Hali tete kwa wakulima, mbolea kg 50 yafikia 120,000

Kama unataka kulima kitaalam, ekari moja inatumia mifuko 3 ya kupandia, 3 kukuzia mara ya kwanza, na mitatu mingine kukuzia mara ya pili. Jumla mifuko 9. Utahitaji mbegu za kisasa nadhani kama kilo 40.

Gharama:

Mbolea sh 9×120,000=1,080,000
Mbegu sh 40×8,000 = 480,000
Kulima ekari 1 sh 80,000
Kupalilia mara 2 sh 100,000
Kuvuna, kupukuchua na kusafirisha sh 200,000

Jumla ya gharama sh 1,940,00

Mapato:
Mavuno magunia 20
Fedha magunia 20×24,000 = 840,000

Jumla ya mapato sh 840,000

Lazima uwe kichaa kulima mahindi.
Na kupata gunia 20 za mahindi kwa ekari moja sio kazi ndogo aisee. Ni ngumu sana
Sanasana ukijitahidi sana basi ni gunia 15, wengi wanaishia gunia 10.
Kwa Bei hizi za pembejeo, tusubiri maumivu tu.
Serikali ilipaswa hizi tozo wanazotoza wazielekeze kwenye kuongeza ruzuku kwenye mbolea
 
Watu wanataka mbolea ishuke ili iweje watu hawajajua tu kwamba kwa wastani mbolea inatakiwa ifike Tshs 250000/= kwa mfuko ili kukuza uchumi na kuwafanya watanzania akili iwasogee vzr.watu muda wote wanashangilia ujinga mtupu hii ya mbolea ni moja ya dawa nzuri nadhani tutaelewa tu na ndio tutajua sasa wapi kwa kupata haki.
 
Mkuu

Mbona kuna mdau alishusha uzi humu akisifia kwamba rais ameshusha bei ya pembejeo kwenye korosho kama mbolea na madawa kumbe alikuwa anawaandaa watu kisaikoloji?

Maisha kwa sasa yamekuwa magumu sana kuliko wakato wowote maana unamkuta mtu kamaliza chuo cha UDSM kazi ambayo zamani ilikuwa haiwezekani na ni mtaalamu wa uhandisi mawasiliano, sheria, mazingira, uahasibu nk..

Kupata kiwanja Dsm kwa sasa kwa viwango tofauti ni kuanzia milioni 2 ukubwa wa 15 kwa 10, 15 kwa 18, 20 kwa 20, 20 kwa 25) hadi milioni 100 eka moja hadi tano. Kwanja cha milioni moja, milioni moja na laki tano utapata nje ya Dar hasa wilaya ya Chalinze, Kisarawe, Mkuranga na kwa uchache baadhi ya sehemu za Bagamoyo kule Fukayosi, Makurunge na Mwavi lakini sio Bagamoyo karibu na mji au Kiwangwa au Msata huko ni balaa.

Maisha yataendelea kuwa magumu lakini wanasiasa wataendelea kuwakejeli wananchi mpaka uchaguzi ukikaribia wanajifanya kuja kuwapigia magoti wapiga kura kwa kuwapa zawadi ndogo ndogo kuwasahaulisha mateso waliyowapa kwa kushindwa kuwasikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi mara moja.
Nawachukia wana siasa haki ya mungu tena
 
Icha iwachome maana wakulima /WANYONGE walijisahau sana,mfugo wa mbolea ufika hata shilingi Laki tatu ili akili ziwasogee.
 
Kwa hiyo wewe mjuaji unatushauri nini mara baada ya kumaliza kunikandia? 😀
Tungeanzia hapa tungekuwa tumepiga hatua kubwa sana, kwa sababu ninayo mengi sana juu ya mada kama hizi zinazohusu kilimo na wakulima wa nchi hii.

Kama bado hujawahi kukutana na ushauri wangu ambao huwa ninautoa kila mara nikutananpo na mada hizi, ngoja niurudie kwa kifupi kwa faida yako na wengine.

"Kilimo na Elimu", maeneo haya mawili yalitakiwa yawekwe kwenye vipaumbele vya kudumu tokea nchi hii ipate uhuru wake, mwaka 1961. Maana yake ni kwamba, kila bajeti ya kila mwaka, maeneo haya yalipaswa kupewa kipaumbele cha juu kabisa katika bajeti ya serikali kila mwaka.

