Think big
Hiyo ndiyo tanzania baba,
Mafisadi wangekuwa na huruma jamani maana yote yanasababishwa na wao
IsayaMwita,
inawezekana kweli hiyo ndiyo Tanzania, lakini Je ni kweli hiyo ndio Tanzania yenye mTanzania anayeitwa Andrew Chenge? .. anayeitwa Yusuf Manji? .. Rostam Aziz? .. mtanashati JK? Kweli? au ndio Tanzania ya wale walalahoi tu!
Ukae ukijua Muhimbili ndio hospital yetu ya Taifa, yaani kiufanisi ndio kubwa kuliko zote! Sasa tujiulize za uko mikoani je? wilayani? ..
Mafisadi wao wanatibiwa nchi za nje UK, US, SA, Kenya na India hivyo hawaoni umuhimu wowote wa kuipatia Muhimbili na hospitali zetu nyingine vitanda vya kutosha na vitendea kazi muhimu.
Kulikuwa kuwe na mkutano wa waandishi wa habari kuhusu malalamiko ya madaktari pale leo hii.. sijui kuna mtu anajua kilichojiri?
Kulikuwa kuwe na mkutano wa waandishi wa habari kuhusu malalamiko ya madaktari pale leo hii.. sijui kuna mtu anajua kilichojiri?
Kulikuwa kuwe na mkutano wa waandishi wa habari kuhusu malalamiko ya madaktari pale leo hii.. sijui kuna mtu anajua kilichojiri?
Ndugu Asha,
Naomba nipingane na kauli yako ya kwamba hali mbaya katika Hospitali ya Muhimbili na Hospitali nyengine hapa Tanzania imesababishwa na Mafisadi. Hilo nadhani mimi ntalipinga.
Ni kweli ya kwamba hawa Mafisadi wamekwamisha kwa kiasi fulani maendeleo ya Taifa hususani katika kuboresha huduma za jamii na kufanya maisha yakawa rahisi kwa Mtanzania wa kawaida. Lakini tunaporudi katika Sekta ya Afya nadhani hapa Lawama haziwezi pelekwa kwa ile "List of Shame" na Mafisadi wengine ambao hawapo katika i le list, bali ni katika mipango mibovu ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mh. Jakaya Mrisho Kikwete kuboreasha huduma zote.
Ari Mpya, Kasi Mpya, Nguvu Mpya... Maisha bora kwa kila Mtanzania. Ni kwamba akiwa kama mwanasiasa, JK amehadaa na ameshindwa yatimiza yale ambayo amewaahidi Wapiga kura wake kuboresha maisha yao. Hapa hakuzuiwa na Mafisadi bali ni mipango yake mibovu katika kutekeleza Ilani iliyomuingiza madarakani mwaka 2005.
Mfumo mbovu wa Afya na Administration ya Kikwete kushindwa kusimamia hilo nadhani ni moja ya mambo ambayo yamesababisha hali kuwa mbaya sana katika Hospitali zetu na sehemu nyengine zinazotoa Huduma kwa Jamii.
Imekuwa kama Watanzania tumepata sehemu ya kulalamikia kwa hiyo inakuwa kila kitu ni Mafisadi, given a chance mimi ningeshauri tuwaponde mawe mpaka wafe lakini katika mambo mengine hatutakiwi kutafuta nani wa kumlaumu ila kujua nini sababu ya kushindwa kwetu na ufumbuzi unaweza kupatikana vipi!!! Kuna siku mvua haitanyesha kwa kipindi kirefu ama jua kuwa kali mno tutawalalamikia mafisadi!!!
Unasema maendeleo katika nyanja ya afya hayazuiwi na ufisadi. Ni mifumo na mipango na ufuatiliaji mbaya wa Kikwete administration.
Nakataa.
Definition yako ya fisadi inajumuisha wizi wa kina Chenge tu, wakati kuna ufisadi mwingine mbaya kama, au kupita, wa Chenge.
Rais, Mawaziri na tabaka tawala zima linapoenda India kutibiwa na hela yetu wakati sisi tunukufa kwa kuumbwa na mbu hospitali, huo ni ufisadi. Hujali.
Utajali vipi kufuatilia mipango ya maendeleo ya afya kama wewe hilo kwako sio tatizo: ukiugua unatibiwa India.
Kama mtu anaamini kwamba kuna madaraja mawili ya binadamu, yule anaestahili huduma bora ya afya, Waziri na Rais, na yule asiyestahili, Kalagabaho mlima kunde wa Gezaulole na Kuhani mpita njia, huyo mtu ni evil. Na hawa watu hiki kitu cha madaraja mawili ya binadamu, hii hulka evil, wanaiamini kwa vitendo: wakiugua wanaenda kutibiwa India kwa hela zetu!
Fisadi maana yake pia ni kiongozi evil.
Yusuph Makamba amepotosha watoto wa shule juzi aliposema maana ya fisadi kwenye kamusi ni mzinzi peke yake.
Huwezi kuwasafisha mafisadi wanaotibiwa nje huku sisi twafa kwa kutokujali kwao kwa kusema eti ni tatizo la mipango ya afya. Hawajali. Ni evil.
Kiongozi evil ni fisadi.
Hivi Mafisadi ndio walitakiwa kutoa yote haya katika Hospitali zetu kama ambavyo Bubu ameainisha...
Naomba Ufafanuzi.