukia tanzania.
 
Kwanza,Nampongeza Waziri Wa Mambo ya Nje Bernard Membe kwa kukubali kuwa kuna haja ya kuwa na wataalamu wa uchumi kwenye Balozi zetu nje ambao wamebobea katika Diplomasia ya Uchumi .Hili suala nimeshaandika hapa mara kadhaa,nimeaandika JF na Pia makala kwenye magazeti.Ni hatua nzuri sasa kama Wizara imetambua umuhimu wa kutumia Balozi Zetu kuvutia watalii ,kuhamasisha Biashara kati ya Watanzania na watu au makampuni ya Nje na pia kuvutia wawekezaji (Foreign Direct Investment).Sasa tumeanza kwenda na wakati ingawa tunahitahi Sera yenye strategic focus kwa EAC,SADCC,AU,ARAB LEAGUE,ASIA,CHINA ,US n.k kama Potential Partners. Uingereza,Kenya,SA,China na US ni strategic partbers katika Uwekezaji.Hapa ni lazima tufanye formulation ya Unique Policy ili hata wanadiplomasia wetu waongozwe na Framework Specific

Pia Economic Intelligence Unit au Think Tank iundwe na iwe na Coordination ya Moja kwa Moja na Department ya Economic Diplomacy.kwa bahati mbaya Wabunge hawakumbana katika Eneo hili.Diplomasia ya sasa ni ya Uchumi na sio Diplomasia ya Kisiasa tena. Leo tunatuma wanasiasa wakatuwakilishe kule Doha kwenye Mikutano ya WTO wakati Wenzetu wanapeleka mabingwa mbinu za majadiliano ya kibiashara na Uchumi kutoka kwenye Economic Intelligence Unit zao

Pili,jana nilitahadharisha juu ya matamshi ya Mbunge Kessy kuhusu yeye kuituhumu Rwanda na nikasema alikosa weledi unaohitajika katika majadiliano ya mijadala ya kidiplomasia ndani ya bunge na nikaonyesha masikitiko yangu kwa Mhe.Bernard Membe kushangilia kauli ya Mhe.Kessy kuwa Rwanda inaiba Raslimali za Congo-DRC na pia inafadhili M-23.

Well,Nilisema Kessy ametuhumu (Hata kama ni Kweli) bila kufanya Rejea .Nikasema labda Membe aje afanye Rejea ya Ripoti ya UN lakini nikatahadharisha kuwa hata akifanya hivyo lakini Rwanda hajaadhibiwa.

Kweli Mhe.Membe alikuja kumsaidia Kessy kwa kufanya Rejea ya Ripoti ya UN na kutumia flirtiring Skills akidhani kuwa anamshambulia msemaji wa kambi ya upinzani.

Membe alichofanya ni makosa makubwa kidiplomasia na hili litachochea mgogoro mkubwa na Rwanda.

Je,Kauli alizotoa Kessy au Membe kuwa Rwanda ni Wezi na M-23 ni kundi la Serikali ya Rwanda,Rais Kikwete anaweza kuzitamka kwenye Mkutano wa EAC,SADCC,ICGLR,AU Au Kule UN General Asswmbly? Waziri mkuu Pinda aliyelitangazia Bunge Mwaka jana kuwa Serikali imemuomba Rais Museveni wa Uganda awapatanishe Kikwete na Kagame alimaanisha nini?Kwamba Rais angefuta kauli yake ya kumshauri Kagame kuongea na FDLR?Vipi mbona Ripoti aliyoinukuu Membe Bungeni pia imeituhumu Uganda kuwa wanashirikiana na Rwanda kulifadhili Kundi la March-23 Movement(M-23)? Siis wengine tulipinga tangu Mwanzo Uganda kuhusishwa maana kama ni confidence ya Mediator sidhani kama Tanzania ingekua nayo kwa Museveni na tena ningeshangaa sana.

Tanzania tumeonyesha kutokua na ajenda kimataifa na nimeshasema mara nyingi tunafuata sera ya fuata mkumbo (Bandwagoning Diplomacy).Tupo tupo tu na tunadandia kila kitu halafu tunasema tunaheshimika sana kimataifa?

