Ni jukumu la mitume, manabii, wachungaji na maaskofu kukemea Maovu hasa ya watawala

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
Kwema Wakuu!

Nikishasikia kiongozi wa kisiasa hataki viongozi wa dini wakemee Maovu hasa ya haohao watawala na kuingiza neno isichanganywe dini na Siasa, hapo napatwa na harufu ya uovu.

Hakuna haja ya uwepo wa dini ikiwa manabii, mitume, maaskofu, wachungaji na wote wanaohudumu kwenye madhabahu Kwa kile wasemacho kuwa wanahubiri neno la Mungu ikiwa watashindwa kukemea Maovu hasa ya wanasiasa.

Watumishi wa dini hiyo ni Job descriptions yenu. Boss wenu ni Mungu. Inashangaza muache kusikiliza amri na oda za kiongozi wenu alafu mnasikiliza na kuwatii wanasiasa.

Isaya anasema;
Isaya 58:1
[1]Piga kelele, usiache,
Paza sauti yako kama tarumbeta;
Uwahubiri watu wangu kosa lao,
Na nyumba ya Yakobo dhambi zao.

Inashangaza kazi ya kupiga kelele na kukemea Maovu mmewaachia wanaharakati ilhali hiyo ndio kazi yenu. Uanaharakati ni kazi ya manabii, mitume, na Makuhani.

Isaya alimfuata Daudi
Yohana mbatizaji alimfuata Herod's
Musa alimfuata Farao.
Elia alimfuata Yezebeli.
Na wengineo wengi.

Kazi yenu wachungaji sio kuwafundisha Watu kuwa wapole na kutii mamlaka hata Kwa mambo ya udhalimu. Jukumu lenu ni kuwafundisha Watu wapendane, waache uovu lakini pia kuungana kuwapinga waovu hasa waovu wenye nguvu.

Kama ninyi ambavyo mtashughulikiwa na sheria za nchi pale mnapovunja sheria ndivyo hivyohivyo nanyi ni jukumu lenu kukemeea na kuwaandama viongozi wa kisiasa ambao ni waovu.

Sio mnakemea mara moja ili kuzuga alafu ndio imeisha. Hapana! Kemeeni mpaka Jambo hilo liondoke.

Yesu anasema amewapa uwezo wa kutoa pepo, yaani kupambana na mapepo yote bila kujali yapo katika nafasi ipi na nguvu gani.
Kutoa pepo sio wale wanaogaragara Kwa kupagawa na maruhani. Bali kutoa mapepo wachafu kwenye vichwa vya watu wakiwepo viongozi wa kisiasa.

Mnawaogopa Wakati hiyo ndio kazi yenu.
Ni Sawa na Mwanajeshi aogope Kufa au kupigwa risasi katika uwanja wa vita.

Kumtii Mungu ni pamoja na kukemea waovu na uovu.
Kumtii shetani ni pamoja na kukemea Waliowema na Wema.

Tunaposema maadili ambayo mnayatoa Huko Makanisani na misikitini ni pamoja na kukemea Waovu hasa wale wa juu kule.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Tusikae kimya sasa kusubiri miaka 10 ijayo Rais wetu aandike Kitabu cha kujutia kuingia mkataba huu mbovu wa Bandari, tumkosoe mapema ili akija kuandika kitabu hicho aseme nilishauriwa ila nilikataa Ushauri"-Baba Paroko wetu leo 27/08/2023
 
Hayupo anayejielewa atakaye nyamaza tuwatazame vipofu wakitutafuna mpama mifupa.
 
Huduma tano za waliopo hapa kwetu, wanakosa msimamo kwasababu wanachanganya wito na biashara.. na imefikia kipindi wanabidi wawe na urafiki na Kaisari ili kulinda michongo yaoo.. hiyo inawaondolea ujasiri wa kukemeea mauvo
 
Back
Top Bottom