Hali kama hii, muda kama huu maaskofu na wachungaji pasingetosha!

Saa hizi wanakula kuku kwa mrinja kwenye maparokia yao yaliyozungukwa na kuta ndeeefu,mvinyo wa kutoka italy kwa pembeni wana shida gani hadi waandike waraka?,
mambo yao sasa yako super sana
 
Nyarwadhnyarwath
unamuonea tu,hivi hata wewe moyo wako kweli haukusuti?,
waraka awamu iliyopita ilikuwa karibu kila jumapili,what happened?,

mbona kimya.

Zile kelele za katiba mpya za maskofu ,kumbe ilikuwa kisingizio tu,

fuata trend utaona
 
Yeah,God is watching....

But ni aibu kwelilweli,maana unafiki uko exposed automatically.

There is no way anyone can make a coverup here,,

it is quite clear,it is about self interest not about God or whatever they call him/her/it
 
Maaskofu aina ya pengo na kilaini ni janga kubwa.Pole sana jakaya ulishambuliwa kwa nyaraka na matamko sababu ya dini yako.mie ni mkatoliki safi Ila nakiri kanisa linekosa mwelekeo
 
Kama ilivyo kwa Kenya ukabila unavyoitafuna ndiyo hivyo hivyo udini kwa Tanzania. Tofauti tu ni kwamba wakenya ubaguzi wao ni wa dhahili wakati Tanzania ni wa kinafiki wa chini kwa chini.
 
JUMBE nyingi za leo zimejikita zaidi kwenye siku yenyewe tu! Kuna nyakati sikukuu kama hizi jumbe ni za kuona mapungufu ya serikali tu,mtu unajiuliza swali,viongozi wa dini nao ni wanasiasa?
 
Ukitaka kupunguza idadi ya waislamu anzisha vita halafu uwaambie hii ni Jihad tunailinda dini yetu basi hapo hadi maprofesa utawapata, lakini wafate wakristo waambie wapiganie dini hata kichaa hutompata, maana dini itajipigania yenyewe kama ni kweli kuna dini.
 
Siku zote nilikuwa siamini kuwa kuna suala la udini Tanzania lakini baada ya ibada ya xmass ambapo hali mbaya ya maisha kutokana na serikali kupuuza misingi ya uongozi ambayo ni pamoja na kutii maazimio yaliyofikiwa na bunge ikiwa ni pamoja na na bajeti ya nchi na kusababisha nchi kwenda kwa matakwa ya mtu mmoja.Lakini cha ajabu hakuna kiongozi yeyote wa kikristo aliyekemea jambo hili lililo wazi hali iliyosababisha mimi nihisi kuwa .ni kwa sababu kiongozi wa nchi ni ni mkristo tofauti na kikwete ambaye walimkemea mara kwa mara kumbe tatizo lilikuwa ni uislam wake.Hii ni kwa sababu siamini kuwa Mkulu hajakosea sehemu yoyote kiasi cha kushauriwa aache jambo fulani na kuzingatia jambo fulani
 
Maoni na makemeo mengi ya maaskofu yalisukumwa na tofauti ya kiimani na kiongozi aliyekuwepo wakati huo na ndicho kilichowapa umaarufu mwingi.Kwa awamu hii hali ni tofauti maaskofu wamekaa kimya kwa sababu Rais ni imani yao.

Nilitegemea kusikia mengi kama vile kukemea ukanda, udini,ubishi na hali ya maisha mtaani.Infact watakuwa wamesikia kwa waumini wao au vyombo vya habari licha ya wao kulishwa na kulipwa na sadaka.

Kwa sasa watajaribu kuwaaminisha waumini wale matango pori,lakini itafika wakati unafiki utajichuja.
Labda ni mipango ya Mungu kutenganisha siasa na dini na hili pengine ni mwanzo tu wa kuonesha uhalisia wa viongozi wa dini aidha Masheikh au maaskofu wanafiki wanaojipendekeza kwa viongozi na serikali.
Ya Mungu apewe Mungu,ya Kaisari apewe Kaisari.
 
Back
Top Bottom