Hiyo nguvu ya usuluhishi unaitoa wapi wakati huu wa sera ya Diplomasia ya Uchumi ambako nguvu ya uchumi na kijeshi ndiyo inayokupa nguvu katika medani za kimataifa ikiwepo usuluhishi? Marekani wakisema Usalama wanamaanisha nguvu ya kiuchumi. Nigeria baada ya Rebasing ya uchumi wao imekua taifa lenye uchumi mkubwa Afrika na hivyo nguvu ya taifa na sauti yao itaheshimika

Kenya wanatupita katika nguvu na sauti kimataifa katika ukanda huu kwa sababu ya nguvu ya kiuchumi na sisi tunaendelea kutumia ile akiba ya Diplomasia ya siasa za Frontline aliyoacha Mwalimu Nyerere

Sasa Ripoti ya Mhe.Membe iliyoandikwa na UN Expert Group ilipingwa na Rwanda,pia Ripoti hiyo ilipingwa na Uganda maana hata Uganda walituhumiwa lakini Membe kwa upotoshaji Mkubwa hakuitaja.

Ni jambo la ajabu kuwa Top Diplomat wa Nchi anashindwa kuzingatia kuwa Tayari Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilishaidhinisha Vikwazo kupitia Azimio namba 2136 (2014) ambalo liliungwa mkono na Rwanda kwa mtazamo wa kuwa Azimio namba 1533(2004) lilotanguliwa na Azimio 1494(2003) linaheshimiwa

Azimio namba 2136 liliweka Vikwazo kwa M-23(Bila kuitaja Rwanda katika Adhabu hiyo) na pia Congo -DRC waliadhibiwa kwa kuifadhili UFDLR ambayo pia ilitajwa na UN report aliyoitumia Membe

FDLR wana extrime Ideology iliyohusika na Mauaji ya Kimbari ya Rwanda na ilithibitishwa na UN Security Council.

Haya Membe hakuyajadili wakati Bunge lilihitaji mjadala ili nchi yetu iangalie namna ya kuwasaidia majirani zetu,pia tudumishe amani,mahusiano ya kidiplomasia hasa ya kiuchumi na pia kulinda mtazamo mpana wa umajumui wa Afrika

Membe alichagua Kufanya siasa kiduchu(Petty Politics) kumshambulia Wenje binafsi(Personal Attack) kinyume na weledi wa Diplomasia na pia kutoa matamshi yatakayochochea mgogoro zaidi baina ya Tanzania na Rwanda kwa kuituhumu Rwanda kuifadhili M-23 huku akijua kwa sasa kulingana na azimio 2136 Nchi wanachama wa ICGLR(Nchi za Ukanda Maziwa Makuu) zina jukumu la jumla na binafsi katika kusaidia kutekeleza maazimio hayo ikiwa ni pamoja na kushirikiana na UN Expert Group iliyopewa Mandate ya kurefusha Sanction Regime hadi February 1,2015 ili kuleta amani ya Kudumu

Waziri wa Mambo ya Nje kupotosha mjadala na kutuhumu kuwa Msemaji wa Kambi ya Upinzani anatumiwa na Mataifa ya Nje (Pengine Rwanda) ni udhaifu mkubwa katika kukwepa hoja .Kama kuhoji kuhusu tuhuma za Rais Kukutana na Kiongozi wa Waasi(Tena Sio Upinzani) basi inamfanya Wenje kuwa Mamluki anayelipwa na Rwanda kuisemea ndani ya bunge ,Je ni wapi Duniani tuliwahi kuona Rais Wa Nchi kulisemea na kulionea huruma kundi la Waasi? Membe hakupima Kauli zake

Ni mwaka jana tu Membe alitoa matamshi tata kuhusu kutengwa kwetu kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki na kudai "tunasubiri Talaka".Tuliipinga kauli hii na kwa bahati nzuri Rais Kikwete aliliona hilo na akatoa hotuba nzito Bungeni kuwa hatuendi Popote.

Mimi ni mzalendo ninayelipenda Taifa langu na nitalipigania popote duniani.Sipendi Blind Patriotism.

Kagame ana matatizo yake ndani ya Rwanda lakini hatuwezi kuruhusu kauli aliyoitoa JK kuwa Rwanda Iongee na Waasi(Kauli ambayo nikiiunga mkono na naendelea kuiunga mkono) itumike kuhatarisha mahusiano yetu na watu wa Rwanda au Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kauli za Mawaziri ambazo wanazitoa bila kipimo

Pia suala la Majeshi yetu kule Congo DRC lipo na ni sehemu ya Tanzania katika kutimiza majukumu yake ya kimataifa(International Obligation) kupitia Azimio no.2098 la kuunda MONUSCO.