Si hivyo tu, maeneo haya yalitakiwa yawe na uongozi imara kwenye wizara hizo, uongozi unaosimamia mageuzi na matumizi sahihi ya raslimali kwenye wizara hizo.

Bado naamini, hata leo hii tukianza kuweka mkazo wa kuzibadilisha wizara hizo kwa kuzipa mkazo unaohitajika, ndani ya miaka mitano tutaanza kuona matokeo ya juhudi hizo.

Sasa ukitaka ufafanuzi wa nini kifanyike katika mazingira ya namna hiyo, nitakueleza kinagaubaga juu ya hayo nikiwa na muda huo.

Kama nchi tumefanya mzaha sana na maeneo haya nyeti ambayo ndiyo yangetuletea mabadiliko ya haraka ya maisha ya wananchi wetu; na kwa bahati mbaya tunaendelea kujifanya kama vipofu tusiojua ni nini tunatakiwa kukifanya, mara tunaimba viwanda, mara uwekezaji, mara madini, n.k., n.k.. Na kwa bahati mbaya, katika yote hayo tunayorukia, tunagusagusa tu, hakuna popote tunapofanya ili kupawezesha kuleta mabadiliko endelevu na ya kudumu.

Juzi juzi tulikuwa na "Kilimo Kwanza", na huko nyuma tulikuwa na "Kilimo ndio uti wa Mgongo......", "Kilimo cha Kufa na Kupona"; yote haya ni nani anakumbuka kulifanyika nini!

Ukiwa makini (serious) na mambo ya kilimo, jaribu kupitia walipoanzia Brazil katika kuleta mabadiliko katika sekta hiyo. Hata India wamebadili kilimo chao, siyo kwa maneno tu bali kwa kazi kubwa zinazofanyika katika kukibadilisha.

Sisi hapa tumebaki nyimbo tuuuu!
 
Magufuli alishaondoka pesa mlisema zitazagaa mitaani mpaka kwenye mitaro ya maji machafu mtazipata,vyooni mtazipata,kwenye madampo mtaziokota,wakija senene wanakuja na hela,wakija nzige watakuja na hela!Mbolea ishapanda bei mnalia,tozo mmelia,mafuta mmelia!Kiko wapi nyie wagalatia?mji wa asali na maziwa na mahrulain mlioufiria mtafika.
 
Wakulima watalima vipi kipindi hiki mbolea ambayo tulinunua kwa elfu 60 Sasa imefikia elf 95 laki mpaka laki na ishirini.

Sasa najiuliza itakuwaje kama Sasa hivi gunia la mahindi kwa eneo nililopo ni elf 24 wakati Bei ya mbolea ni laki na ishirini.

Kwamba unatakiwa kuuza gunia 5 Za mahindi ili kununua mbolea mfuko mmoja .

What a failed state!
Ngoja nikwambie kitu! Suala la mbolea lina siasa sana hapa nchini, si wizara husika wala si Serikali ambayo iko tayari kujikwamua kutoka kwenye matumizi ya haya mambolea ya chumvi chumvi ya viwandani, ambayo kisayansi hayana tija kwa wakulima na ardhi zao zaidi ya kuharibu rutuba ya asili kwenye ardhi na udongo wa nchi yetu. Hivi ni kwa nini wizara husika na hilo shirika la mbolea la Tanzania hawapigii upatu mbole ORGANIC!? Wewe ulishawahi kujiuliza swali hilo?

Kwa nini siku zote mazungumzo ni juu ya haya haya mambolea ya viwandani? Kuna nini hapa? Je hao watengenezaji wa haya mambolea ya chumvi chumvi ndiyo wenye vibali pekee vya kuuza haya mambolea yao hapa nchini pekee? Hata hao waagizaji na hilo shirika la kusimamia masuala ya mbolea hapa nchini halizungumzii hii mbolea ORGANIC, wao nao wamenaswa na huu mtego wa mbole za chumvi chumvi zenye kufubaisha mboji za ardhi na udongo wetu na hivyo kuharibu na kushusha uzalishaji wa mazao hapa nchini. Nauliza haya maswali kwa sababu, mimi binafsi najua kuna waagizaji wa mbolea nzuri za ORGANIC kwa muda mrefu lakini si wizara wala Serikali inawapigia upatu hawa waagizaji wa mbolea ORGANIC ambayo ni chakula rafiki kwa ardhi/udongo wetu na mimea pia. Wizara ya Kilimo na mawaziri wake na watendaji wote huko wizarani WAKE UP jamani muisaidie nchi hii in this area.
 
