Hali ya Hospitali ya Taifa Muhimbili

Wanatuibia mabilioni kwenye rasilimali zetu na makusanyo ya kodi. Kwa mwaka mmoja tu 2005/2006 pale BOT wamekwapua billioni 288 na hapa hatujaweka wizi wa rasilimali zetu dhahabu, Almasi, Tanzanet n.k. kutokana na mikataba isiyo na maslahi kwa Watanzania . Fikiria kama mapesa yote hayo yangeelekezwa katika kuboresha mahospitali yetu basi hata mafisadi wasingezikimbia hospitali zetu
Mkulu Bubu ataka kusema, mimi nilitoa hoja siku moja na nadhani kama JF wataifutilia itakuwa ni hoja yenye nguvu sana. Niliomba sana wakulu wenye kujua hesabu kamili kuhusu kila pahala ccm wanapoiba pesa washushe dataz hapa JF, tutaenda na moja baada ya nyingine na kuzifanyia kazi inayotakiwa, tukifanikiwa hata kwa 50% nakupeni hakika ccm itakuwa matatani. Sasa hawana wasiwasi sana maana wanajua pesa ipo na wakitaka kufanya lolote wana imani linawezekana...pesa bwana. La msingi sisi tuchimbe sources zao za hela, tukizipata TUZIZIBE, KWISHA. Naomba hii iwe kipaumbele hapa JF kama akili zangu zitakuwa zimenielekeza vyema wakulu, tukilifanyia kazi nadhani yaweza kupunguza muda wetu. Faida zake kubwa ni mbili; 1. Kwanza tutawakosesha nguvu ccm na viongozi watashika adabu maana wasiwasi wao utaongezeka. 2. Automatically hizo fedha zitakwenda maeneo mengine muhimu kutoa huduma kama huko tunakoona panakosa huduma kila siku. Ama wapewe basi hata wale wazee wetu ambao walikuwa pale ikulu jana wakisubiri JK aseme kama ameamua kuwasanii jumla waelewe moja maana inaonekana kizazi cha wanaodai malipo ya EAC kitakwisha chote kabla hawajalipwa. Warithi hawana nguvu kama wahusika kwahiyo nguvu zinapungua siku hadi siku wanavyokufa wale wahusika kamili, hadi wafe wote.
 
kama nimeangalia vizuri hizi picha ninachoona mimi ni ufinyu wa nafasi wagonjwa wamelala kwenye corridor na magodoro ,inamaanisha kwamba wagonjwa ni wengi mno na nafasi ya hakuna,nadhani pamoja na huo ufisadi/sihasa- tukiri kuwa hospitali yetu ya rufaa ni ndogo mno kuweza kukidhi idadi ya wagonjwa wanaotoka mikoani na wilayani hapahapa dar, inatakiwa iongezwe au ziwe idara tofauti sehemu tofauti,kama sikosei nilisoma mahali kwamba wanataka kupanua hospitali ya rufaa
 
kama nimeangalia vizuri hizi picha ninachoona mimi ni ufinyu wa nafasi wagonjwa wamelala kwenye corridor na magodoro ,inamaanisha kwamba wagonjwa ni wengi mno na nafasi ya hakuna,nadhani pamoja na huo ufisadi/sihasa- tukiri kuwa hospitali yetu ya rufaa ni ndogo mno kuweza kukidhi idadi ya wagonjwa wanaotoka mikoani na wilayani hapahapa dar, inatakiwa iongezwe au ziwe idara tofauti sehemu tofauti,kama sikosei nilisoma mahali kwamba wanataka kupanua hospitali ya rufaa

Jamani! Mbona tunashindwa kuunganisha vitu simple?!

Hoja ya watu ni kuwa hela zisingeibiwa na mafisadi zingeweza kutumika kupanua na kuboresha hospitali. Au mnategemea hospitali ipanuke kwa miujiza ipi?
 
Jamani! Mbona tunashindwa kuunganisha vitu simple?!

Hoja ya watu ni kuwa hela zisingeibiwa na mafisadi zingeweza kutumika kupanua na kuboresha hospitali. Au mnategemea hospitali ipanuke kwa miujiza ipi?

Hizi bilion 300 walizochukua trip hii, ebu fikiri kama zingetupwa ktk reli ya kati ingeweza kuboresha vipi mazingira? kuanzia kunuua mabehewa mapya pamoja na kukarabati reli yenyewe,. Cha ajabu hao wasomi wetu wanaojiita wasomi hawayaoni haya, wao bado wamekumbatia kadi za ccm kwenye wareti zao, wakifikiri ni sifa, sasa hivi naaza kukubaliana na ile kauli aliyoitoa kiongozi mmoja wa africa kwa nyerere kuwa, ANATAWALA MAREHEMU, Yaani wao bora kumekucha
 
Hali Muhimbili haiwezi kutengemaa hadi serikali itakapopiga marufuku kwenda kutibiwa nje ya nchi kwa kutumia fweza za walipa kodi.
 
Serikali haina uwezo wa kujenga hospitals na kutibu wagonjwa wote,Hospitals kama muhimbili kwa kutibu wanaojifungua mpaka malaria ni waste of brain & money,hizo billions serikali inazospend Muhimbili bora zingeenda kununua insurance za watu na research,ukweli ni kwamba kama health insurance zipo watu wengi wangejenga hospitals nzuri kupita muhimbili na kusingekuwa na tatizo la vitanda na huduma mbovu.
 
Jamani kama hamta-review compensation/mishara ya serikali kiasi kwamba wakurugenzi wasihemee kwenye safari na vikosi kazi yote munayosema ni ya bure tu.... graduate anayelipwa laki 3 hawezi ku-THINK BIG wala kufikiria bistali ni chafu au inahitaji ukarabati. Lazima muda wote afikirie kutengeneza safari tu.
 
Afadhali hawa wanaolala wanajua kesho wanaamkaje
kuliko wale wauwaji pale

temeke

na

mwananyamala

kila siku wanakufa watu na awafanywi chochote wanaishia kujiundia tume kula ulaji wa marehe,u shame tanzania
 
Naomba kuuliza, tunaona rufaa nyingi za wagonjwa kutoka Hospital za Wilaya na Mikoa... hivi mumewahi kuona wagonjwa wanatolewa Muhimbili (Nationa Referal Hospital) kupelekwa hospital za chini kwa kuwa mgonjwa hakustahili kupelekwa Muhimbili? Other than special cases kama za vipindupindu?
 
Hii inaonekana Muhimbili naweza kusema kwa kizungu is the tip of an iceberg...Kuna mtu ameuliza huko Wilayani kukoje, Ni balaa. Kulala chini sio issue kama unapata huduma inayotakikana. Ila kama hakuna wauguzi, madaktari na kila mtu anapiga longo longo maisha yanakuwa magumu sana kwa wagonjwa.
Kuna jamaa mmoja alisema kama ukiamua kuumwa bongo lazma ufe...Namuunga mkono asilimia mia moja kwa sababu huduma zetu za afya ni weak kutokana na mipango dhaifu, lack of vision na kuendeleza siasa kuliko utaalamu.
Kwa mafisadi hata kama anaweza kwenda kutibiwa America kama akipata medical emergency hawezi fika hata airport so atakufa tu. Debilitated medical system ni kama zimwi linakula waliomo na wasiokuwe.
Najaga!
 
attachment.php


Baadhi ya wagonjwa wakiwa wamelala chini katika hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wodi namba 17 Sewa Haji kunakosababishwa na upungufu wa vitanda katika hospitali hiyo. (Picha na Peter Twite, Majira)

vitanda hakuna!
madawa je?
wauguzi je?



Ndio maana wakuu wanakwenda nje kutibiwa,Muhimbili ni kwa walala hoi.Kama dokta wa Muhimbili,anajifunzia kwa hawa watu,sio dokta tena.
Nakumbuka picha ya Super Model pale TEMEKE kwenye wodi ya waja wazito.

EPA,Meremeta,BoT towers,Richmond,Gulfstream 550 ,Kiwira,zinaweza kulipia gharama ya afya nchini.
Mwafrika hauna dignity ukiwa kwako nyumbani hasa kama hauna pesa.
Bora upige mabox Ulaya,ukiumwa utalazwa first class hospital,first class consultant,first class dentist.

Wazungu wanatutukana sisi kama Nyani kwa ajili ya baadhi ya matendo yetu.Uwezo tunao,tuko lazi kuiba hela na kuweka Ulaya wakati watu wetu wanalala chini.
 
Tukiendelea kuwalaumu viongozi hao hao kila siku tunakosea. Ukichunguza kwa makini jibu ni rahisi. Tatizo lipo kwa wananchi ambao wamewaweka viongozi hao katika madarka. Wananchi wana uwezo wa kubadilisha viongozi wasiowataka muda ukifika wa kuwabadilisha. Lakini mwaka nenda rudi, mnawachagua hao hao. Tutaacha kweli kulala chini kwa namna hiyo? La hasha!
 
Back
Top Bottom