Hata hivyo halizuii mijadala bungeni maana hata Obama aliposema "Dumb War" ilikua ni matokeo ya mjadala ndani ya Congress kule US kuhusu Rais Bush kulidanganya Taifa kuwa Iraq ina silaha za Kemikali kumbe ni Uongo.Marekani ilipata hasara.

Ni lazima kuwe na mjadala bungeni kwa kukosoana na kurekebishana ili tuunde mwafaka wa kisera kama nchi tusonge mbele.Waziri alikosa weledi juu ya matumizi ya Code Words and Politeness

Unachagua kujadili millitary adventure huko DRC halafu unashindwa kutoa majibu ya kushindwa kwa Serikali kutuma Millitary Plane kufanya Evacuation hata ya Raia wetu kule Sudan Kusini wakati wa Vita? Kwanza nampongeza Membe kwa kukubaliana na ile Hoja yangu ya jana kuwa Tanzania imezubaa na wizara haina takwimu ya idadi ya Raia wa Tanzania nje hivyo hata mikakati ya kunufaika na Diaspora ni lazima tutatue changamoto hii kwanza

Tatu,Membe Alishangaza kwa kutetea ziara za Rais nje .Rais amefanya ziara zaidi ya 365 nje ya nchi kushinda Mwalimu Nyerere ambaye hakufikisha ziara 70 kwa kipindi chake cha miaka 24 madarakani.Rais anataka kuwa Member wa Diaspora?Maana ameshinda angani na nje ya nchi kwa sababu dhaifu kabisa kabisa.

Membe anatoa sababu dhaifu kuwa Rais anapendwa na kuheahimika,Je kati ya Rais Kikwete na Mwl.Nyerere ni nani alikua akiheshimika zaidi kimataifa?

Rais anashindwa kubaki nyumbani na kudhibiti wizi wa mali za umma kama bilioni 200 za ESCROW kwenye sakata la IPTL badala yake anaenda kuomba bilioni 40 au 100 nje ya nchi tena sehemu nyingine kama Singapore anapokelewa na mkurugenzi wa Idara kinyume na Itifaki kabisa?

You can't defend the trip maniac president in that way

Ifike Mahali sasa kwenye Katiba tudhibiti ziara hizi kama Mexico ambako Rais Vicente Fox alionja fedheha hii kwa kuzuiwa na Bunge lake la Senate mara Mbili Kusafiri ikiwepo ziara yake US na Canada.Safari za Rais ilikua ni lazima zipate approval ya Bunge. Chama cha Upinzani cha PRI kilizuia safari zisizokua na Tija.

Mexico walipata dawa ya kudhibiti Marais ambao ni wazururaji utadhani wamelelewa kwa supu za usafiri(Makanyagio) ya kuku wa kienyeji. Balozi za nje na hata wizara zinaweza kufanya baadhi ya safari na kupunguza gharama.

Hatuwezi kuegemea kwenye ziara za Rais katika Diplomasia ya Kuomba na Kushukuru badala ya kuweka Diplomasia ya Uchumi.Tunahitaji kudhibiti ziara za Rais kikatiba kabisa na safari zipate Approval ya Bunge kama Mexico. How can we justifty global trotting to seek aid and loans while we cant protect our Cash reserves?
 
Mkuu Tanzania haikujipeleka yenyewe iliombwa na UN na haikombwa yenyewe uliona akina Malawi na SA wakiwemo. Baada ya serikali kukubali kupeleka majeshi huko hatupaswi kuanza kuilaumu serikali wakati huu. wabunge kama walikuwa hawataki wasingesubiri hdi leo wangelizuia majeshi kabla ya kuondoka kwenye ardhi ya tanzania. kuanza kuilaumu serikali hadharani ni kuichochea serikali ya Rwanda izidi kuichukia tanzania.
Yani sisi kupeleka majeshi huko Congo kusiwachukize, halafu maneno ya Wenje ndo yasababishe watuchukie zaidi!?Mawazo gani hayo mkuu?

Labda kama angesema kuwa yamechochea mgogoro or something else(jambo ambalo Membe yeye ndo kalifanya).Lakini kusema ni uchonganishi, hilo halileti mantiki.

Mchonganish hapo(kama anatafuta scape goat), labda wangekuwa UN walio omba majeshi kutoka kwetu.
 
Back
Top Bottom