Wakulima watalima vipi kipindi hiki mbolea ambayo tulinunua kwa elfu 60 Sasa imefikia elf 95 laki mpaka laki na ishirini.

Sasa najiuliza itakuwaje kama Sasa hivi gunia la mahindi kwa eneo nililopo ni elf 24 wakati Bei ya mbolea ni laki na ishirini.

Kwamba unatakiwa kuuza gunia 5 Za mahindi ili kununua mbolea mfuko mmoja .

What a failed state!
Wakomae la sivyo serikali itafute pesa kwa ajili ya ruzuku maana hata ikifuta ushuru zote haiwezi kushuka chini ya 90,000
 
Tatizo la bei ndogo ya mahindi ni tatizo la miss divesification/ crop miss rotation au mono cropping kwa lugha rahisi. Hii inatokea pale wakulima wengi wanapoamua kulima zao la aina moja. Iwapo wakulima wengi wangejikita kwenye kilimo cha fursa, huenda wangelima mazao kama alizeti na ufuta ambayo yana bei nzuri sokoni na kulima mahindi kidogo kwa ajili ya chakula.
Wakulima wenyewe wamekariri kilimo ni mahindi tuu
 
kila mtu alitegemea hivyo maana ukishagusa tozo kwenye mafuta kuna impact kubwa sana kwa bidhaa nyingine kwani mafuta yanagusa karibu kila sekta ya uzalishaji.
Tozo za mafuta zinahusikaje na bei ya mbolea?

Kwenye mafuta tozo hazijaanza leo ona hapa 👇

IMG-20210906-WA0002.jpg
 
Magufuli alishaondoka pesa mlisema zitazagaa mitaani mpaka kwenye mitaro ya maji machafu mtazipata,vyooni mtazipata,kwenye madampo mtaziokota,wakija senene wanakuja na hela,wakija nzige watakuja na hela!Mbolea ishapanda bei mnalia,tozo mmelia,mafuta mmelia!Kiko wapi nyie wagalatia?mji wa asali na maziwa na mahrulain mlioufiria mtafika.
Magufuli hajawahi fanya chochote cha maana kwenye kilimo zaidi ya kuharibu bei za Mazao kwa hiyo futa ujinga wako hapa.

Sababu ya bei kupanda ni supply ndogo Duniani kote na njia pekee ya serikali kuwasaidia wananchi ni ruzuku sasa hiyo kitu ya ruzuku serikali ilijitoa toka 2015,alijaribu Kikwete lakini ilikuwa mzigo kwa wananchi.
 
Magufuli hajawahi fanya chochote cha maana kwenye kilimo zaidi ya kuharibu bei za Mazao kwa hiyo futa ujinga wako hapa.

Sababu ya bei kupanda ni supply ndogo Duniani kote na njia pekee ya serikali kuwasaidia wananchi ni ruzuku sasa hiyo kitu ya ruzuku serikali ilijitoa toka 2015,alijaribu Kikwete lakini ilikuwa mzigo kwa wananchi.
ndio maana unajiita opportunity cost kwa upumbavu uliokithiri.Maisha ni magumu sana kwa vipofu kama wewe!Subiria hela kwenye mitaro!
 
Tatizo la bei ndogo ya mahindi ni tatizo la miss divesification/ crop miss rotation au mono cropping kwa lugha rahisi. Hii inatokea pale wakulima wengi wanapoamua kulima zao la aina moja. Iwapo wakulima wengi wangejikita kwenye kilimo cha fursa, huenda wangelima mazao kama alizeti na ufuta ambayo yana bei nzuri sokoni na kulima mahindi kidogo kwa ajili ya chakula.
Wewe ni mjinga
 
Tuma salamu kwa watu watatu ukianza na mume wako mpendwa!
Tatizo mnakurupuka ku post mambo ya huyo jambazi ukifikir hamna rekodi zake wanawake huwa wasahaulifu sana we mama umesahau kama lile jambazi lilivamia clouds na mitutu bil camera lingeruka bado liliagiza vitu kwa mgongo wa walimu lile ni jizi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom